Waziri Mkuu apiga marufuku kusafirisha chakula nje, ukipewa kibali basi safirisha unga sio mahindi

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Ni marufuku kusafirisha kuuza mahindi nje ya nchi na ukitaka kusafirisha saga hayo mahindi kwanza then omba kibali Serikali.

Serikali inajaribu kukabiliana na njaa kwa watanzania kutokana na uhaba wa mahindi nchini

Na ameongeza ni vizuri kuongea value kwa maana ya kusaga mahindi ambayo itakuwa ni nafuu zaidi kwani itasaidia ajira kwa vijana nchini Kulikoni kuuza mahindi yenyewe

Hayo yamesemwa na Wazuri mkuu Kassim Majaliwa huko Moshi ktk Sikukuu ya Eid leo.

======


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku usafirishaji wa chakula nje ya nchi bila kibali na kuwataka wafanyabiashara kuuza chakula kwenye maeneo yenye uhaba nchini.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Jumatatu wakati akihutubia Baraza la Eid katika Msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu huyo amesema kuwa kuna maeneo ambayo wananchi hawakupata chakula vizuri kutokana na uhaba wa mvua hivyo wafanyabiashara wapeleke chakula kwenye maeneo hayo.

“Serikali bado haijatoa kibali cha kutoa chakula nje ya nchi, kama unaona kuna umuhimu kaombe kibali, lakini utapewa kibali cha kusaga upeleke unga na siyo mahindi,”amesisitiza Majaliwa.

Majaliwa ameonya kuwa kwa wale watakao kamatwa wakisafirisha mahindi nje ya nchi kinyume na utaratibu, mahindi hayo yatataifishwa na kupelekwa kwenye ghala la Taifa na magari yatapelekwa polisi.

Amesema kuwa Serikali imepokea barua za maombi ya kupeleka chakula nchi jirani, lakini bado haijatoa ruhusa.
 
Ni Marufuku Kusafirisha Chakula nje ya Nchi bila ya Kibali, Na Ukipewa kibali sio usafirishe mahindi bali usafirishe Unga

Ukikamatwa unasafirisha Mazao ya chakula nje Bila ya Kibali: Utakamatwa na Mazao hayo yatataifishwa na hilo gari pia litataifishwa na Kupewa jeshi la polisi.

Waziri Mkuu
Kilimanjaro Leo.
 
Naunga mkono serikali kudhibiti utokaji wa chakula nje ya nchi ili kama Taifa tusitumbukie kwenye baa la njaa. Hata hivyo, Gari lina kosa gani jamani??? Mwenye mahindi na mwenye gari wanaweza kuwa watu wawili tofauti. Mwenyezi MUNGU awape hekima viongozi wetu ili wasiwe wanatoa matamko yanayoweza kusababisha dhulma na uonevu kwa wanachi wanaowangoza.
 
Ni Marufuku Kusafirisha Chakula nje ya Nchi bila ya Kibali, Na Ukipewa kibali sio usafirishe mahindi bali usafirishe Unga

Ukikamatwa unasafirisha Mazao ya chakula nje Bila ya Kibali: Utakamatwa na Mazao hayo yatataifishwa na hilo gari pia litataifishwa na Kupewa jeshi la polisi.

Waziri Mkuu
Kilimanjaro Leo.
Huwa nashangaa viongozi wanawapangia sana wakulima nani wamuuzie na kwa bei gani? Mbona masuala mengine kama saruji, Sukari nk hawapigi marufuku. Naomba wakulima wawehuru nao wafaidi jasho lao
 
Gari lina kosa gani jamani??? Mwenye mahindi na mwenye gari wanaweza kuwa watu wawili tofauti. Mwenyezi MUNGU awape hekima viongozi wetu ili wasiwe wanatoa matamko yanayoweza kusababisha dhulma na uonevu kwa wanachi wanaowangoza.

Naona Polisi wa mikoa ya mipakani wanatanuliwa wigo wa Rushwa zaidi
Ukishatishwa Fuso yako itataifishwa lazima uvunje kibubu hata nyumbani washindie uji mwez mzima urudishe gar yako. Unapigwa kama mil 10 hivi unakuja kupanfa foleni ya watu tunaosoma hisabati.

Sema utakua umechelewa topic. Tumemaliza namba za kirumi saivi tupo za kiebrania
 
Wakulima tunaonewa sana. Mbona wao hatuwazuii kwenda nnje kutumia mishahara yao? Hawajui mishahara yetu ndo mavuno hayo?
Bei humu ya chini, basis wanunue mazao yetu kwa bei tunayoipata nnje.
 
Jamani wengine tunalima kwa ajili ya biashara kulima nilime mie halafu baadae mnipangie matumizi
 
Afu tunaulizana kwa nini hatujaendelea. Serikali iwekeze kwetu wakulima ili tuzalishe zaidi. Sio matamko ya kukatishana tamaa. Kilimo hakiwezi kuendelea wenye miraji hawataingia.
 
Sionagi mkono wa serikali kwenye kusaidia wakulima ila wakishavuna serikali iyoooo.
Apo ndo ninapochoka.
Wapeni ata subsidy basi ili mkija ingilia issue zao baada ya mavuno mtaeleweka
 
16256c71d7c0f87299f1f0a52061c859.jpg
 
Gari lina kosa gani jamani??? Mwenye mahindi na mwenye gari wanaweza kuwa watu wawili tofauti. Mwenyezi MUNGU awape hekima viongozi wetu ili wasiwe wanatoa matamko yanayoweza kusababisha dhulma na uonevu kwa wanachi wanaowangoza.
Dhuluma na uonevu utatufikisha pabaya.
 
Gari lina kosa gani jamani??? Mwenye mahindi na mwenye gari wanaweza kuwa watu wawili tofauti. Mwenyezi MUNGU awape hekima viongozi wetu ili wasiwe wanatoa matamko yanayoweza kusababisha dhulma na uonevu kwa wanachi wanaowangoza.
Meli ya vipusa ya kinana unaikumbuka?
 
Serikali ya Tz ime prove total failure kwenye kilimo kwahiyo silishangai hilo

Peasantry,/ subsistance farming /Traditional Agriculture characterictics zake
1.No surplus -Always binadam wana trade surplus
2.Poor methods/small scale/no modernization ,no agricultural fertilizers(low technological capabilities) tunatumia under developed traditional methods kama jembe la mkono, no irrigation etc

3.No industrial diversification ya mazao simple primary producers of raw materials in case ya cash crops

Sasa ulizia watunga sera wa CCM kama kuna siku wamekuja na realistic strategies ya kutukwamua kutoka hapo juu nilipokuelezea instead watamko kiongozi ameshamaliza ,We lack visionary leaders hata hao waliopo wanaendeshwa na mihemko na sio classical philosophies

Thats why better Ujamaa policy ya Nyerere ililenga kukwamua over 90% ya population despite weakness but we saw the real intention

We haujiulizi tumerukia viwanda badala ya kilimo?
 
Meli ya vipusa ya kinana unaikumbuka?
Ndugu yangu usipende kuangalia mambo kwa ushabiki. Mahindi ni zao halali kulima na halali kuuza. Mtu mwenye mahindi kakodi gari langu anataka kusafirisha mzigo wake, kazi ya kutafuta vibali sio ya mwenye gari bali ni ya mwenye mzigo. Kwa mtizamo huu mimi naona kutaifisha gari ni dhulma na ni uonevu mkubwa. Ni sawa na kusema unataifisha ndege abiria aliyesafiri na ndege hiyo akikutwa na madawa ya kulevya. Tusirahisihe mambo, tuyashughulikie kwa hekima na haki. Matamko ya namna hii yanaweza kusababisha uonevu mkubwa sana katika nchi kutoka kwa vyombo vya dola. Hata kutaifisha mahindi mi naona kama si sawa kwasababu kayapata kwa jasho lake mwenyewe ama kwa kununua au kwa kulima. Mtu husika ashughulikiwe kwa kosa la kusafirisha mazao bila kibali sio kunyang'anywa mali halali aliyoitafuta kwa jasho lake.
 
Back
Top Bottom