Waziri Mkuu aliyefanya kazi chini ya kiwango tokea Uhuru wa Tanganyika

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Tokea Uhuru wa Tanganyika mpaka baadae ikawa Tanzania, tumepata mawaziri wakuu mbalimbali, lakini kwanza sifa ziwaendee hawa, Julius Kambarage Nyerere, Edward Sokoine, Salimu Ahmed Salim, Mizengo Pinda, Warioba. Na Kawawa Rashid,

Hawa wamekuwa mawaziri wakuu wa kuigwa ,kwa busara, ubunifu wa kutatua matatizo na uwezo wa kutenda kazi.
Ni mawaziri wakuu ambao walikuwa wakiweka misingi mbali mbali kwa taifa changa sana, na kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa
Wengine waliofanya kazi kiwango cha Kati ni, Cleopa Msuya, John malecela, na Kassimu Majaliwa mwaka mmoja akiendelea na kasi hii naye atafika mbali. Pia Fredrik Sumaye naye yupo kati.

WAZIRI MKUU ALIYEAIBISHA TASNIA ILE NI EDWARD NGOYAI LOWASSA.

1. Kusimamishwa uwaziri mkuu ni suala la aibu sana.
2. Waziri mkuu aliyekaa muda wa mwaka mmoja na miez 6 lakin bila kuonesha kazi aliyofanya.
3. Waziri mkuu aliyelazimisha baadhi ya taasisi kuidhinisha mambo mbali mbali kwa maslai yake. Kusema kweli alituangusha sana, he underperformed.
 
Kwa sisi tunayemfahamu kikazi Mh Lowasaa huyu jamaa anachapa kazi bwana Tamisemi wanajua na ndiyo maana alipojiuzuru kuna baadhi ya halmashauri walifanya sherehe jamaa aliwabana kisawasawa ana silika kama za Marehemu Edward Moringe Sokoine.

Pamoja na kuhamia CHADEMA lakini utendaji wake kwa muda mfupi alipokuwa Waziri Mkuu ulikuwa una tija kubwa sana.

Kashfa ya Richmond ndiyo imevuma sana kumuondolea sifa ya uchapakakazi wake

Na watumishi chini ya Tamisemi wa najua nini nilikuwa kinatokea ktk ziara zake.

Nakumbuka Tabora kuna Katibu Tarafa mmoja aliuza mshindi ya msaada wa njaa na Lowassa alipotembelea huko huyo bwana hakwenda ktk mkutano na wanainchi wakalalamika.

Lowassa akatuma Gari yake ikamlete yule bwana alipoambiwa unaitwa na Mh Lowassa ktk mkutano yule Katibu Tarafa akapata mshtuko wa moyo na kupoteza maisha kwani alishajua issue imejulikana kwa Waziri Mkuu kuuza mshindi.

Kwenye ukweli wacha tuseme ukweli nakiri nimefanya naye kazi jamaa ni mtenda kazi madhaifu ya kibinadamu kila MTU anayo tu.
 
Yeye mwenyewe alikwishasema kuwa tatizo la yeye kuondolewa ilikuwa ni uwaziri mkuu uliokuwa unatakiwa na sitta(mchafuzi wa katiba), na akasema suala la Richmond alikuwa anafuata maagizo kutoka juu, na akaongezea mwenye ushahidi aupeleke mahakamani ili ashitakiwe, hakuna aliyempeleka mahakamani mpaka leo
 
Kwa sisi tunayemfahamu kikazi Mh Lowasaa huyu jamaa anachapa kazi bwana Tamisemi wanajua na ndiyo maana alipojiuzuru kuna baadhi ya halmashauri walifanya sherehe jamaa aliwabana kisawasawa ana silika kama za Marehemu Edward Moringe Sokoine.

Pamoja na kuhamia CHADEMA lakini utendaji wake kwa muda mfupi alipokuwa Waziri Mkuu ulikuwa una tija kubwa sana.

Kashfa ya Richmond ndiyo imevuma sana kumuondolea sifa ya uchapakakazi wake

Na watumishi chini ya Tamisemi wa najua nini nilikuwa kinatokea ktk ziara zake.

Nakumbuka Tabora kuna Katibu Tarafa mmoja aliuza mshindi ya msaada wa njaa na Lowassa alipotembelea huko huyo bwana hakwenda ktk mkutano na wanainchi wakalalamika.

Lowassa akatuma Gari yake ikamlete yule bwana alipoambiwa unaitwa na Mh Lowassa ktk mkutano yule Katibu Tarafa akapata mshtuko wa moyo na kupoteza maisha kwani alishajua issue imejulikana kwa Waziri Mkuu kuuza mshindi.

Kwenye ukweli wacha tuseme ukweli nakiri nimefanya naye kazi jamaa ni mtenda kazi madhaifu ya kibinadamu kila MTU anayo tu.
Usimlinganishe Sokoine na fisadi
 
Alianzisha shule za kata, ndiye aliyepeleka maji shinyanga baada ya vitisho vya misri. Mizengo Pinda alifanya nini zaidi ya kulia tu bungeni?
Hakuanzisha yeye. Kama hujui wakati wa Mkapa kulikuwa na Mpango wa Elimu ya Msingi (MEM) na Mpango wa Elimu ya Sekondari(MES). Alipoingia JK alikuwa anaendeleza kazi ya mtangulizi wake. Acha kumpa ujiko huyo bwana kwa mahaba ya kijinga!!
 
Back
Top Bottom