Waziri Mkuu ataka kuunganishwa kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) na Shirika la Viwango nchini(TBS)

Hapana, ni bora ofisi ya Waziri Mkuu iwe inafanya hiyo kazi kwasababu hizi taasisi na Wizara zinapigania ulaji kwenye the same commodities hawawezi kukubaliana lakini ofisi ya PMO inaweza kufanya maamuzi magumu.
Ndiyo maana kuna mahala ameagiza Mawaziri husika watunge sheria kuunganisha Taasisi zote mbili.
 
Siku ingine atasema TANTRADE,EPZA na TIC viunganishwe,

Mi nadhan hata kama kwa namna fulan kazi zinafanana lakini kuunganisha taasisi ni kupunguza baadhi ya ajira. Maana kama kila taasisi ina DG lazima mmoja apigwe chini, vivyo hivyo kwenye kwenye yeo vingine pia.
 
Kwanini uajiri watu watatu kwa kazi ya MTU mmoja halafu gharama unaniletea mimi mwananchi? Unafahamu mishahara yao inatoka kwenye kodi zetu.
 
Ushauri wa mh Majaliwa ni madhubuti.

Major reforms are urgently needed. kama alivyosema muheshimiwa, bunge lijalo la mwezi wa sita inabidi lipelekewe muswada wa kufanya mabadiliko kwenye taasisi hizi ili kuondoa umangimeza, rushwa na kutokuwajibika huku urasimu na ucheleweshwaji wa matokeo ya vipimo ukikithiri.

Mh Majaliwa, huko tuendapo inabidi TBS na TFDA zibaki na supervisory and appellate role. Kuwe na makampuni yatayopitishwa (prequalified) kufanya kazi za kiutendaji za TBS na TFDA hawa kazi yao ibaki kutoa vibali tu.
TBS na TFDA ziwe kama REA na Tanroads.
Yan mfano REA wao kazi yao sio kujenga miundimbinu ya umeme bali kutoa hela na kusimamia wakandarasi kujenga miundombinu ya umeme.

Tanroads sio kujenga bara bara bali ni kutoa hela na kusimamia wakandarasi wa bara bara.
TFDA nayo ijitoe kwenye kufanya vipimo na ukaguzina bali ijikite kwenye kazi ya kusimamia kampuni binafsi ambazo zitafanya kazi za ukaguzi na upimaji wa chakula na madawa ambazo kwa sasa zinafanywa na TFDA. Then kampuni hizo zitakuwa zinalipwa kamishen.
TBS vivyo hivyo. Itakuwa inasimamia mawakala wa kudhibiti ubora. Mfano sasa TBS ina mawakala wa kusimamia ubora wa magari yanayoingia nchini kama JAAI, NIT nk. Hii inabidi iende kwenye field zote. Hili litaondoa urasimu, kukuza wigo wa ajira na kuongeza uwajibikaji.

Kina TFDA na TBS wao watakuwa wanapekekewa daily reports ambapo wataweza kufanya cross cheking pale riport isipowaridhisha.
Wakiridhishwa na ripoti iliyopelekwa, then wao wanagonga muhuri na kibali kinatolewa sasa na hao TFDA na TBS on the next day.
By the way, kwenye system kwa TFDA au TBS ku approve report iliyowekwa na wakala huchukua muda mfupi tu...
Mifano iko mingi. Hata pale bandarini, TPA ime sub contract kampuni za kupakua mizigo na yenyewe inabaki kuzisimamia. Hivi ndivyo TFDA na TBS mpya inavyotakiwa kuwa.

Appellate Functions ya TFDA/ TBS
Iwapo importer A ameleta mzigo wake nchini. Atapeleka sampuli za mzigo wake kwa wakala wa kwanza kwa ajili ya vipimo. Ikiwa vipimo vitaonesha mzigo wake uko chini ya kiwango then atatakiwa kupeleka sampuli kwa mawakala wengine wawili akitumia reference no itayokuwa generated kwenye system ya TFDA/TBS iwapo hakuridhika na uamuzi wa mpimaji wa kwanza. Iwapo mpimaji mmoja wapo atatoa vipimo vitavyoonesha mzigo haufai ikiwa mpimaji wa tatu ataona kuwa mzigo unafaa then mzigo huo utakuwa deemed kuwa haufai kwa matumizi ya binadamu. But iwapo mawakala wawili waliopima kwa mara ya pili wote wakiukubali mzigo huo basi utapita.
Lakini iwapo imetokea mawakala wawii kati ya watatu wameukataa mzigo na mmoja kuukubali, then muagizaji atakata rufaa tena na kupeleka vipimo kupimwa na TFDA/TBS wenyewe.
Uamuzi wa TFDA/TBS utakuwa final and conclusive na hautategemea majibu ya vipimo vya mawakala waliotangulia. Uamuzi wa TFDA/TBS utakuwa ni free standing decision...
 
Mh Majaliwa acha siasa katika vyombo hivi vina majukumu mhimu ya kutulinda wanananchi. Waondoleeni kero zinazowalazimisha kutafuta fedha kama wafanya biashara. Wote tunajua madhara ya bidhaa dhaifu. Je unataka twende huko kweli ambako hatimaye gharama zake ni kubwa mno!
Io siasa laiti ungejua Ni usumbufu mkubwa kiasi gani tunapata tunao subiri uthibitisho wa bidhaa zetu na vibali vya ithibayi ungempongeza pm wetu
 
Waziri mkuu " Anauwezo mkubwa sana wakufikiri kuliko yule mzee anayejiita malaika mkuu--- ukisoma hili bandiko utakubaliana na hiki ninacho kisema..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri wa mh Majaliwa ni madhubuti.

Major reforms are urgently needed. kama alivyosema muheshimiwa, bunge lijalo la mwezi wa sita inabidi lipelekewe muswada wa kufanya mabadiliko kwenye taasisi hizi ili kuondoa umangimeza, rushwa na kutokuwajibika huku urasimu na ucheleweshwaji wa matokeo ya vipimo ukikithiri.

Mh Majaliwa, huko tuendapo inabidi TBS na TFDA zibaki na supervisory role. Kuwe na makampuni yatayopitishwa (prequalified) kufanya kazi za kiutendaji za TBS na TFDA hawa kazi yao ibaki kutoa vibali tu.
TBS na TFDA ziwe kama REA na Tanroads.
Yan mfano REA wao kazi yao sio kujenga miundimbinu ya umeme bali kutoa hela na kusimamia wakandarasi kujenga miundombinu ya umeme.

Tanroads sio kujenga bara bara bali ni kutoa hela na kusimamia wakandarasi wa bara bara.
TFDA nayo ijitoeiwe kwenye kufanya vipimo na ukaguzina bali ijikite kwenye kazi ya kusimamia kampuni binafsi ambazo zitafanya kazi za ukaguzi na upimaji wa chakula na madawa ambazo kwa sasa zinafanywa na TFDA. Then kampuni hizo zitakuwa zinalipwa kamishen.
TBS vivyo hivyo. Itakuwa inasimamia mawakala wa kudhibiti ubora. Mfano sasa TBS ina mawakala wa kusimamia ubora wa magari yanayoingia nchini kama JAAI, NIT nk. Hii inabidi iende kwenye field zote. Hili litaondoa urasimu, kukuza wigo wa ajira na kuongeza uwajibikaji.

Kina TFDA na TBS wao watakuwa wanapekekewa daily reports ambapo wataweza kufanya cross cheking pale riport isipowaridhisha.
Wakiridhishwa na ripoti iliyopelekwa, then wao wanagonga muhuri na kibali kinatolewa sasa na hao TFDA na TBS on the next day.
Mifano iko mingi. Hata bale bandarini, TPA ime sub contract kampuni za kupakua mizigo na yenyewe inabaki kuzisimamia. Hivi ndivyo TFDA na TBS mpya inavyotakiwa kuwa.
Umenena mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,
kwani hatuwezi tukawa na taasisi moja itakayokuwa na vitengo tofauti vya kupima ubora na viwango badala ya kila taasisi kufanya mambo yake kivyake?
Mh Majaliwa acha siasa katika vyombo hivi vina majukumu mhimu ya kutulinda wanananchi. Waondoleeni kero zinazowalazimisha kutafuta fedha kama wafanya biashara. Wote tunajua madhara ya bidhaa dhaifu. Je unataka twende huko kweli ambako hatimaye gharama zake ni kubwa mno!
 
Hapo kwenye usimamizi wa dawa kwa kampuni binafsi utaleta matatizo makubwa. Do not mess up with control and regulation of medicines it will result into disasters.
 
Ushauri wa mh Majaliwa ni madhubuti.

Major reforms are urgently needed. kama alivyosema muheshimiwa, bunge lijalo la mwezi wa sita inabidi lipelekewe muswada wa kufanya mabadiliko kwenye taasisi hizi ili kuondoa umangimeza, rushwa na kutokuwajibika huku urasimu na ucheleweshwaji wa matokeo ya vipimo ukikithiri.

Mh Majaliwa, huko tuendapo inabidi TBS na TFDA zibaki na supervisory role. Kuwe na makampuni yatayopitishwa (prequalified) kufanya kazi za kiutendaji za TBS na TFDA hawa kazi yao ibaki kutoa vibali tu.
TBS na TFDA ziwe kama REA na Tanroads.
Yan mfano REA wao kazi yao sio kujenga miundimbinu ya umeme bali kutoa hela na kusimamia wakandarasi kujenga miundombinu ya umeme.

Tanroads sio kujenga bara bara bali ni kutoa hela na kusimamia wakandarasi wa bara bara.
TFDA nayo ijitoeiwe kwenye kufanya vipimo na ukaguzina bali ijikite kwenye kazi ya kusimamia kampuni binafsi ambazo zitafanya kazi za ukaguzi na upimaji wa chakula na madawa ambazo kwa sasa zinafanywa na TFDA. Then kampuni hizo zitakuwa zinalipwa kamishen.
TBS vivyo hivyo. Itakuwa inasimamia mawakala wa kudhibiti ubora. Mfano sasa TBS ina mawakala wa kusimamia ubora wa magari yanayoingia nchini kama JAAI, NIT nk. Hii inabidi iende kwenye field zote. Hili litaondoa urasimu, kukuza wigo wa ajira na kuongeza uwajibikaji.

Kina TFDA na TBS wao watakuwa wanapekekewa daily reports ambapo wataweza kufanya cross cheking pale riport isipowaridhisha.
Wakiridhishwa na ripoti iliyopelekwa, then wao wanagonga muhuri na kibali kinatolewa sasa na hao TFDA na TBS on the next day.
Mifano iko mingi. Hata bale bandarini, TPA ime sub contract kampuni za kupakua mizigo na yenyewe inabaki kuzisimamia. Hivi ndivyo TFDA na TBS mpya inavyotakiwa kuwa.
toa mfano wa nchi wanayofanya hayo unayopendekeza
 
Hapo kwenye usimamizi wa dawa kwa kampuni binafsi utaleta matatizo makubwa. Do not mess up with control and regulation of medicines it will result into disasters.
na mimi nimemuliza swali..subiri tuone majibu yake
 
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirikia la Viwango Tanzania (TBS) kuacha urasimu huku akimtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda kuandaa muswada wa kuunganisha taasisi hizo na kuwasilisha bungeni ili sheria zake zifanyiwe mapitio upya.

Majaliwa aliyasema hayo juzi katika kikao chake na wafanyabiashara wa kati na wadogo uliofanyika kwenye ukumbi wa Anatoglo ambapo alionyesha kukasirishwa na urasimu wa taasisi hizo mbili na kuagiza pia wakurugenzi wa taasisi hizo kufanya mapitio ya utendaji wa watumishi wao. Alisema mamlaka hizo zikiunganishwa zitaweza kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilalamikia kuwepo kwa tozo nyingi na urasimu unaosababisha taifa kupoteza makundi makubwa ya wafanyabiashara na wateja.

“Sheria za TBS na TFDA zote zinafanana, ni maneno tu mnacheza nayo huku ubora, sijui viwango, vikiwa na viwango lazima vitakuwa bora, urasimu tu ndio uliokithiri TBS na TFDA, mizigo inakuja bandarini inakaa miezi miwili mitatu mnajifanya mnapima, mnapima nini?”alihoji Majaliwa. Aliongeza kuwa ukimwi wenyewe siku hizi unapimwa kwa dakika tano unapewa majibu yako na kuongeza kuwa typhoid unapima leo, kesho mtu anatakiwa kupewa majibu lakini akahoji kwa nini wao wanachukua siku 20.

“Kama mashine zenu mbovu kwa nini msiagize mashine nyingine nje, Mkemia mkuu yupo kwa nini msiende kupima huko, mnakaa na bidhaa za watu muda mrefu mpaka zinaoza ndio maana wakati mwingine TRA wanaruhusu mizigo itoke mnakuja baadae kusema bidhaa haina viwango… mawaziri wa wizara zote kaeni na taasisi zenu mbadilike, kama mashine yenu inachukua miaka mitano kutoa majibu basi nunueni zenye ubora, nimesikia TBS wanapima mpaka stuli za kukalia, hivi stuli unapima nini? “alihoji.

Waziri Majaliwa alizitaka taasisi hizo zitoe mwongozo kama kwenye soko bidhaa za thamani za ndani zinazotakiwa sio kusumbua wafanyabiashara. “TBS mnapima mpaka shati, nadhani kuna haja ya kufanya mapitio taasisi hii, kuna mtu mmoja alikuja ofisini kwangu kanunua vifaa vyake China vya ujenzi vya nyumbani madirisha, milango na masinki ya vyoo, kalipia kila kitu vimefika bandarini TBS imezuia miezi minne eti mwisho mnasema vipo chini ya kiwango, kila kitu kikitoka Italia wananchi wa Magomeni Mapipa watawaweza kumudu gharama?” aliuliza.

Majaliwa pia aliwataka wafanyabiashara wasikubali kutoa rushwa kwa chombo chochote na kuwataka watendaji kuacha lugha za dharau kwa wananchi na kuzitaka taasisi zote zinazohusika na masuala ya Bandari, TRA, TBS na TFDA kukaa jengo moja kuwaepusha wananchi na usumbufu wa nenda rudi.

“Bandarini kuna jengo moja kubwa sana pale limekaa kama meli, kuna vyumba vipo tupu, taasisi zote zinazousika zikae pale mtu akienda kulipia mizigo yake anamaliza kila kitu pale sio kupiga makitaimu mara bandarini, Ubungo achene urasimu, na nyie wananchi, rushwa si sehemu ya mkakati wa serikali, hivyo vita dhidi ya rushwa lazima iendelezwe na watu wote. Mafanikio tuliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa huduma za afya, maji na barabara ni matokeo ya kupiga vita rushwa,” alisema.

Majaliwa aliwataka pia watumishi kuacha kukaa ofisini na badala yake wajenge tabia ya tabia ya kuwatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao na kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao ili kutafuta ufumbuzi.

“Kila mtendaji katika eneo lake atekeleze majukumu yake kikamilifu urasimu, dharau, lugha za ajabu zimeshamiri kwenye maeneo ya kutolea huduma jambo ambalo si sahihi. Badilikeni,” alisema. Alisema serikali imepanga mpango wa kulibadilisha utaratibu wa kufanya biashara katika eneo la Kariakoo ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa saa 24 kama yalivyo masoko makubwa duniani.

Waziri Mkuu alisema lengo la mabadiliko hayo ni kukuza uchumi wa taifa na wa wafanyabiashara kwa ujumla. “Nchi yetu ina usalama na ulinzi wa kutosha hivyo hatuwezi kushindwa kufanya biasahara wakati wote.”

Katika mkutano huo aliouitisha kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu alisema atakutana na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam ili kupanga namna ya kutekeleza utaratibu huo. Alisema jiji la Dar es Salaam moyo wa kitivo cha kibiashara nchini, hivyo serikali itahakikisha mwenendo wa biashara unaboreshwa pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya biashara zao wakati wote na bila usumbufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata shirika la vipimo nalo liwe kitengo cha TBS au vipi?
 
YaE="beth, post: 30610217, member: 98660"]WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirikia la Viwango Tanzania (TBS) kuacha urasimu huku akimtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda kuandaa muswada wa kuunganisha taasisi hizo na kuwasilisha bungeni ili sheria zake zifanyiwe mapitio upya.

Majaliwa aliyasema hayo juzi katika kikao chake na wafanyabiashara wa kati na wadogo uliofanyika kwenye ukumbi wa Anatoglo ambapo alionyesha kukasirishwa na urasimu wa taasisi hizo mbili na kuagiza pia wakurugenzi wa taasisi hizo kufanya mapitio ya utendaji wa watumishi wao. Alisema mamlaka hizo zikiunganishwa zitaweza kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilalamikia kuwepo kwa tozo nyingi na urasimu unaosababisha taifa kupoteza makundi makubwa ya wafanyabiashara na wateja.

“Sheria za TBS na TFDA zote zinafanana, ni maneno tu mnacheza nayo huku ubora, sijui viwango, vikiwa na viwango lazima vitakuwa bora, urasimu tu ndio uliokithiri TBS na TFDA, mizigo inakuja bandarini inakaa miezi miwili mitatu mnajifanya mnapima, mnapima nini?”alihoji Majaliwa. Aliongeza kuwa ukimwi wenyewe siku hizi unapimwa kwa dakika tano unapewa majibu yako na kuongeza kuwa typhoid unapima leo, kesho mtu anatakiwa kupewa majibu lakini akahoji kwa nini wao wanachukua siku 20.

“Kama mashine zenu mbovu kwa nini msiagize mashine nyingine nje, Mkemia mkuu yupo kwa nini msiende kupima huko, mnakaa na bidhaa za watu muda mrefu mpaka zinaoza ndio maana wakati mwingine TRA wanaruhusu mizigo itoke mnakuja baadae kusema bidhaa haina viwango… mawaziri wa wizara zote kaeni na taasisi zenu mbadilike, kama mashine yenu inachukua miaka mitano kutoa majibu basi nunueni zenye ubora, nimesikia TBS wanapima mpaka stuli za kukalia, hivi stuli unapima nini? “alihoji.

Waziri Majaliwa alizitaka taasisi hizo zitoe mwongozo kama kwenye soko bidhaa za thamani za ndani zinazotakiwa sio kusumbua wafanyabiashara. “TBS mnapima mpaka shati, nadhani kuna haja ya kufanya mapitio taasisi hii, kuna mtu mmoja alikuja ofisini kwangu kanunua vifaa vyake China vya ujenzi vya nyumbani madirisha, milango na masinki ya vyoo, kalipia kila kitu vimefika bandarini TBS imezuia miezi minne eti mwisho mnasema vipo chini ya kiwango, kila kitu kikitoka Italia wananchi wa Magomeni Mapipa watawaweza kumudu gharama?” aliuliza.

Majaliwa pia aliwataka wafanyabiashara wasikubali kutoa rushwa kwa chombo chochote na kuwataka watendaji kuacha lugha za dharau kwa wananchi na kuzitaka taasisi zote zinazohusika na masuala ya Bandari, TRA, TBS na TFDA kukaa jengo moja kuwaepusha wananchi na usumbufu wa nenda rudi.

“Bandarini kuna jengo moja kubwa sana pale limekaa kama meli, kuna vyumba vipo tupu, taasisi zote zinazousika zikae pale mtu akienda kulipia mizigo yake anamaliza kila kitu pale sio kupiga makitaimu mara bandarini, Ubungo achene urasimu, na nyie wananchi, rushwa si sehemu ya mkakati wa serikali, hivyo vita dhidi ya rushwa lazima iendelezwe na watu wote. Mafanikio tuliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa huduma za afya, maji na barabara ni matokeo ya kupiga vita rushwa,” alisema.

Majaliwa aliwataka pia watumishi kuacha kukaa ofisini na badala yake wajenge tabia ya tabia ya kuwatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao na kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao ili kutafuta ufumbuzi.

“Kila mtendaji katika eneo lake atekeleze majukumu yake kikamilifu urasimu, dharau, lugha za ajabu zimeshamiri kwenye maeneo ya kutolea huduma jambo ambalo si sahihi. Badilikeni,” alisema. Alisema serikali imepanga mpango wa kulibadilisha utaratibu wa kufanya biashara katika eneo la Kariakoo ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa saa 24 kama yalivyo masoko makubwa duniani.

Waziri Mkuu alisema lengo la mabadiliko hayo ni kukuza uchumi wa taifa na wa wafanyabiashara kwa ujumla. “Nchi yetu ina usalama na ulinzi wa kutosha hivyo hatuwezi kushindwa kufanya biasahara wakati wote.”

Katika mkutano huo aliouitisha kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu alisema atakutana na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam ili kupanga namna ya kutekeleza utaratibu huo. Alisema jiji la Dar es Salaam moyo wa kitivo cha kibiashara nchini, hivyo serikali itahakikisha mwenendo wa biashara unaboreshwa pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya biashara zao wakati wote na bila usumbufu.

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]
Tangu awe waziri mkuu,hapa nimwelewa na kumpa pongezi.kanena kiukweli
 
Back
Top Bottom