GRAMAA
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 1,155
- 3,399
Leo bungeni kwenye kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe aliuliza maswali ya msingi sana kwa Waziri Mkuu. Maswali hayo yakiwepo.
(i) Ni lini Serikali ya CCM itaruhusu vyama vya upinzani vifanye mikutano yao ili vijiandae na uchaguzi mkuu wa mwaka huu?
(ii) Kwanini Serikali ya CCM imejipanga kuleta ubabe kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu?
(iii) Waziri Mkuu haoni umuhimu wa kuwepo na tume huru ya uchaguzi ili kuufanya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa huru na haki?
(iv) Je, ni sheria ipi Serikali ya CCM imetumia ili kuzuia mikutano ya kisiasa?
Majibu ya waziri mkuu yalikuwa ni tofauti kabisa na kile alichoulizwa.
Sasa sijui hakuelewa maswali?
Alifanya makusudi?
Au ndiyo mfumo unambana inabidi tu ajibu simple simple tu kwenye mambo ya msingi.
Hongera mh. Mbowe kwa maswali ya msingi japo kuwa yamekosa majibu ya msingi.

Freeman Mbowe (MB): Ni lini mtaruhusu vyama vya siasa vifanye wajibu wake wa uenezi ili kujiandaa na Uchaguzi Mkuu na Serikali ina mpango gani wa kuwezesha taifa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ili uchaguzi huu uwe wa haki na halali.
Waziri Mkuu: Kwanza nataka nikanushe Serikali haiongozi kibabe, Mbowe ni kiongozi tunazungumza na kubadilishana mawazo na lengo ni kulifanya taifa liwe salama, Watanzania wanahitaji maendeleo na hakuna Mbunge au Diwani aliyezuiliwa kufanya mikutano kwenye maeneo yake.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa: Vyama vya siasa havijazuiliwa kufanya shughuli zake ila tumeweka taratibu muhimu kwa wale viongozi waliopata ridhaa kwenye maeneo yao, ratiba za uchaguzi zitatolewa na kueleza lini shughuli za kampeni zitaanza.
Waziri Mkuu: Tume ya Uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa sheria na chombo hiki hakipaswi kuingiliwa na chombo chochote awe Rais wa Nchi au chama chochote, chombo hiki kipo huru.