Waziri Mkuu awasimamisha Wakurugenzi Saba wa Tume ya Umwagiliaji akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Wakurugenzi Saba wa Tume ya Umwagiliaji akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Waziri Mkuu Majaliwa amechukua hatua hiyo wakati wa kikao na viongozi wa tume hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina, Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Mawaziri, Naibu Mawaziri na Makatibu Wakuu.

Aidha, Waziri Mkuu amemwagiza CAG, Profesa Mussa Assad kufanya uchunguzi wa kina wa ubadhirifu wa fedha za umma unaodaiwa kufanywa na Wakurugenzi saba wa Tume ya Umwagiliaji waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi huo.
 
Back
Top Bottom