Waziri Mkuu 'ashusha rungu' kwa wanaowapa mimba wanafunzi, awataka TAMISEMI kukamilisha maabara 4587

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
PM.jpg

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote atakayebainika amemkatisha mwanafunzi wa kike masomo kwa kumpa mimba au kumfanyia vitendo vya ukatili vitakavyopelekea kukatisha masomo yake ni lazima afungwe miaka 30 jela.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Lugalo jeshini Jijini Dar es Salaam wakati akizindua na kukabidhi vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 16.9 kwa ajili ya shule 1696 kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha uboreshaji wa masomo ya sayansi.

Vilevile Majaliwa ameiagiza TAMISEMI kuhakikisha wanakamilisha maabara za shule zote nchini 4587 ambazo bado hazijakamilika ili vifaa hivyo vianze kusaidia wanafunzi kwa haraka na kufikia malengo ya nchi ya kuwa ya uchumi wa kati.

Pamoja na hayo, Majaliwa amesema watendaji watakaoenda kinyume na maadili ya kazi zao ni lazima mkono wa sheria uchukue nafasi yake.

Chanzo: Mpekuzi
 
Hakuna rungu aliloshusha maana haijawahi kuruhusiwa kumpa mwanafunzi mimba ...... ....


Swala la msingi "Wanafunzi nao waache vihere here"
 
The same person alitoa tamko la bandari kuanza kutoa huduma za masaa 24 kwa muda wa siku mbili.

Baada ya kulazimisha makampuni ya simu yatoe public offers za vodacom mpaka deadline date share kibao zilibaki matokeo yake wakaongeza muda, akaja akazipigia debe na hakuna anaejua kama ziliuzwa zote.

I'll be wary na maamuzi technical ya hii serikari mara nyingi huwa awafikirii kwanza namna sahihi kinachokuja kichwani wao wanapokea tu.

Huku kwenye maswala ya wizara ya afya, jinsia, wazee na watoto; ndio kila wanapogusa wanaboronga wanamtazamo wao wa kufanya mambo unajiuliza hivi hawa watu kwanini waone mambo tofauti na dunia kwenye approaches zao. Wakati kila mtu anaongozwa na directives za WHO kinachohitajika ni watu tu wenye uelewa wa health management to implement those directives.

Sio wenzetu contributing factors wao huwa wanazi ignore, namna sahihi ya kutatua matatizo awafauati; wakija wanakuja na simple solutions ambazo hazina ubunifu wowote na wala azilengi kubadilisha asilimia kubwa ya tatizo in the long run.
 
Mi naona hii inakuwa sio haki kwan mwanafunz yy hana haki ya kupata hicho kitu,kama ni hivyo bas ingekuwepo sheria ya kwa nn mwanafunz kakubali kupewa mimba? Atakae kubali miaka 15 jela,ote wangeenda tu jela 30 kwa 15 na tano baada ya kujifungua kw nn ss rufungwe ili hali yy n mwanafunz na ukute kajipendekeza,mara aje getto na kanga moko mara hai wakat ni dent iwepo sheria ile huk na huku ndo watakomesha
 
sheria ya wanaowapa wanafunzi mimba haikuzingatia makosa kwa pande zote mbili.lawama zimeelekezwa zaidi kwa wanaume kuwa ndio wakosaji wakubwa na kutungiwa adhabu kali.

lakini utakuta binti amepewa ujauzito halafu aidha anaamua kwa makusudi kutomtaja mhusika, au kesi ikifikishwa mahakamani binti hatoi ushirikiano kwa waendesha mashtaka, na wakati mwingine anatoroka asifike kutoa ushahidi matokeo yake kesi inafutwa.

ingekuwa vizuri ikatungwa sheria sambamba ya nyongeza kuwa mwanafunzi atakayepewa mimba halafu kwa makusudi hatoi ushirikiano wa kumtia hatiani mhusika basi nae apatiwe kifungo kwa kosa la kuficha uhalifu ili kukomesha tabia hiyo.
 
Mimba ni outcome ya tendo la ndoa, sasa either kuwe na age definition ya kusema mtoto ni umri gani na adult ni kuanzia age gani.

Na ieleweke kabisa an adult aruhusiwi kufanya tendo la ndoa na mtoto mdogo adhabu yake wakisema ata miaka 100 jela no problem; kama lengo ni watu wazima kuacha kuchukua advantage ya watoto awe anasoma au la.

Lakini wao awajitambui ni kama wanaruhusu watoto kufanya ngono lakini wasipewe mimba kuendekeza tu ufuska wao; isitoshe wanafunzi wengi Tanzania walio A level ni over 18 and adults utawapangia hawa.

Ni watu ambao wana majibu rahisi kwenye matatizo yenye changamoto ngumu zinazo hitaji mikakati ya wizara na kushirikiana na taassi kadhaa kupambana na mimba za wanafunzi.

Baba jela miaka 30 nani atamtunza huyo mtoto.
 
Wanafunzi wanapata mimba sababu ya vihere here vyao, by jakaya kikwete in mwanza.kwenye may mosi
 
tatizo LA mimba ni kubwa sana,

shule x mkoani geita, darasa LA kidato cha tatu wanafunzi watano wamepata ujauzito. wazazi hawajapeleka kesi popote hata akija kuwahojo majaliwa mwenyewe hatapata usbirikiano.


hizi skendo za ngono ni nyingi sana!!!!

walimu wangu wote primary wameoa wanafunzi wao,

o-level wote walioa wanafunzi wao waliomaliza kati ya 2006-2008!

a level tulikiwa boys!!

lkn chuoni Udsm waliwaoa tu.


njooni kwa mbu-nge hapo Dodoma huwanyatia sana cbe na udom

nikiwa mabibo hostel vigogo walikiwa wanakuja 'kuvusha'


yaani, haya maswala yanayofanyika kwa siri ni yakuamuliwa kiimani zaidi.

kama sobibo walitongozana, sembuse kwa mkwala wa KM alioutoa baada ya kifurahishwa na msaada!?

he, "mtoni" hawapati mimba wakiwa shule?

je, wametia elimu ya jinsia na afya ya uzazi?

je, walimu hawapati "teaching allowances"?

je, umasikini umepungua? yaani binti akitiwa mimba na mzee akapewa 2m unadhani atatoa ushirikiano, afungwe halafu alee mtoto na mjukuu?

je, watoto wa kishua na kikayumba ni wapi hupata mimba zaidi?

je, watoto wa mjini na kijijini wapi wanapata mimba zaidi?

je, wajua kuwa watoto wanatumia vidonge vya kuzuia mimba, maana yake bya kuchochea zinaa?



hitimisho
mimba hazitaisha ndani ya miaka mitatu ijayo, tuwaelimisheni watoto wetu.

binafsi mdogo wangu au mwanangu akipewa ujauzito sitamfunga mtu, badala yake mhusika atoe ghalama nilizotumia na nitakazotumia baada ya kujifungua kisha anarudi shule.

nikimfunga litakiwa fundisho kwa wengine lkn sitanufaika na chichote.

tutokomeze mimba utotoni
 
Sheria kali imekuwepo kwa takriban miaka 20 sasa; usimamizi haupo. Matamko haya yamekuwa yakitolewa miaka yote bila impact. Tatizo: usimamizi hafifu.
 
Back
Top Bottom