Waziri Mkuu amsimamisha kazi mweka hazina Kibondo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mweka hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Thomas Chogolo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo.

Mh. Majaliwa amewataka watendaji wa halmashauri huyo kumaliza haraka migogoro yao ya kiutendaji kabla ya Serikali haijawachukulia hatua kwani wanachokifanya ni kinyume na maelekezo yake.

Amechukua hatua hiyo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo.

“Katika Serikali hii suala la ukusanyaji wa mapato ni jambo nyeti na limepewa kipaumbele, hivyo ni lazima fedha inayokusanywa itumike kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.”Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa wananchi wa halmashauri hiyo wanalipa kodi kupitia kwa watendaji wa kata katika maeneo yao lakini mweka hazina haingizi kwenye mfumo wa Serikali.

-ITV
 
Hapa ndipo napo mkubali waziri mkuu,
Anazingatia sheria za utumishi wa Umma.


Sio hawa wanaofukuzafukuza pasipo zingatia sheria walizopitisha wenyeqe bungeni.

Heko Majaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo Kigoma ni balaa sana kila uchwaao ni majanga hayo ya huko yalishatokea hata Manispaa ya Kigoma/Ujiji mabadiliko hakuna kabisa kazi ni kwa mazoea sana labda ashuke malaika pengine mambo yatakaa sawa! Hongera Waziri mkuu kwa hilo ila endelea kuiangalia Kigoma kwa jicho LA tatu Matatizo ni mengi sana hasa ya kiutumishi
 
Back
Top Bottom