Waziri Mkuu amsimamisha kazi Mkurugenzi (DED) wa Wilaya ya Mbozi kwa matumizi mabaya ya madaraka

Who is that barafu? Songwe kuna mmoja amepewa miezi ajirekebishe.
Kusema kweli halmashauri zetu zina ubabaishaji mkubwa kwenye tender na manunuzi ya serikali. Watu wamejisahau sana. Wanakula bila woga hata visivyo vyakwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema kweli halmashauri zetu zina ubabaishaji mkubwa kwenye tender

Normal trend - year in, year out. Nadhani hata CAG keshachoka kuandika kwenye report zake.

Kuna haja sasa ya kwenda one more step. Badala ya kuwasimamisha kazi tu, wanapaswa kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kuwapima stool, mikojo, jasho na damu maDED wote waliokwapua fedha. Bahati mbaya maDED wote wamepachikwa kwa mjuano na inakuwa ngumu kwelikweli kudeal nao. Kila DED ana connection either ya PM, VP, Kinana, Speaker au Malaika mwenyewe
 
Amewasimamisha na watumishi wengine 4 Halmashauri ya Songwe.Kwasababu walikuwa wanapeleka kutengeneza magari gereji binafsi bila kufuata taratibu za zabuni.
 
Hao ma DED si wateula wa mkuu!? Wanapata wapi ujasiri wa kuiba? Au tuseme wsteuliwa na mteuaji ni wale wale??
Who is that barafu? Songwe kuna mmoja amepewa miezi ajirekebishe.
Kusema kweli halmashauri zetu zina ubabaishaji mkubwa kwenye tender na manunuzi ya serikali. Watu wamejisahau sana. Wanakula bila woga hata visivyo vyakwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa TAMMISEMI haendani na kasi ya serikali hii. He is not so much serious.Kwenye halimashauri/manispa kuna mchwa usiokufa hata uweke sumu gani. Kigwangala angafaa kushika TAMMISEMI.
 
Serikali ya uonevu tu hii. Ni kweli wapo watu walioiba, washughulikiwe. Lkn maamuzi ya kutafta sifa siyo kabisa.

Hivi Maja anaujua halimashauri zimechoka, kiasi kwamba hata hawana uwezo wa kutengeneza magari ya halimashauri?

Hivi anajua kwa sasa gari za halimashauri hata tair zinazofungwa kwenye magari ni 2nd to 3rd hand? Yaani mpaka wenye nazo wavue ili wewe ununue tairi la tsh.20,000/- unaweka kwenye gari la serikali?

Hivi anajua kuwa service na matengenezo yote yamebaki ni mzigo wa madereva ambao wanawajibika kutengeneza ili wawe barabarani, maana kama gari lako ni bovu, huna safari yoyote?

Hivi unajua madereva wanawajibika kuchukua sehemu ya mishahara yao au posho kukarabati magari hayo?

Wacheni uonevu, toeni pesa watu wafanye kazi kwa kujiamini, siyo kutishiana kutumbuana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni uongozi wa mihemko na kiki za kipumbavu......yaani waziri mkuu anafuatilia service za magari badala ya kuzungumzia viwanda, serikali inafanya nn kuhakikisha wakulima wananufaika na mazao yao etc anaongea ujingaujinga tu......
 
Mimi nashindwa kuelewa, ukisikia watafuta kick wanasema sasa hivi nidhamu imerejea serekali, rushwa imedhibitiwa sana. Sasa inakuwaje kwenye hili? Huko kuna mkuu wa mkoa na DC mbona hawachukui hatua? Au hao maRC na maDC wao wako active tu kwenye majimbo yenye wapinzani?
 
Magu aliwateua makada wakawe wakurugenzi,baadala ya kuangalia watu sahihi,DC Kada,DED Kada,RC Kada!!!

Ufanisi ni ngumu,zaidi ya deal na kuvutana!!!!
 
Serikali ya uonevu tu hii. Ni kweli wapo watu walioiba, washughulikiwe. Lkn maamuzi ya kutafta sifa siyo kabisa.

Hivi Maja anaujua halimashauri zimechoka, kiasi kwamba hata hawana uwezo wa kutengeneza magari ya halimashauri?

Hivi anajua kwa sasa gari za halimashauri hata tair zinazofungwa kwenye magari ni 2nd to 3rd hand? Yaani mpaka wenye nazo wavue ili wewe ununue tairi la tsh.20,000/- unaweka kwenye gari la serikali?

Hivi anajua kuwa service na matengenezo yote yamebaki ni mzigo wa madereva ambao wanawajibika kutengeneza ili wawe barabarani, maana kama gari lako ni bovu, huna safari yoyote?

Hivi unajua madereva wanawajibika kuchukua sehemu ya mishahara yao au posho kukarabati magari hayo?

Wacheni uonevu, toeni pesa watu wafanye kazi kwa kujiamini, siyo kutishiana kutumbuana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wanaonewa au kazi haiwezekani, wanachokomaa nacho ni nini?

Halmashauri zina watu wasiojua maana ya uadilifu. Ni kujipendelea tu kwenye mambo ya manunuzi. Rushwa iliyoko huko huwezi kuamini. Ndio maana miradi mingi inasuasua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom