Waziri Mkuu ashuhudia usafirishaji wa Korosho bandari ya Mtwara

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1569995446841.png

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea bandari ya Mtwara na ameshuhudia shehena ya korosho ziliyonunuliwa na kampuni ya Tang Long zikipakiwa katika meli kubwa yenye jina la AS Christiana kwa ajili kusafirishwa kwenda nchini Vietnam.

“Ni faraja kuona mzigo wa korosho ukiondoka na kutoa nafasi ya kuingiza mzigo mwingine mpya wa korosho utakaopatikana baada ya kuanza msimu mpya mwezi huu. Na mnunuzi huyu ameahidi kununua tani 100,000 katika msimu wa mwaka huu.”

Waziri Mkuu ametembelea Bandari ya Mtwara leo (Jumanne, Oktoba 1, 2019) kwa ajili ya kujionea kazi ya usafirishaji wa korosho inavyofanyika na amesema kwamba ameridhishwa na kasi na utaratibu unaoendelea badarini hapo.

Amesema kampuni ya Tang Long ya nchini Vietnam licha ya kuahidi kununua korosho katika msimu wa mwaka huu, pia imeomba kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho nchini na kwamba wapo tayari kuanza hata Desemba, 2019.

Waziri Mkuu amesema suala la ujenzi wa viwanda vya kubangulia korosho nchini litaongeza thamani na kuwezesha dunia nzima kutambua kuwa korosho hizo zimetoka Tanzania kwa sababu kwenye vifungashio watakuwa wameandika, hivyo kuongeza soko.

Akizungumzia kuhusu msimu wa uuzaji wa korosho wa mwaka huu, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha kwanza watapewa wenye viwanda vya ndani na kisha tani zinazobaki zitauzwa kwa wanunuzi kutoka nje.

“Wito wa Rais Dkt. John Magufuli wa ujenzi wa viwanda unalenga katika kuongeza ajira kwa wananchi kwa kuwa viwanda vinaajiri watu wengi wenye kada tofauti. Wakuu wa mikoa endeleeni kurahisisha mazingira ya uwekezaji.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Geoffrey Mwambe amesema licha ya kampuni ya Tang Long kununua korosho nchini pia imeomba ikodishwe kiwanda kimojawapo cha Serikali ili waweze kuanza ubanguaji wa korosho ikiwa ni mpango wa muda mfupi na katika mpango wao wa muda mrefu wameomba eneo kati ya mkoa wa Lindi au Mtwara ili wajenge kiwanda cha kubangua korosho. Taratibu zinaendelea
 
Uchaguzi umekaribia lazima kila kitu kipate solution,hata watakatisha hela kuomba msamaha bila kuhukumiwa ili wawe injini ya kutoa support wakati wa uchaguzi
 
Asanteni kwa taarifa hii njema ya matumaini. Hongera PM kwa kufuatilia jambo hili muhimu.
 
Korosho zimenunuliwa Hapo utashangaa kuna kitu cha Watu kinanuna!
ziliporwa mwaka jana poyoyo wewe. hujui kuwa haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyopokwa kwa kiburi na ufedhuli wa huyo kichaa anayesamehe aliwaita wezi bila kuthibitishwa popote
miaka minne ya makelele yake ya anayoita vita dhidi ya ufisadi kamfunga nani
 
View attachment 1221319
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea bandari ya Mtwara na ameshuhudia shehena ya korosho ziliyonunuliwa na kampuni ya Tang Long zikipakiwa katika meli kubwa yenye jina la AS Christiana kwa ajili kusafirishwa kwenda nchini Vietnam.

“Ni faraja kuona mzigo wa korosho ukiondoka na kutoa nafasi ya kuingiza mzigo mwingine mpya wa korosho utakaopatikana baada ya kuanza msimu mpya mwezi huu. Na mnunuzi huyu ameahidi kununua tani 100,000 katika msimu wa mwaka huu.”

Waziri Mkuu ametembelea Bandari ya Mtwara leo (Jumanne, Oktoba 1, 2019) kwa ajili ya kujionea kazi ya usafirishaji wa korosho inavyofanyika na amesema kwamba ameridhishwa na kasi na utaratibu unaoendelea badarini hapo.

Amesema kampuni ya Tang Long ya nchini Vietnam licha ya kuahidi kununua korosho katika msimu wa mwaka huu, pia imeomba kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho nchini na kwamba wapo tayari kuanza hata Desemba, 2019.

Waziri Mkuu amesema suala la ujenzi wa viwanda vya kubangulia korosho nchini litaongeza thamani na kuwezesha dunia nzima kutambua kuwa korosho hizo zimetoka Tanzania kwa sababu kwenye vifungashio watakuwa wameandika, hivyo kuongeza soko.

Akizungumzia kuhusu msimu wa uuzaji wa korosho wa mwaka huu, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha kwanza watapewa wenye viwanda vya ndani na kisha tani zinazobaki zitauzwa kwa wanunuzi kutoka nje.

“Wito wa Rais Dkt. John Magufuli wa ujenzi wa viwanda unalenga katika kuongeza ajira kwa wananchi kwa kuwa viwanda vinaajiri watu wengi wenye kada tofauti. Wakuu wa mikoa endeleeni kurahisisha mazingira ya uwekezaji.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Geoffrey Mwambe amesema licha ya kampuni ya Tang Long kununua korosho nchini pia imeomba ikodishwe kiwanda kimojawapo cha Serikali ili waweze kuanza ubanguaji wa korosho ikiwa ni mpango wa muda mfupi na katika mpango wao wa muda mrefu wameomba eneo kati ya mkoa wa Lindi au Mtwara ili wajenge kiwanda cha kubangua korosho. Taratibu zinaendelea
Hivi waziri mkuu halindwi sana?
 
Korosho zimenunuliwa Hapo utashangaa kuna kitu cha Watu kinanuna!

Walionuna wananiuliza zimeuzwa kwa bei elekezi ya elf 3 na ushee kwa kilo au tumewapa discount kubwa kuliko ile ambayo Wafanyabiashara walikuwa tayari kununua wakati ule?

Nmekosa jibu la kumpa

Kama tumepata wa kununua kwa bei nzuri sioni sababu ya mwaka huu kuruhusu wale Wafanyabiashara wazushi kulalia Wakulima

Tupeleke tena Majeshi yasombe kama mwaka jana kwa kuwa si tuna Mteja tayari
 
Back
Top Bottom