Waziri Mkuu Majaliwa apiga marufuku mikutano ya kisiasa

PM ameanza kushindwa mapema hivi?! Anafaa kuambiwa kuwa utendaji wa Serikali hauna uhusiano wowote na shughuli za vyama vya siasa.

Biashara kuu ya vyama vya siasa ni kufanya siasa ili kuongoza dola. Hivyo, shughuli za kushika dola zianaanza pale uchaguzi unapokwisha pasipo lengo kuu kutimia. Kinyume na hivyo kinakuwa sio chama cha Siasa.
 
Hivi jaman hawa walioshindwa hawajui,wakati tulionao kwamba ni muda wa kazi na siyo siasa za maji taka.hapa kazi tu
 
Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku mikutano ya wapinzani ya kushukuru wananchi. Kasema mtu aliyeshindwa atashukuru nini kama siyo kuleta vurugu?

Kaonya wakuu wa mikoa na polisi watakaotoa vibali watashughulikiwa bila huruma
Huo ni udikteta
 
Khaa!! We vipi bana? Sera za chadema tumezisoma mtandaoni sasa kwa nini hizo shukrani wasiweke kule? Tusipotezeane mida bwana :mvutaji:

Mijitu mwingine sijui darasa la 6

Vyama vya siasa vimeunda kwa Mujibu wa Sheria avikuota kama uyoga nivyema tujue sheria nazo zinasemaje
 
Kitendo cha waziri mkuu kuzuia mikutano ya kisiasa wagombea mbalimbali kuwashukuru wapiga kura wao si kitendo cha haki,sio kitendo cha kidemokrasia ni udikteta,ningeunga mkono katazo hilo kama mgombea yeyote yule wa ngazi ya udiwani,ubunge au urais hakupata kura hata moja alafu anataka kwenda kuwashukuru wapiga kura wake.Waacheni wanasiasa wafanye shughuli zao za kisiasa kwa kuzingatia sheria na iacheni serikali ifanye shughuli zake za kiserikali.Madaraka mliyopewa msiyatumie vibaya kwa kuwanyima haki yao ya kikatiba watu wengine.
 
CCm kweli ni ile ile,watu wamelewa madaraka kwa siku moja,athari ya lowassa akifanya mikutano ni nini?wanacho ogopa ni nini?Kuna kitu nyuma ya pazia ambacho pm anakiogopa,kushinda au kushindwa lkn suala la kutoa shukhrani liko palepale,watu zaidi ya milioni sita jamani kwa nini asiwashukuru,pm hapo vipi?
 
Asante muh.Kasim Majaliwa. Tuache upuuzi Wa kushukuru. Tujenge nchi. Wazungumze bungeni au kuitisha press conference.

Ulaya na marekani uchaguz ukimalizika, hakuna mikutano ya kisiasa. Siasa huhamia bungeni, kwenye makongamano au mkutano na waandishi Wa habari.

Hongera Waziru Mkuu

Ulaya ya wapi acha unafiki wewe usiyejua ulaya akili tope hiyo.
Chama kinakuwaje kama hakifanyi mikutano?
 
waziri mkuu nakupa big up sana?!!!!!!! Lowasa mkutano wa mini ????? Kama hizo hela zako za kifisadi basis peleka msaada kwa watoto yatima au peleka vitanda mahospitalini kama unataka wasaidia watanzania kwa roho nzuri!!!!

Wanataka wajilipue kama arusha halafu waanze singizia serikali...... Shabaaaaashi....... Amshukuru mke wake na familia yake shabaaaaashi

hapa kazi tu

000000q
 
Siungi mkono hili tamko maana nchi haiendeshwi kwa udikteta au kijeshi, ingekuwa jeshi ndilo limeshika utawala wa nchi, ingekuwa sahihi kabisa lakini kwa democratic state kama tz. so vizuri, waziri mkuu atakuwa aliteleza, unajua ukizungukwa na jeshi la polisi na maofisa mbalimbali wa serikali na walinzi unaweza kuropoka jambo lolote.
 
Duh e1.ELIMU(kwa magufuli) 2.ELIMU(kwa majaliwa) 3.ELIMU (kwa wapiga kula WAP) tatizo yakupewa kazi ya kumchuna ng'ombe wakati umezoea kutoa manyoya shii...t ELIMU upo wp

Usijisahau na wewe pia Elimu, wanaitwa wapiga kura na siyo kula!
 
Kwa kile kinachoitwa mshtuko Waziri mkuu MAJALIWA KASSIM MAJALIWA leo Apiga marufuku mikutano ya kisiasa ya kuwashukuru wananchi hasa kwa wale wagombea walioshindwa uchaguzi.

Nini tafsiri ya hii kitu? Kwa haraka haraka ninavyohisi huu UTAWALA utakuwa ni moja kati ya utawala ambao UTAWALA BORA umewekwa mfukoni na kuongozwa kwa Proclamations and Decrees,Which is not good.

NACHUKUA NAFASI HII KULIKEMEA HILI kwa majina yote

Yaani wewe uliyepost ujinga huu ndiyo unanithibitishia chadema ni kundi la wapuuzi na haitaki watu wawe na maendeleo nchi ilisimama kwa joto la uchaguzi zaidi ya miezi sita nadiriki kusema ni mwaka mzima tumemaliza uchaguzi tena tuanze kufunga biashara kusikiliza wagombea hivi tutakuwa na akili au matope vichwani ????
Nyie mnaoendekeza upuuzi huu tayari mna mapesa yenu ya kutosha mnataka kuwapumbaza watu wasifanye kazi zao na washindwe kulipa ada za watoto wao Mimi binafsi NAUNGA MKONO MAAMUZI YA MHESHIMIWA MAJALIWA KUPIGA MARUFUKU MIKUTANO YOTE YA SIASA KWANI KILA KITU KINA MUDA WAKE HATUWEZI KUISHI KWA SIASA ZA KITAPELI MUDA WOTE.
KAMPENI ZILISHAKWISHA TUFANYE KAZI SASA TUSUBIRI 2020 HAKUNA NAMNA.
 
Asante muh.Kasim Majaliwa. Tuache upuuzi Wa kushukuru. Tujenge nchi. Wazungumze bungeni au kuitisha press conference.

Ulaya na marekani uchaguz ukimalizika, hakuna mikutano ya kisiasa. Siasa huhamia bungeni, kwenye makongamano au mkutano na waandishi Wa habari.

Hongera Waziru Mkuu
Ulaya Na Marekani raka akifanya losa anashitakia ?ta kama yupo madaraka au ameishatoka.Vipi hapo Tanzania
 
Mkuu nina akili timamu na sjaandika kishabiki nimetoa hisia zangu
Kasema wale waloshinda ndo watashukuru ila kwa walioshindwa hawana nafasi hizo zaidi ya kutuvuruga na huu ni wakati wakazi

Huu unaweza tafsirika kama ubaguzi kwan itaonekana kuna tabaka fulan ndo linastahili kupata haki zote na jingine haliruhusiwi
Sio vizuri
Huenda PM aliteleza
Msemaji wa SERIKALI AJITOKEZE
ALIWEKE SAWA!
kama ni kweli basi tujue tumevuka mipaka,huu si wakati uleee nchi bado changa,ngoja nisubiri uthibitisho kwanza
 
Yaani wewe uliyepost ujinga huu ndiyo unanithibitishia chadema ni kundi la wapuuzi na haitaki watu wawe na maendeleo nchi ilisimama kwa joto la uchaguzi zaidi ya miezi sita nadiriki kusema ni mwaka mzima tumemaliza uchaguzi tena tuanze kufunga biashara kusikiliza wagombea hivi tutakuwa na akili au matope vichwani ????
Nyie mnaoendekeza upuuzi huu tayari mna mapesa yenu ya kutosha mnataka kuwapumbaza watu wasifanye kazi zao na washindwe kulipa ada za watoto wao Mimi binafsi NAUNGA MKONO MAAMUZI YA MHESHIMIWA MAJALIWA KUPIGA MARUFUKU MIKUTANO YOTE YA SIASA KWANI KILA KITU KINA MUDA WAKE HATUWEZI KUISHI KWA SIASA ZA KITAPELI MUDA WOTE.
KAMPENI ZILISHAKWISHA TUFANYE KAZI SASA TUSUBIRI 2020 HAKUNA NAMNA.

Uneuona ni ujinga mbona umeleta nyege zako kuchangia kafe wakuzike na makoleo

Ulifaa uzaliwe karne ya 4 enzi za umajinuni

Nakukemea USHINDWE
 
Back
Top Bottom