Waziri mkuu atangaza vita na wauza dawa za kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu atangaza vita na wauza dawa za kulevya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wikolo, Jun 27, 2012.

 1. w

  wikolo JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ametangaza kiama kwa vigogo wa dawa za kulevya na kuwataka watafute kazi nyingine za kufanya vinginevyo siku za kukamatwa kwao zinahesabika.Pinda alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya kimataifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya.

  Alisema tatizo la dawa za kulevya bado linazidi kuwa kubwa , licha ya juhudi zinazofanywa na vyombo vya dola katika kuwakamata. Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali iko katika mchakato wa kuanzisha chombo huru kitakachokuwa na uwezo wa hali ya juu wa kupambana na dawa za kulevya.

  “ Ole wenu mnaoendelea kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, ni suala la muda tu , tumejipanga na tutawakamata tu,” alisema alisema Pinda katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi. Alisema biashara ya dawa za kulevya inakithiri kwa sababu ya tamaa ya baadhi ya watu kutaka utajiri bila ya kufanya kazi halali.

  Aidha waziri mkuu huyo pia, alizungumzia pia tatizo la bangi ambapo alisema, matumizi yakebangi yanaendelea kuwa makubwa kutokana na kulimwa kwa wingi katika baadhi ya mikoa.
  “ Nawataka viongozi wa mikoa inayolima bangi kudhibiti kilimo hicho ili wananchi wajishughulishe na kilimo cha mazao ya chakula na biashara yenye kuwaletea wananchi maendeleo,” alisema.

  Pinda alisikitishwa na matukio yaliyoanza kujitokeza ya baadhi ya wanawake kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.


  “ Kama wanawake tunaowategemea katika kujenga maadili ya vijana nao wanakamatwa basi tatizo hili sasa ni kubwa na tunatakiwa kujipanga zaidi kulidhibiti,” alisema Pinda.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema urefu wa mipaka ya nchi yetu na kukithiri kwa rushwa miongoni mwa watendaji wa Serikali ni changamoto inayoikabili Serikali katika kupambana na biashara hiyo.


  Alisema licha ya changamoto hizo, serikali imejipanga kuendelea kupambana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa kadiri ya uwezo wake wote.

  Kwa upande wake, Kaimu Kamishina wa Tume ya Kuratibu na kudhibiti wa Dawa za Kulevya, Aida Tesha alisema, tangu Januari hadi Mei mwaka huu, jumla ya kilogramu 234 za dawa aina ya Heroine zilikamatwa.

  “ Kiasi hicho ni kikubwa kukamatwa katika kipindi hicho cha miezi mitano, zamani kiasi kama hicho kilikamatwa katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu,” alisema Tesha.
  Alisema ongezeko la kukamatwa kwa wahusika wa dawa za kulevya kumetokana na ushirikiano wanaoutoa wananchi kwa Jeshi la Polisi.

  Source: Mwananchi

  Hivi kweli unaweza kupambana na wauzaji wa madawa ya kulevya kwa kauli kama hizi? Kuna mwingine aliwahi kusema kwamba ana majina ya wahusika wote na akawataka waache mara moja! Kama majina yapo kwa nini hayafanyiwi kazi na badala yake tunaendelea kupewa kauli kama hizi? Au nalo limeshakuwa kete ya kisiasa?
   
 2. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  kila siku wanatoa hizi kauli hatuoni lolote..waache porojo hawa watu.......
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kwani mbona mkulu alituambia list ya wauza madawa ya kulevya anayo mezani imekuaje hadi leo??????
  au list ililiwa na panya?????
   
 4. King2

  King2 JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hana lolote Mnafiki huyo lile kontena la madawa ya kulevya lililokamatwa kusini na akina binti wa Liyumba kesi yake mbona Kimya hadi leo.
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  wimbo uleule, waimbaji walewale, hadhira ileile
   
 6. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hizi kauli wakati mwingine ni matatizo. Tangu lini tumanza kuasikia hivyo? je ili kumkamata mwizi unahitaji kutangaza? orodha ilipelekwa kwao (rais), wanawajua kwa majina na wakati mwingine wanapokea misaada yao na kuipeleka katika majimbo yao. Upo pia uwezekano ndizo ziliwafanya wakashinda katika majimbo yao.

  Inasikitisha kiongozi mkubwa kwenda kuwatishia nyau watu wanaoangamiza taifa ulilopewa dhamana ya kuliongoza. Please stop such kind of jokes.
   
 7. v

  vngenge JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Anyamaze tu. Asubiri muada wake wa kupumzika tushachoka na hizi single
   
Loading...