Kwa mbwembwe kabisa waziri mkuu Majaliwa K. Majaliwa alitoa masaa manne tu sukari iwe inauzwa 1800 nchi nzima. Baada ya hapo alipokuwa ziarani Kagera ni kama alinyosha mikono kiaina baada ya kusema amekuta sukari ina kodi nyingi na serikali inaangalia namna ya kuzipunguza.
Sasa hali ni mbaya zaidi, sukari imefikia shilingi 2500. Badala ya kushuka sasa imepaa na haikamatiki. Uamzi wa 'kukurupuka' wa kuzuia sukari inayotoka nje sasa ni shubiri kwa wananchi. Kwa vile tunaambiwa wana kasi inayosifiwa na walio wengi, basi tunatarajia wafanye uamzi kwa kasi kuruhusu sukari ya nje ili kuwapunguzia wananchi maumivu.