Waziri Mkuu awataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko Serikali.

Ametoa kauli hiyo jana jioni wakati akifungua Kikao Kazi cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema ni vema viongozi hao kabla ya kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo halitaleta athari za kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za wizara zao.

Pia amewataka viongozi hao wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili kuithibitishia jamii kuwa Rais Dkt. John Magufuli aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao kiutendaji.

“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiwekee utaratibu wa kusikiliza hoja na shida za Wabunge na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.

Pia amewataka wafanye ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Waziri Mkuu amesema Mawaziri na Naibu Mawaziri wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

Pia wasimamie utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.

Chanzo: ITV
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
12,781

huyu kiboko yake DAB tu!
 
Nelson Masaduki

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
348
500
afadhali amewaambia. Maana nilisikia juzi juzi hapa kuwa kila MKUU WA MKOA AHAKIKISHE MWISHO WA MWAKA ANA VIWANDA 100 :)
 
kijana wa leo

JF-Expert Member
Nov 28, 2011
2,828
2,000
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko Serikali.

Ametoa kauli hiyo jana jioni wakati akifungua Kikao Kazi cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema ni vema viongozi hao kabla ya kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo halitaleta athari za kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za wizara zao.

Pia amewataka viongozi hao wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili kuithibitishia jamii kuwa Rais Dkt. John Magufuli aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao kiutendaji.

“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiwekee utaratibu wa kusikiliza hoja na shida za Wabunge na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.

Pia amewataka wafanye ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Waziri Mkuu amesema Mawaziri na Naibu Mawaziri wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

Pia wasimamie utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.

Chanzo: ITV
Upumbavu wa hii nchi yetu ni kwamba kila kiongozi anatakiwa afanye kazi kumfurahisha rais na sio kwa mujibu wa matakwa ya wapiga kura, tumemfanya rais zaidi ya malaika, yani kama mtu asiyekosea katika jambo lolote lile, rais amekua ndio muongozo wa kila kitu....hatuna dira ya nchi, viongozi wote malengo yao ni miaka 10,hakuna kiongozi anayewaza juu ya watoto wake, wajukuu zake wataishi katika nchi yenye sera ipi?? na ndio mana unaweza kukuta waziri mzima ila hajui amshauri mwanae au mwanafunzi wa shule ya msingi kuja kusomea nini, hakuna mtu anayejua baada ya miaka 20 au zaidi Tanzania itakuwaje....
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,080
2,000
Yeye mwenyewe alishawahi sema serikali imeagiza mitambo ya kukagua madawa ya kulevya hata wakipita tu nje ya nyumba yako wanagundua!!
Sijui aliishia wapi?
Nae ni mropokaji mzuri tu
 
Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,591
2,000
Mama Samia Sulluh alitakiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Tanzania na Baba John Magufuli awe rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.....

Kassim Majaliwa awe Makamu wa rais wa Tanzania...
images
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,256
2,000
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko Serikali.

Nilishasema humu ndani, Kassim Majaliwa ndiye aliyefaa kuwa Raisi wa nchi hii, na Magufuli kuwa Waziri Mkuu. Lakini kuwa na Majaliwa kama Waziri Mkuu na Magufuli kama Raisi ni sawa na pikipiki kuvuta lori. Inaweza, lakini ni tatizo.

Na ukweli ni kwamba hekima na busara za Majaliwa katika uongozi zinazimwa sana na Raisi Magufuli - Majaliwa kwa sasa hatendi kwa kutumia uwezo wake wa kiuongozi asilimia kwa asilimia 100% kwa sababu yuko chini ya kivuli cha Magufuli

Fact: Majaliwa is not exerting his full leadership potential because he is constrained by the President

The best next thing for Tanzania after the discovery of Tanzanite is to have Majaliwa as president of the country. And I am not talking of 2020 elections here. CCM take note.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom