Waziri Mkuu amuokoa DED aliyesimamishwa Shinyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu amuokoa DED aliyesimamishwa Shinyanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 26, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Celina Kombani.  Ofisi ya Waziri Mkuu, imemhamisha Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga, Jane Mutagurwa, aliyesimamishwa kazi kwa amri ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mutagurwa amehamishimiwa katika halmashauri ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara atakapoendelea kuwa katika wadhifa huo.
  Uhamisho huo umetangazwa siku chache baada ya baraza hilo, kumsimamisha Mutagurwa kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.
  Taarifa zilizoifikia Nipashe zilieleza kuwa, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( Tamisemi) iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, ilitoa uhamisho huo unaojulikana kuwa wa kawaida.
  Alipoulizwa na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu taarifa hiyo, Mutagurwa, alikiri kupokea uhamisho huo na kwamba ulitolewa tangu Ijumaa iliyopita.
  Mara baada ya madiwani hao kumsimamisha Mkurugenzi huyo, zilisikika tetesi kuwa tayari, alikuwa ameshapata uhamisho kwenda katika kituo chake kipya cha kazi.
  Akizungumzia kuhusu tuhuma zilizotolewa na madiwani dhidi yake, Mutagurwa, alizikanusha na kusema madiwani hao hawakufanya uchunguzi kuhusiana na kadhia hiyo.
  "Hivi sasa tunapozungumza niko wilayani Kiteto, kwani ofisi ya DED wa manispaa ya Shinyanga nimeshakabidhi tangu Ijumaa iliyopita, kwa sasa nipo katika ofisi mpya hapa wilayani Kiteto," alisema.
  Hata hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Celina Kombani, alisema utaratibu uliotumika kufikia uamuzi wa madiwani hao, ni kinyume cha uendeshaji wa halmashauri hapa nchini.
  Kombani, alisema utaratibu unaotakiwa kufanywa na madiwani ni kuandika malalamiko yao kwa Mkuu wa mkoa mwenye mamlaka ya kuyawasilisha Tamisemi na hatimaye kufikishwa kwa Waziri MKuu mwenye mamlaka ya kuwajibisha.
  Pia, Kombani alithibitisha kuhusu uhamisho wa Mutagurwa na kwamba ulifikiwa kabla ya madiwani hao kumtimua.
  “Nipo jimboni lakini taarifa nilizozipata ni kwamba Mkurugenzi huyo amepata uhamisho wa kawaida kwenda halmashauri ya wilaya ya Kiteto..” alisema.
  Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Hassan Mwendapole, alisema uchunguzi wa kina utafanywa kuhusu tuhuma zinazomkabili Mutagurwa na kwamba ushahidi ukithibitika kisheria, atafikishwa mahakamani.
  Mwendapole aliyezungumza kwa njia ya simu kutoka Dodoma, alisema halmashauri ya manispaa ya Shinyanga inatambua kwamba tuhuma zinazomkabili Mutagurwa, hazitofautiani na wahalifu wengine wanaovunja sheria.
  Hata hivyo, alisema kinachomkabili Mutagurwa ni tuhuma, hivyo si vizuri kumhukumu kwa vile hajapatikana na hatia.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Business as usual ya CCM....ukiharibu point A unahamishiwa Point B ukaharibu as if hakuna watu wengine waadilifu au as if huyo muharibifu alizaliwa kuongoza! Mara nyingi mtu kama huyo anakula na wakubwa wengi so 'toto baya, zuri kwa mama yake'. Siamini kwamba baraza la madiwani woooote wawe wendawazimu wamsingizie huyo mama. Madiwani ndio wenye manispaa yao tofauti na hao ma-DED wanaoletwa kutoka wanakotoka. Madiwani wana uchungu na manispaa yao maana wamezaliwa ,wamekulia,wanazeekea na watafia hapo in contrast na hao ma-DED wakuletwa ambao anajua akistaafu au atahamishwa. Kombani ni mwepesi sana wa kupokea zawadi toka kwa watendaji halmasahauri so huwa anawekwa mfukoni sana. Amebadilika sana kama mwenzake Msola tofauti na walivyokuwa SUA. Kombani alikuwa mchapakazi sana (PAO) hata alipoteuliwa na kikwete,wengi tulisikitika lakini sasa system ya kifisadi ishammeza!!!
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Haki ya Mungu!! Kwa mtaji huu unafikiri huyu atajirekebisha!!??? kwa kumwajibisha wangempunguza cheo. Madiwani wanawakilisha wananchi si zani kwa idadi yao watakuwa na chuki binafsi; kama anasingiziwa basi ilikuwa haina haja ya kumwamisha bali kuwaelimisha hao madiwani.
   
Loading...