Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Wana JF,
Nikiwa nimesomea Uhandisi ujenzi wa barabara ingawa sipo kwenye ujenzi tena, nimelipokea kwa furaha sana tangazo la serikali kuwa hatimaye wanahamishia DODOMA Makao Makuu ya taifa la Tanzania ambayo ni zaidi ya miaka 40 tangu tutangaze kuhamishia huko.
Naiomba tu Serikali yetu ya awamu wa ya tano kuchora mapema barabara za mduara kuzunguka Dodoma walau mbili. Ukiangalia miji mingi mikubwa wana hizo RINGS kuzunguka miji yao na mara nyingi zinakuwa ni Highway Roads au Express roads.
Hizi barabara zitawasaidia ambao hawataki kupita Dodoma mjini hasa Maroli kuuzunguka mji na kutokusabisha foleni za magari pamoja na zenyewe pia kuingia kwenye foleni za magari kama ulivyo mji wa Dar es salaam.
Najua sasa hizi kuna maeneo tayari watu wameshajenga na hivyo serikali itabidi ilipe fidia ila ninaamini hawajajenga wengi na hivyo kuwahamisha haitakuwa gharama kubwa. Ila mara tu Serikali na Mabalozi wakihamia basi utafumuka msululu mkubwa sana wa magari mjini Dodoma na itakuwa taratibu tunahamisha shida za Dar kuja Dodoma.
Tukichelewa kuhamisha watu na kusimamisha ujenzi kwenye maeneo zitakapopita hizi RINGS za barabara kuzunguka dodoma (napendekeza ziwe barabara 2 kwa kila upande na upana uwe 3.5m kila barabara ambayo inaleta upana wa min. 20m) huko mbele gharama zitakuwa kubwa na tutapata shida kama ilivyo leo mtaa wa Uhuru Dar es salaam.
Natamani watu wa CDA wawe wameshalifanyia kazi na kama bado basi wafanye haraka ili liingizwe kwenye Master Plan ya DODOMA na watu wa Urban Planing wakisaidiana na wizara ya ujenzi pamoja na TanRoads.
Kwenye picha nimeweka tu kwa haraka muonekano wa hiyo miduara au RINGS kuzunguka Dodoma ila wataalamu wa Urban Planing watajua ni nini nilimaanisha na kuziweka kwa usahihi zaidi wakishirikiana na watu wa Road designing.