Waziri Mkuu ashangaa Tanzania kuwa na wachambuzi wengi wa mpira huku haina kocha hata mmoja anayefundisha nje

So mchambuzi anawezaje kumkosoa kocha kila wakati wakati yeye hajui lolote kuhusu ukocha? Au ni blah blah tu?
Chief kuna wengine wanakosoa kwa hoja kweli na wengine ni blah blah tu, sio kila mchambuzi anafaa kuwa kocha na ni rahisi kwa kocha kuwa mchambuzi ila sio rahisi sana kwa mchambuzi kuwa kocha
 
Kwahio sababu huwezi kutaga inamaanisha kwamba huwezi kutambua yai Viza ?
Huo mfano wako hauendani sababu kutambua unahitaji tu kuona ila kutaga ni kuunda.
Kocha anahitaji tu kusema, yaani kuwaeleza wachezaji cha kufanya, mchambuzi naye ni kusema tu, sema yeye anakuwa redioni akisema na wasikilizaji.
 
Chief kuna wengine wanakosoa kwa hoja kweli na wengine ni blah blah tu, sio kila mchambuzi anafaa kuwa kocha na ni rahisi kwa kocha kuwa mchambuzi ila sio rahisi sana kwa mchambuzi kuwa kocha
Kwa hiyo tunapigwa na hawa wachambuzi sio?
 
Unajua kukosoa jinsi chakula kilivyopikwa ila wewe hujui kupika? Wewe utakuwa ni tapeli
Kwa mfano hapa ikitokea Jamiiforums unapost halafu ujumbe wako hauonekani au inaandika kilugha ambacho hakieleweki ukikosoa mfumo ukasema haufanyi kazi vizuri huku haujui kutengeneza hiyo mifumo ya computer, utakuwa ni tapeli ?
 
Hebu niambie kinachomfanya mchambuzi anyejua kila mchezaji wa timu A ana weakness hii na strength hii kiufundi na kisaikolojia, na anajua namna bora ya kuwapanga ili wa perfom vizuri, na pia anajua pia timu pinzani wachezaji wake, udhaifu wao na umahiri wao, na pia anajua kocha wao mbinu zake

Huyu mchambuzi nini kinamzuia asiwe kocha?

Mfano uliotoa ni hauendani sababu kutengeneza mfumo unatakiwa ujue mambo ya code n.k ila kwenye ukocha na uchambuzi wote wanachotakiwa kuwa nacho kufahamu technic za mpira tu
 
imagine huyu naye ni mchambuzi na anaapa kwa jina la mama yake kwamba hii list imetolewa na CAf mwezi april...
Screen Shot 2022-04-05 at 7.24.11 PM.png
 
Hebu niambie kinachomfanya mchambuzi anyejua kila mchezaji wa timu A ana weakness hii na strength hii kiufundi na kisaikolojia, na anajua namna bora ya kuwapanga ili wa perfom vizuri, na pia anajua pia timu pinzani wachezaji wake, udhaifu wao na umahiri wao, na pia anajua kocha wao mbinu zake

Huyu mchambuzi nini kinamzuia asiwe kocha?

Mfano uliotoa ni hauendani sababu kutengeneza mfumo unatakiwa ujue mambo ya code n.k ila kwenye ukocha na uchambuzi wote wanachotakiwa kuwa nacho kufahamu technic za mpira tu
wachambuzi wanachambua zaidi matokeo, makocha wanafundisha mbinu za soka
 
Sasa wachambuzi kama privadinho ndio wakpasomee ukocha na ukilaza wake ule alio nao.
 
Hebu niambie kinachomfanya mchambuzi anyejua kila mchezaji wa timu A ana weakness hii na strength hii kiufundi na kisaikolojia, na anajua namna bora ya kuwapanga ili wa perfom vizuri, na pia anajua pia timu pinzani wachezaji wake, udhaifu wao na umahiri wao, na pia anajua kocha wao mbinu zake

Huyu mchambuzi nini kinamzuia asiwe kocha?

Mfano uliotoa ni hauendani sababu kutengeneza mfumo unatakiwa ujue mambo ya code n.k ila kwenye ukocha na uchambuzi wote wanachotakiwa kuwa nacho kufahamu technic za mpira tu
Mchambuzi anaongea kwa nadharia kwamba ukimpanga hapa ata perfom vizuri, na wengi wanakuwa mahiri kuchambua baada ya mechi ni post mortem analysis. Hao wachezaji anaowaongelea sio mashine kwamba unaipanga tu hapa atacheza vizuri. Kocha wa mpira ana manage watu lazima ajue psychology ya watu wake ili aweze kuwa motivate vinginevyo hawezi kudumu kwenye kazi yake.

Gary Neville ni mchambuzi mashuhuri uingereza na kuna kipindi alikuwa anasifiwa mpaka akaanza kutafutwa na timu za mpira, akaenda Valencia mwenyewe anasema alikuwa anajiamini kwa sababu ya kucheza soka miaka 20 na pia kutokana na sifa nyingi alizopokea kuhusu uchambuzi wake. Alivyoanza mkataba ndio akajua kuna mambo mengi hayafahamu, ndani ya miezi minne akafukuzwa.

Kuna vitu vingi ambavyo kocha hufanya na kupangilia mpaka wanapoingia uwanjani wachambuzi wao wanaishia tu kuongelea kile kinachotokea ndani ya dakika 90 na habari chache kama tetesi au taarifa zinazoripotiwa na waandishi wa habari.

Mfano wangu unatofauti gani na mfano uliotoa kuhusu chakula ? Ukocha wa mpira ni fani inayohitaji mtu asome pia ili apewe leseni na aanze hatua kwa hatua mpaka kuweza kuwa mahiri, haina tofauti yoyote na hizo codes, lazima ujifunze na upite hatua kwa hatua mpaka uweze kuwa programmer mzuri. Kocha anahitaji zaidi ya technique za mpira kocha anahitaji kuelewa psychology, people management skills etc. mfano wa mwisho ni Thiery Henry, anafahamu technique nyingi za mpira na amecheza kwa ngazi ya juu kabisa duniani, alienda kwenye ukocha Monaco, alitupiwa virago alikuwa anafika hatua anagombana na wachezaji kwa kushangaa kwanini hawaelewi anachowaambia, ndani ya miezi mitatu aliondolewa. Kazi ya ualimu na uongozi wa timu ya watu zaidi ya 20 si tu kujua technique ni zaidi ya hayo.
 
Kwa hiyo mtu anaweza kukosoa jinsi mpishi anavyopika chakula ila yeye ukimpeleka jikoni hajui lolote? Huyo anajuaje sasa mpishi anavyokosea?
Kwamba sababu sijui kuweka chumvi kiasi fulani kwahio siwezi kujua kwamba chumvi imezidi ?

Wacheza mpira wengi they don't make good coaches why ? Kina Wenger, Ferguson je walikuwa wachezaji hodari ? Kwa logic yako kina Maradona na Pele ingebidi wawe ndio makocha wazuri kuliko wote...

Utagundua coaching inahitaji skills tofauti na uchambuzi, wakati uchambuzi unahitaji tu kujua the game / rules na kupenda unachokifanya as well as kufuatilia na kuangalia as many games as possible..., ukija kwenye coaching unahitaji the following:-
  • Good communication Skills,
  • Approachable
  • Leadership skills
  • Mahusiano mazuri na wachezaji wako
  • Organizational Skills na Attention to details
 
Hatuna hata kocha wa kufundisha Simba au Yanga achilia mbali nje!
Wa kufundisha Yanga wapo wengi sana, labda Simba Ni changamoto sana kumpatia mwenye viwango vya kimataifa. Simba Ni KUBWA kuliko kocha yyte mzawa.

Minziro, Mgunda, kihwelo pale yanga wanapiga mzigo fresh tu, mechi za yanga vs geita, prison, mbuni FC watashindwa nini.
 
Kwamba sababu sijui kuweka chumvi kiasi fulani kwahio siwezi kujua kwamba chumvi imezidi ?

Wacheza mpira wengi they don't make good coaches why ? Kina Wenger, Ferguson je walikuwa wachezaji hodari ? Kwa logic yako kina Maradona na Pele ingebidi wawe ndio makocha wazuri kuliko wote...

Utagundua coaching inahitaji skills tofauti na uchambuzi, wakati uchambuzi unahitaji tu kujua the game / rules na kupenda unachokifanya as well as kufuatilia na kuangalia as many games as possible..., ukija kwenye coaching unahitaji the following:-
  • Good communication Skills,
  • Approachable
  • Leadership skills
  • Mahusiano mazuri na wachezaji wako
  • Organizational Skills na Attention to details
Sio kila mchezaji must be a tactician kuna kuwa managerial officer , administration officer, kuna kuwa ambassador and influencer all can be in a field of soccer depending on someone's character and calibre and where he can fit most
.
Maana i ve seen best and good players become better coaches kama Johan Cruyff, Pep, Ancelotti, Mkwasa, Mexime , Ferguson , David O'leary, Viera, Arteta, Steve G , Klopp, Conte, Diego Simeone. Ila kuna Good players in administration post doing good kama Kidau, Ettoo, Kalusha Bwalya.
.
Again nimeona kuna good players becoming good ambassadors and influencers in sports kama Beckham, Romario, Abidal, Drogba etc.
.
Na vice versa the same.
.
Nadhani sometimes tuna hukumu former players katika ukocha pekee wakati Soka ni tasnia kubwa beyond ukocha
 
Uchambuzi na ufundishaji ni One and the Same ?

Gary Lineker huenda akashindwa kuifundisha hata timu ya chekecheka ila katika uchambuzi yupo vizuri..., Martin Oneal huenda akiongea usimuelewe ila kwenye Coaching sio wa kubeza

Coaching is a different ball game....
Coaching ni taaluma.
.
Practice Coaching is where there's a difference and hata inside Coaching practice kuna field zaidi ya kuwa Head Coach ambayo a coach can do .
 
Back
Top Bottom