Waziri Mkuu awachimba mkwara UHAMIAJI

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameichimba kwara mzito Idara ya Uhamiaji nchini akiituhumu kuruhusu uingizaji holela wa wageni mkoani Kagera.
Amesema ongezeko kubwa la kiholela la wageni kutokea mipaka ya mkoa wa Kagera ni hatari kwa ustawi wa mkoa na hatari kwa taifa.

"Uhamiaji mmekuwa chanzo cha kuingia watu kiholela. RIO (Mkuu wa Uhamiaji wa Mkoa), na wenzako wa wilaya mbadilike mara moja kulinda nchi,"

Alisema uingiaji holela wa watu unaleta matatizo makubwa ikiwamo kuhatarisha usalama wa nchi, kuongeza idadi ya watu na ongezeko la bajeti hivyo kuathiri utoaji wa huduma kwa Watanzania.

Alisema mipaka ya nchi inapaswa kulindwa na kudhibitiwa. Aidha, alisema kumekuwa na mauaji ya wananchi Watanzania katika ranchi ya Missenyi ambayo kuna mifugo kutoka nje.

"Serikali isingependa kurejesha ile operesheni ya mwaka 2012 na 2013 lakini Ikibidi tutaanzisha tena,"

Source:HabariLeo
 
Back
Top Bottom