Waziri Mkuu aliyefanya kazi chini ya kiwango tokea Uhuru wa Tanganyika

Na aliyeleshindwa kuwafukuza hadi wakuu wa vitengo kwenye halmashauri kwa kudai eti 'hana mamlaka hayo'!?
 
Yeye mwenyewe alikwishasema kuwa tatizo la yeye kuondolewa ilikuwa ni uwaziri mkuu uliokuwa unatakiwa na sitta(mchafuzi wa katiba), na akasema suala la Richmond alikuwa anafuata maagizo kutoka juu, na akaongezea mwenye ushahidi aupeleke mahakamani ili ashitakiwe, hakuna aliyempeleka mahakamani mpaka leo
Lowassa alikuwa mwizi wa kisayansi, jeuri ya kutaka mwenye ushahidi ampeleke mahakamani inatokana na ujuzi wa kuiba kisayansi alijua hakuna wa kujua. Hana la kujitetea adhabu ya kumnyima urais inamtosha.
 
Mawaziri wakuu wa tendaji ni wawili tu,ambao ni Edwards.Moringe na Lowassa.
Akina Sumaye,Pinda,Majaliwa etc hawana kitu...
 
Yeye mwenyewe alikwishasema kuwa tatizo la yeye kuondolewa ilikuwa ni uwaziri mkuu uliokuwa unatakiwa na sitta(mchafuzi wa katiba), na akasema suala la Richmond alikuwa anafuata maagizo kutoka juu, na akaongezea mwenye ushahidi aupeleke mahakamani ili ashitakiwe, hakuna aliyempeleka mahakamani mpaka leo
Waambie John Mnyika na Kubenea walisema wanao ushahidi.
 
Alikuwa chini ya Gavana mwakilishi wa malkia, hujui Ilo?
Watoto wa .com hata historia ya nchi yao hawajui. Ni shida kweli kweli. sijui huko shuleni siku hizi wanafundisha nini? Kama historia ya nchi vijana hawajui kabisa. Anavyouliza utadhani si Mtanzania
 
Siasa mbaya sana hasa za majitaka..

Unaweza vipi kumuhukumu WAZIRI MKUU ambaye akiwa na rais wake kazi waliofanya kwa miaka miwili tu ya uwepo wake haikuweza kufanywa kwa miaka nane iliyobakia.

Waziri Mkuu ambaye UDOM ilijengwa kwa kiasi kikubwa kwa msukumo wake. Chuo cha kisasa cha serikali ya mitaa ambacho ni kati ya vyuo bora hadi kwa mazingira nchini kikiwa na Hadi bwawa la kuogelea kubwa kama la pale Mlimani na majengo ya kisasa.

Ujenzi wa Shule za kata ulikamilika ndani ya miaka miwili ya uwepo wake kwa msukumo na mwaka alioondoka alitaka kuja na mpango wa Zahanati kila Kijiji ambao haukupata kufanyika..

Kwa miaka nane yote angeweza kuwepo, maendeleo yangekuwa makubwa sana kwa kuwa ndio mtu pekee ambaye walikuwa wanaelewana na Rais kwa maana kila mmoja alikuwa anajuwa kujazia udhaifu wa mwenzake ....

Kama rais alikuwa anachukua muda mrefu kufanya maamuzi na mpole mwenzake alikuwa mkali na mtu wa maamuzi.

Kama Rais angeendelea kuwa naye kama waziri mkuu angekuwa moja ya marais bora kabisa kutokea Africa! Hii reli na bandari ya bagamoyo wangekuwa pamoja wangeshaimaliza..

Waliowagombanisha wametupotezea sana muda and of late ashaondoka madarakani ndio anagundua..
 
Tokea Uhuru wa Tanganyika mpaka baadae ikawa Tanzania , tunepata mawaziri wakuu mbali mbali, lakin kwanza sifa ziwaendee hawa , Julius kambarage Nyerere, Edward Sokoine, Salimu Ahmed Salim, Mizengo Pinda, Warioba.

Hawa wamekuwa mawaziri wakuu wa kuigwa ,kwa busara, ubunifu wa kutatua matatizo na uwezo wa kutenda kazi,
Wengine waliofanya kazi kiwango cha Kati ni, Cleopa Msuya, John malecela, na Kassimu Majariwa mwaka mmoja akiendelea na kasi hii naye atafika mbali, Pia Fredrik Sumaye naye yupo kati.

WAZIRI MKUU ALIYE AIBISHA TASNIA ILE NI EDWARD NGOYAI LOWASSA,
1. Kusimamishwa uwaziri mkuu ni suala la Aibu sana.

2. Waziri mkuu aliyekaa muda wa mwaka mmoja na miez 6 lakin bila kuonesha kazi aliyofanya.

3. Waziri mkuu aliyelazimisha baadhi ya taasisi kuidhinisha mambo mbali mbali kwa maslai yake, kusema kweli alitunangusha sana, he underperformed ,
Nilidhani ulikuwa unawachambua mmoja baada ya mwngne kwa kaxi zao, kumbe nia yako ilikuwa ni kumtafta tu Lowassa umuongelee.hongera.
 
Usipende kuzungusha mambo-swali lilikuwa nani alisimamia shule za kata? Hata kama humpendi mtu usipindishe ukweli. Mimi si mpenzi wa EL na shule za kata lakini watu hawawezi kujisifia shule za kata na hapo hapo wsione mchango mkubwa wa EL kwenye hiyo kitu.
Mchango wa miaka 2 tu. Programu ya MES ilikuwepo miaka minne ya mwisho ya Utawala wa Mkapa. Usimpe ujiko kwa mambo asiyostahili. Aliwaonea watumishi kwa kuwasimamisha bila kuwasikiliza mfano Chang'ombe Village ilipoporomoka, lakini akawalaani kina Mwakyembe kwamba hawakumsikiliza (natural justice). Wakurugenzi hawakumgwaya kwa sababu ya utendaji mzuri bali uonevu wa kutowasikiliza!
 
Kwa sisi tunayemfahamu kikazi Mh Lowasaa huyu jamaa anachapa kazi bwana Tamisemi wanajua na ndiyo maana alipojiuzuru kuna baadhi ya halmashauri walifanya sherehe jamaa aliwabana kisawasawa ana silika kama za Marehemu Edward Moringe Sokoine.


Kuchapa kazi ni neno pana sana, hasa linapotumiwa na watu goi goi!
 
Mleta mada naona umekuja kuchekesha tu humu. Lowassa alimfunika hadi Rais Kikwete kwa utendaji wake mahiri na hilo hata serikalini wanakiri hilo!

Nchi ilikuwa inasonga mbele kwa kasi kuu. Ni mmoja wa mawaziri wachache hodari waliowahi kuwepo!
 
wee mtoa mada ni kwamba bado hujawa great thinker, el hakuachishwa, alijiuzulu tu mwenyewe, kwa kuwa aliona kuna maneno mengi yanasemwa juu yake, hata mchunguzi wa richmond, alimwambia ajipimie kwanza uwepo wake hapo, akaona huu ni mchongo, akatangaza kujiuzuli na sio kuachishwa kama unavyopotosha
 
wee mtoa mada ni kwamba bado hujawa great thinker, el hakuachishwa, alijiuzulu tu mwenyewe, kwa kuwa aliona kuna maneno mengi yanasemwa juu yake, hata mchunguzi wa richmond, alimwambia ajipimie kwanza uwepo wake hapo, akaona huu ni mchongo, akatangaza kujiuzuli na sio kuachishwa kama unavyopotosha
Aliachishwa kazi kama hujui Ilo, aliwekwa mtu kati akapewa ushauri akae pembeni, tatizo hamjui propaganda za CCM ndo maana itaendelea kutawala milele wanawachezea wanavyoweza kwa sababu hamna uwezo wa Ku question, na kufikiri kwa kina, miundo inakuwa mbinu kwa kupangwa huelewi hii
 
Usipende kuzungusha mambo-swali lilikuwa nani alisimamia shule za kata? Hata kama humpendi mtu usipindishe ukweli. Mimi si mpenzi wa EL na shule za kata lakini watu hawawezi kujisifia shule za kata na hapo hapo wsione mchango mkubwa wa EL kwenye hiyo kitu.
Hivi ulizaliwa lini? Unajua shule za kata zilianza miaka gani??
 
Back
Top Bottom