Waziri mkuu awachambua CHADEMA; Lema amtuhumu kudanganya

Katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu leo asubuhi mh.Waziri mkuu amesimulia kilichojiri katika mauaji ya Arusha na kwa mujibu wa maelezo yake yameonesha kuituhumu CHADEMA kuwa ni chanzo cha mauaji ya raia kwenye maandamano,amesema kuwa mh.Godbless Lema ni mtu wa fujo fujo hivi na alianzisha fujo kwenye kikao cha pili cha baraza la madiwani halmashauri ya Arusha.
Mwisho mh.Pinda kawashauri CHADEMA kuunda chama kitakachoaminiwa na wananchi kuongoza taifa hili chama chenye kuleta amani.
Wakati huo huo mh.Godbless Lema atumia mwongozo wa Spika kumtuhumu mh.Waziri mkuu kuwa kalidanganya bunge.
Kutokana na maelezo ya Pinda na IGP Mwema kutofautiana inaonesha wazi Pinda amebaka swali na haina umuhimu wa kumjadili sababu Tunajua tukio zima la Arusha.
 
Tuliytegemea hayo mana kma huna upeo na unasubiri tui kuambiwa ndio utaamini kila kitu. Waliouwa raia rusha nia CDM au polisi?
Je polisi waliamriwa na nani? ndio majibu tunayotaka.
 
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu leo asubuhi mh.Waziri mkuu amesimulia kilichojiri katika mauaji ya Arusha na kwa mujibu wa maelezo yake yameonesha kuituhumu CHADEMA kuwa ni chanzo cha mauaji ya raia kwenye maandamano,amesema kuwa mh.Godbless Lema ni mtu wa fujo fujo hivi na alianzisha fujo kwenye kikao cha pili cha baraza la madiwani halmashauri ya Arusha.
Mwisho mh.Pinda kawashauri CHADEMA kuunda chama kitakachoaminiwa na wananchi kuongoza taifa hili chama chenye kuleta amani.
Wakati huo huo mh.Godbless Lema atumia mwongozo wa Spika kumtuhumu mh.Waziri mkuu kuwa kalidanganya bunge.

Namuheshimu sana Mtoto wa Mkulima mwenzangu lakini katika hili hajasema ukweli kabisa. Siasa za Bongo bwana wee acha tu, au alitaka Batilda ashinde ndiyo aseme Lema ni mtu mpole, msikivu na mzalendo?.

Sasa nimeelewa :angry:
I HAVE TO HATE THE GAME AND NOT A PLAYER.
 
Duuu, wakuu alichosema ndio msimamo wa serikali.... kwakifupi mnazidi kujua serikali yenu jinsi ilivyo!!!
 
hizo zako nindoto za mchana za alinacha ila jipe moyo ila chadema kutawala nakuongoza nchi hii msahau milele chadema haitoweza kushinda uchaguzi na kuongoza taifa hili,hata hao chadema wenyewe wanalijua hilo,msinichukie huu ni mtazamo wangu.


Mkuu kama wewe ni miongoni mwa wale walio kwenye payroll ya CCM kwa ajili ya kutumika kuja humu kwenye mitandao kuwaondoa watu katika hoja za kitaifa, sawa endelea hivyo na unayo sifa ya kuwa hivyo, ila kama wewe ni miongoni mwa watu kama mimi tunaonunuwa umeme wa sh elfu kumi na kuambuli unit 20 kwh, kulipa ada ya mtoto ni shughuli pevu, ninamuomba mungu kama magonjwa basi niwe napata ugonjwa wa maleria na kuhara tu, maana kama nikipata ugonjwa utakaohitaji gharama ya sh laki tano Kutibiwa basi hapo ndio mwisho wa maisha yangu, sentensi hii ndio maisha halisi ya Wantanzania asliimia 90%, sasa basi kama na wewe upo kwenye category hii kuishabikia CCM ni sawa na kwamba wewe ni mfu ingali upo hai. mimi niko tayari kuiunga mkono CCM kama itawapa wananchi maisha bora iliyowaahidi, lakini imekuwa kinyume chake, kwa sababu hiyo nina kila sababu ya kukisapoti chama mbadala ninachoamini kinaamanisha kinachosema. wewe endelea na kejeri zako lakini mimi nakuhakikishia kama litatokea sharti la kupiga kura kati ya kuchaguwa CCM au kuchaguo kifo, mimi nitachaguwa kifo. PERIOD.
 
tatizo watu wanasafishana na kutaka kujiweka salama machoni pa watu kumbe ndo wnaharibu zaidi, Pinda ukweli ni kuwa amekuwa daraja kati ya wakulima na mafisadi, ila hana ata aibu kusifia mauaji ya arusha! najua kuwa PEOPLE POWER itafanya kazi, mda si mrefu wao wajiwekee matumaini ambayo hayapo, nchi ishawashinda umeme, maji, mfumuko wa bei, everything is out of control. police nao wakiitwa ni mabomu tu wanajua! tutaanza na mapolisi huku mitaani we ngoja!
 
Anajikanyaka tu!!hii impromptu questions and answers session naona inamshinda sasa!
 
kama zito alimtuhumu karamagi kuwa kalidanganya bunge akawa suspended, huyu kamtuhumu PM itakuwaje? au kwa jibu la spika ndio yameisha?
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt; Miss Judith hayajaisha Spika Makinda amemtaka mh.Lema awasilishe hoja yake kwa maandishi ili kuona wapi Waziri mkuu amedanganya.Vile vile Pinda amekubali hoja ya Mbowe uchunguzi huru ufanyike<br />
<br />
Ninavyofahamu mimi ni kuwa wabunge wa CCM hasa wa viti maalum watashupalia kuwa Pinda kadhalilishwa lakini mh.Lema aliuliza swali tu,sasa ikiendelea hivi wa kusulubiwa atakuwa mh.Lema.
 
hamna jipya katika hayo aliyoongea pinda kwani ndio msimamo wa serikali yake ya kidhalimu
 
Baada ya waziri Pinda kutoa ile taarifa ya kile kinyang'anyiro cha umeya wa jiji la Arusha then Mbunge wa chama cha Chadema Mh.Godbless Lema kudai mweshimiwa waziri amelidanganya bunge, then muheshimiwa spika mama Anna Makinda amemtaka ndugu Lema hadi tarehe 14 ya mwezi huu awe ameshawasilisha barua ya kudhibitisha kua waziri mkuu bwana Mizengo Pinda amelidanyanga bunge.

Kwa mtizamo wangu naona kama wabunge wa chama cha CCM kuna kulindana hapa na kuukandamiza upinzani bungeni, lakini natumaini bwana Lema yeye ndiye anajua mustakabali wa yaliyojiri pale Arusha kuhusiana na kinyang'anyiro hicho na natumaini barua itawasilishwa hiyo tarehe 14 kwa maelezo ya kina kabisa kwakua hata sisi tunajua yaliyojitokeza pale Arusha kwenye kinyang'anyiro kile bwana Pinda naona katika taarifa aliyopewa inautata.

Nawasilisha.
 
Mimi sioni mantiki ya Pinda kuegemea maelezo ya upande mmoja(maelezo ya Polisi)
Kwa nini asiamue kuunda chombo huru ambacho hakitaegemea chama chochote kuchunguza chanzo cha vurugu za Arusha?kwa nini Pinda asikiri kuwa jeshi la Polisi lilifanya makosa,mbona kule mbarali waliua?
 
Pinda hajakosea... ameambiwa amesema uongo, sasa ulitaka akubali tu kwasababu yupo CCM?

I hate bunge la sasa linavyoendeshwa lakini tusije tukafikia wakati kwamba yoyote anayepinga au kutoa challenge kwa wabunge wa chadema bungeni basi awe mnyanyasaji

Nina imani Lema atakuja na exhibits zitakazotosha

Lets cool down a little bit na haya ma whining and moaning
 
TAmemuambia aandike, ili asulubiwe vizuri, umesahau kilicho mpata zitto ?

Ungeeleweka zaidi ungesema 'kilichoipata ccm kwa kumtoa Zitto?'

Amini usiamini ndicho kinachowasumbua sasa hivi na ndio maana Makinda anakwepa kwa kila mbinu wasitoe mtaji mwingine kwa kumtimua Lema. Nothing will happen to Lema, mark my words
 
nilisema na ntaendelea kusema kuwa ni bora LOWASSA KULIKO PINDA nikandieni ila ukweli ndio huo
 
Back
Top Bottom