Waziri Mkuu fuatilia haya mabasi ya mwendokasi, siku za weekend tunateseka

Carlos Valderrama

JF-Expert Member
Dec 27, 2014
664
240
Wana JF.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wananchi wanapata usumbufu mkubwa mno kutoka kwenye haya mabasi ya mwendokasi siku za weekend, Jumamosi na Jumapili.

Hawa wamiliki wa haya mabasi wanatumia mabasi machane mno wananchi wanajazana kwenye vituo kwa wanasubiri mabasi zaidi ya masaa mawili mpaka matatu halafu tunaita mwendo kasi.

Kama wanataka kupumzika siku za weekend bora waruhusu daladala ziendelee kutoa huduma kwa wananchi.

Vituo vya Manyanya, Mkwanjuni, Morocco, Usalama, Magomeni, Fire, Manzese, Leo mida ya asubuhi vilikuwa vimejaa abiria wengi sana na wengi wao walichewa makazini.
 
Watu wengi wanalalamika kuhusu hili serikali wafanye uchuguzi wao kuondoa huo usumbufu.
 
Huo usumbufu kweli upo na nimeshakumbana nao, ni wakati sasa mamlaka husika kulifuatilia kwa umakini, kiukwel huu ni uonevu ba kwa bahat mbaya ukishaingia kituoni ndo imekula kwako...
 
Kwakweli mimi nashukuru hata umesema ndugu yangu. Siyo weekend tu, hata mchana kwenye saa tano siku za weeki magari shida sana. Wewe fikiria mwanzoni watu wenye magari walishaanza kuacha magari nyumbani na kupanda mwendokasi, ila imekuwa balaa, ni kukanyagana, kugombania, kukaa vituoni muda mrefu. Mfano Kimara, Ubungo na Posta ya Zamani na Nyerere Square shida sana, nani aache gari nyumbani kwa adha hii. Kiukweli na hivi wamefuta ruti za daladala, tutapata shida sana. Nadhani wao hawafuatilii ili kujua kero zinazowakabili watumiaji wa magari haya.
 
Hilo suala ni sugu nilishawahi piga simu kadhaa kwa huduma kwa wateja; nao wakasema bosi wao amekuwa siyo msikivu kwa hilo akanipatia namba yake... Kwa kweli hili ni tatizo.. Unalipa hela lakini unakuwa mtumwa.. "STRANGE'
 
Huu mradi ni kama unaenda kufa kama hatua stahiki hazijachukuliwa.
 
Wana JF.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wananchi wanapata usumbufu mkubwa mno kutoka kwenye haya mabasi ya mwendokasi siku za weekend, Jumamosi na Jumapili.

Hawa wamiliki wa haya mabasi wanatumia mabasi machane mno wananchi wanajazana kwenye vituo kwa wanasubiri mabasi zaidi ya masaa mawili mpaka matatu halafu tunaita mwendo kasi.

Kama wanataka kupumzika siku za weekend bora waruhusu daladala ziendelee kutoa huduma kwa wananchi.

Vituo vya Manyanya, Mkwanjuni, Morocco, Usalama, Magomeni, Fire, Manzese, Leo mida ya asubuhi vilikuwa vimejaa abiria wengi sana na wengi wao walichewa makazini.

Ni kawaida hiyo kuwa na mabasi machache siku za weekend, mbona wewe hauendi kazini/shuleni kila siku mpaka Jumapili? Sasa kama yakifanya kazi yote kila siku ni lini yatapelekwa gereji kwa matengezo na marekebisho ya hapa na pale? Wewe huyo huyo Jumatatu unataka ukifika Kituoni ukute basi safi na linalokwenda bila ya kuharibika njiani sasa unafikiri miujiza ndiyo inayotoa hiyo huduma? Weekend na siku kuu kwa kawaida siyo siku ya kazi hivyo hawapaswi kuweka mabasi yote br. huwo ni utaratibu wa kawaida kabisa na unatumika Dunia nzima, vinginevyo chukua taxi!
 
Sio weekend tu bali hata siku za kawaida ni usumbufu mkubwa, ni kama vile hawawezi kuusimamia huu mradi,
 
Wana JF.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wananchi wanapata usumbufu mkubwa mno kutoka kwenye haya mabasi ya mwendokasi siku za weekend, Jumamosi na Jumapili.

Hawa wamiliki wa haya mabasi wanatumia mabasi machane mno wananchi wanajazana kwenye vituo kwa wanasubiri mabasi zaidi ya masaa mawili mpaka matatu halafu tunaita mwendo kasi.

Kama wanataka kupumzika siku za weekend bora waruhusu daladala ziendelee kutoa huduma kwa wananchi.

Vituo vya Manyanya, Mkwanjuni, Morocco, Usalama, Magomeni, Fire, Manzese, Leo mida ya asubuhi vilikuwa vimejaa abiria wengi sana na wengi wao walichewa makazini.
PM ana kazi nyingi kwani sumatra hawawezi???PM ana mishe za kuhamia dom
 
Hata kama tatizo la kuwahi unakofika endapo unapata Gari kwa wakati....jipu ni uhaba Wa mabasi mchana na weekend days; kuchelewa kufika kwa Gari ktk vituo vikuu hali inayosababisha foleni na virugu vituoni...asbh na jioni...utadhani ni vita...kila MTU kutaka kuwahi seat, yani shida , kama huna ubavu huingii na ukiingia ni kwa maumivu ....Je hii ndo plani ya mabasi haya? Nilidhan tatizo la kuparamiana na kuibiana vitu wakati ukipanda !!!
 
Ni kawaida hiyo kuwa na mabasi machache siku za weekend, mbona wewe hauendi kazini/shuleni kila siku mpaka Jumapili? Sasa kama yakifanya kazi yote kila siku ni lini yatapelekwa gereji kwa matengezo na marekebisho ya hapa na pale? Wewe huyo huyo Jumatatu unataka ukifika Kituoni ukute basi safi na linalokwenda bila ya kuharibika njiani sasa unafikiri miujiza ndiyo inayotoa hiyo huduma? Weekend na siku kuu kwa kawaida siyo siku ya kazi hivyo hawapaswi kuweka mabasi yote br. huwo ni utaratibu wa kawaida kabisa na unatumika Dunia nzima, vinginevyo chukua taxi!
je ni kweli hayo mabasi yaliyopaki yard yote yanafanyiwa service? au yote yanafanyiwa usafi kiasi kwamba haiwezekani gari kutoka?
kiukweli ni kwamba kama huyu mwendesha mradi ni kama amepewa "viatu vikubwa kuliko mguu wake" hivyo vinampwaya tusiwe wanafki kwenye ukweli
 
Unapaswa uelewe kwamba weekend inaitwa weekend kwa sababu, kwa nini haulalamika kwamba Maduka yamefungwa Jumapili Kariokoo na kwamba hauwezi kufanya manunuzi? Au kwa nini haulalamiki kwamba Posta hawafungui Jumapili ili ukaposti Barua? Huu ni utaratibu wa kawaida Dunia nzima kwamba weekend ni tofauti na siku za kawaida na kwa kuwa hawa wanafanya biashara hauwezi kuweka mabasi yote yatumike kila siku ni lazima wapumzishe mengine, kama nilivyokwisha kusema kama unahitaji huduma ya haraka weekend chukua Taxi lkn haiwezekeni Mabasi yaendeshwe kwa matakwa ya kila mtu, kesho mwingine atasema akitoka kwenye Harusi usiku hakuna basi wkt anayaona mengi yamepaki yadi, naye atataka yafanye kazi mpaka saa nane usiku!
 
Hizi hoja zako unazong'ang'ania hazina mashiko. Biashara inatakiwa iwe adjusted kutokana na demand. Hao wenye mabasi hawasafirishi watu bure. Kama kuna tatizo la service ni wao watafakari watafanya nini ili huduma zisikwame. hizi mentality ndio zinakwamisha nchi yetu. Hii dhana ya dunia nzima ni ya kukariri. Watu wanaenda shopping weekend. Unataka watembee kwa miguu. Tatizo kubwa ni uchache wa magari. Hawa hawaangalii uwingi wa watu na ndio hasa tatizo la monolopy. Kwenye hizo lane ikitokea kampuni nyingine, watapata akili.
 
Hivi hii ni weekend tu? Kila siku za kazi huwa naona bonge la nyomi pale kimara mwisho ambalo hata mabasi 20 yakifika kwa pamoja hayawezi kuwabeba wote wakaisha.
 
Wamezd,, kuna madreva wa hayo magari wanaweza ondoa gari kituon likiwa Tupu wakati abria wa ruti yake wapooo,,, swali huwa wanafanyiwa mental fitness kabla ya ajira?
 
Back
Top Bottom