Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,495
- 51,089
Leo nimemsikiliza waziri mkuu ndugu Majaliwa akiwa kwenye kongamano la viongozi wa dini la kuisifu serikali.
Waziri Mkuu ameutangazia umma wa Watanzania kuwa serikali italinda Amani wakati wote hata kipindi cha uchaguzi mkuu, na akataka siasa za kistaarabu.
Wakati akiyasema hayo, viongozi wa vyama vya ACT-Wazalendo kwa takribani wiki moja sasa wanalaani vikali vitendo vya kinyama, vya utekaji na kujeruhiwa kwa wagombea wao wa ngazi za ubunge na udiwani katika jimbo la Ruangwa ambalo ndilo jimbo la ubunge la waziri mkuu.
Katika press conference iliyofanyika jana, katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo ndugu Ado Shaibu amemtaka Waziri mkuu ambaye ndiye mwenye dhamana ya utendaji wa kila siku wa serikali atumie mamlaka yake kukomesha vitendo hivi vya kihuni, kinyama na kikatili visiendelee katika jimbo lake.
Sisi wananchi tungependa kufahamu; Je, Waziri Mkuu amechukua hatua gani zilizo ndani mamlaka yake ya kuwabaini waliohusika ili sheria ichukue mkondo wake na kukomesha vitendo hivi vya kinyama visitokee tena?
Wananchi tungependa kujua ili tuweze kuiamini kauli yake aliyoitoa leo mbele ya viongozi wa dini kuwa yeye binafsi ataendesha kampeni za kistaarabu, zisizo za uonevu kwa wengine, maana matendo ya utekaji wa wagombea wengine wasio wa chama cha mapinduzi katika jimbo hilo yanatuogopesha sana!