Waziri Mkuu apiga marufuku kusafirisha chakula nje, ukipewa kibali basi safirisha unga sio mahindi

serikali yetu ya mihemko,wakati our number 1anasema hakuna njaa,Lieutenant wake anatutangazia njaa,mkulima huyu ambaye hakupata support yoyote from gov.eti sasa anawekewa masharti kuhusu mavuno yake,wakulima wakubwa katika nchi zilizoendelea katika kilimo serikali ipo bega kwa bega na wakulima na wafugaji wake ,ikibidi serikali inapunguza makali yanayowakabili wakulima hawa,again tumekulaumu tulikoangukia sio tulipojikwaa.
 
Yuko sahihi Kisiasa
Yupo sahihi Kijamii

Hayupo sahihi Kiuchumi na Kibiashara
Atakuja Bosi wetu Mkuu atasema wakauze popote pale wanapotaka kama alivyotoaga agizo Mwaka Jana kule Shinyanga. Hivyo sisi washabiki na waungaji mkono wa Serikali hii tuwe na angalizo tunaposhabikia kauli ya viongozi wetu. Nakaa kimya mpaka pale atakaposema Mkuu wetu kabisa. Pohamba utarudi tena hapa kuunga mkono kauli ya Mh. Rais inayopinga hii ya WM.

Let's wait
 
Eti kilimo ndio msingi wa maendeleo nendeni mkalime... alafu mtu unaenda kulima kumbe ni ili uje kusaga unga ukauzwe kwenye duka la mangi... khaaaaa
 
Hata kiuchumi yupo sahihi pia
Sababu:
Ikiwa utasafirishwa unga maana yake utasanga kwa mashine za Tz, hivyo utaongeza kipata kwa wamiliki wa mashine pia utasaidia kupatikana kwa ajira kwa wasagaji.
Pia ukisaga unga lazima utaweka ktk vifungashio, hivyo utakuwa umeongeza thamani ya zao husika, vilevile utatoa kodi kwa serikali ambayo itatumika kwa maendeleo ya nchi.
La mwisho, mabaki ya mazao kama pumbs yatauzwa na kulisha wanyama wa Tz. Hivyo serikali IPO sahahi tena imechelewa sana kufanya maamuzi haya.
Lakini lengo sidhani kama ni hilo ifike kipindi tuangalie mambo kwa jicho la tatu. Kikubwa ni kukabiliana na njaa, njaaa IPI na wakati Tanzania haijawahi kuwa na uhaba wa chakula?. Una gunia 20 za mahindi unataka kwenda kuuza Kenya lakini kibali hupewi mpaka usage gunia hizi ishirini ili uruhusiwe juziuza Kenya huku unapigana juu ya njaa na uhaba wa chakula hii inanipa shida kuilewa mantiki yake
 
Nchi ya hovyo sijapata kuona..

Wamesaidia vipi mkulima ajikwamue kwenye kilimo kisicho na tija?
 
Swali sasa watanzania wakishindwa kununua hayo mazao ina maana wakulima watapata hasara. Je serikali itawafidia hasara watakayopata? Hii serikali inaendeshwa na anti business people. Utapigajje vita exportation ya bidhaa ?Kuna mbadala wa kupiga vita njaa lakini sio kama hivi, hii itasababisha mfumuko wa bei kucover transportation costs etc
 
Shamba lako, hata kama ulikodi sawa tu ila ulitumia kwa pesa zako kugharamia vibarua..mbegu..mbolea..palizi..na mahangaiko yote mwenyewe sasa kwenye kuuza mavuno yako serikali inaingilia na kukupangia soko haiingii akilini hata kidogo..

Umelima kwenye ardhi ambayo ni mali ya serikali
 
Tatizo njaa ikukula unaigeukia tena serikali kwamba njaaa njaaa serikali saidia. Serikali inasaidia kwa kukusaidia njisi ya kupanga matumizi yako kama hivyo, huo ndo msaada mkuu wenye tija ndo huo.
Ilime iwauzie wenye njaa, mbona wafanyabiashara hawapangiwi pa kuuza bidhaa zao? Kama hawafanyi wasile mkulu alishasema kama unanjaa kalime hakuna msosi wa msaada vivyohivyo wakulima waachwe wachague soko wanalotaka
 
Je, wameweka vizuri soko la ndani?
Kuropoka sio kazi hata kidogo
....Mahindi ndo yanakauka debe elfu 5, yakivunwa na jinsi yalivyo mengi debe itakuwa elfu 2, nchi hii mkulima ataendelea kuwa maskini. Hakuna msimu uliokuwa mgumu kama huu, mpaka viwavi jeshi walishambulia mazao, sikuona msaada wowote wao wanaibuka kwenye mavuno.
 
Bavicha hamna jema ,ukitokea upungufu kidogo wa chakula mnataka Rais atangaze baa la njaa ,akidhibiti chakula mnalalamika hivi mkoje upstairs?
....Halafu unajiita ndugu wa Trump, nadhani aliona comments zako ndo akasema tuendelee kutawaliwa...
 
Ila kulalamika njaaa njaaa njaaa njaaa ndio serikali iingilie, akili za kina Lisu hizi zitatupeleka shimoni
...Walipolia njaa uliwapa hicho chakula? Una uwezo wa kulisha watanzania asilimia 80 wewe? Acha ulofa wako hapa...
 
When 1+1 = 3 ???????
....Wewe fanya dhihaka but jua kwamba watanzania wengi (ambao ni wakulima) wanaishi maisha ya dhiki sana, sababu kubwa ni ukosefu wa reliable market for their crops. Mwaka juzi nyanya ilivyouzwa debe elfu mbili mluwasaidia? Mwaka huu watakapouza mahindi elfu 20 gunia mtawasaidia?
 
IL
Shamba lako, hata kama ulikodi sawa tu ila ulitumia kwa pesa zako kugharamia vibarua..mbegu..mbolea..palizi..na mahangaiko yote mwenyewe sasa kwenye kuuza mavuno yako serikali inaingilia na kukupangia soko haiingii akilini hata kidogo..
A IKITOKEA NJAA HUSEMI NJAA YAKO SERIKALI INAHUSIKAJE?
 
....Wewe fanya dhihaka but jua kwamba watanzania wengi (ambao ni wakulima) wanaishi maisha ya dhiki sana, sababu kubwa ni ukosefu wa reliable market for their crops. Mwaka juzi nyanya ilivyouzwa debe elfu mbili mluwasaidia? Mwaka huu watakapouza mahindi elfu 20 gunia mtawasaidia?
Hawa wanaoishi kwa taabu hawatakiwi kuuza mahindi sasa hivi!Maana wanalaliwa bei, trust me hakuna mkulima anayepeleka mahindi Kenya!Hao ni middle men wanaolalia bei wakulima wetu!
 
Back
Top Bottom