Waziri Mkuu akiri 'kukurupuka' kushusha bei ya sukari!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Tunaposema serikali hii wanafanya mambo bila utafiti na kwa style ya zima moto watu hawatuelewi. Kuthibitisha hili jana akiwa Kihanga, Karagwe alisema kwa mbwembwe "niliagiza hivi karibuni kuja kufika saa nne siku hiyo bei ya sukari ishushwe hadi Tsh 1800". Wananchi wakapiga kelele " haijashuka, haijashuka"...

Waziri mkuu akashuka na kusema " Unajua leo asubuhi nimetembelea kiwanda cha Kagera Sugar na kukuta sukari ya kutosha kwenye maghala, shida kubwa nimeambiwa sukari ina kodi nyingi. Sasa tumeamua kuanza mchakato wa kuondoa kodi hizo".

My take: Kama alijua anaanza ziara ya Mkoa wa Kagera na atatembelea kiwanda cha sukari, kwa nini asingesubiri kutoa amri ya kushusha bei ya sukari ili ajionee hayo anayotwambia leo?
 
Hii serikali inaweza kufanya mambo mengine vizuri lakini mengi zaidi itaharibu.

Ni serikali itakayojikuta inatengeneza mikwaruzano mingi na kila mtu, hii ni serikali ya ajabu sana,haina inaemfurahisha, inajifurahisha yenyewe.

Serikali ni,mfumo lakini hii yasasa serikali ni personal, mtu anaamka asubui hajapiga hata mswaki anasema sukari bei iwe hivi au mafuta ya taa bei iwe hivi alafu hakuna kinachotekelezeka maana yake nini kama sio kukurupuka.

Tusubiri, tutaona maajabu mengi.
 
Walipochemka ni kufuta uagizaji wa sukari kabla hawajafanya utafiti manake kila mwenye akili yake anafahamu miaka ya nyuma vibali vilifutwa na nini kilifuata baada ya hapo matokeo yake serikali ya Magu ikawaona wenzake wapumbavu. Ingawaje ni kweli kabisa kwamba tunatakiwa kuwa-favor producers kwa ajili ya uchumi wetu lakini bado serikali ilitakiwa kwanza kutafiti ni kwanini hapo mwanzoni zoezi kama hilo lilikwama ili hatimae waanze kuondoa hivyo vikwazo vya awali kabla ya kuzuia uagizaji! Kinyume chake, wakaamini watendaji wa zamani walikuwa wazembe ndo maana wali-fail huku wakisahau 99% ya hao wazembe bado wamo humo humo serikalini!
 
Kwa hiyo hutaki bei ya sukari kuwa Tsh 1800?

Mchakato wa kupunguza kodi sio suala jipya na halihitaji muda mrefu wa majadiliano.

Siku hizi mnaishi kwa kusubiri kauli tata za viongozi wa serikali ya Rais Magufuli ili mpate sehemu ya kusimama kisiasa!

Kauli tata ikitokea mnakimbia Jamiiforums kuja kusema, MNAONA NILIWAMBIA.

Mmekuwa kama wachawi ambao wako tayari kuhakikisha wengine hawapigi hatua za kimaendeleo!

Kuna baadhi ya watu hawapendi mafanikio ya serikali ya Magufuli!

Kuna wengine bado mko kwenye kampeni za Uchaguzi!

Ni bora kuwa na viongozi wanaofanya maamuzi haraka bila kuogopa kufanya makosa kwa sababu makosa ni sehemu ya kazi na kujifunza lakini vile vile ni muhimu kuwa na viongozi wanaokubali kama wamekosea ili kufanya marekebisho.
 
Hii serikali inaweza kufanya mambo mengine vizuri lakini mengi zaidi itaharibu.

Ni serikali itakayojikuta inatengeneza mikwaruzano mingi na kila mtu, hii ni serikali ya ajabu sana,haina inaemfurahisha, inajifurahisha yenyewe.

Serikali ni,mfumo lakini hii yasasa serikali ni personal, mtu anaamka asubui hajapiga hata mswaki anasema sukari bei iwe hivi au mafuta ya taa bei iwe hivi alafu hakuna kinachotekelezeka maana yake nini kama sio kukurupuka.

Tusubiri, tutaona maajabu mengi.
Ungefanyika utafiti kwanza wa kimyakimya kabla ya kucheza na media. Hakukua na sababu ya kuja kwenye media kabla ya kupata majibu sahihi ya utafiti
 
Kwa hiyo hutaki bei ya sukari kuwa Tsh 1800?

Hiku hizi mnaishi kwa kusubiri kauli tata za viongozi wa serikali ya Rais Magufuli ili mpate sehemu ya kusimama kisiasa!

Kauli tata ikitokea mnakimbia Jamiiforums kuja kusema, MNAONA NILIWAMBIA.

Mmekuwa kama wachawi ambao wako tayari kuhakikisha wengine hawapigi hatua za kimaendeleo!

Kuna baadhi ya watu hawapendi mafanikio ya serikali ya Magufuli!

Kuna wengine bado mko kwenye kampeni za Uchaguzi!
Nani hataki mafanikio ya serikali? we huoni hoja kwenye hii hoja kweli? Au kila kinachofanywa na serikali kwako ni sahihi?
 
Hadi leo sijaona na sioni ule uelekeo kama wa taifa. Kila mtu anakuja na lake. Mara huyu majipu, mara huyu sukari, mara yule nauli za walimu.... Vurugu tupu kwa kwenda mbele. Tukitaka kufanya kila kitu tutaishia kutofanya lolote. Mwezi wa sita huu niulize hiyo Tanzania ya viwanda iko wapi? Au viwanda vya majipu?
 
Nani hataki mafanikio ya serikali? we huoni hoja kwenye hii hoja kweli? Au kila kinachofanywa na serikali kwako ni sahihi?
Kwa hiyo unataka kusema kilichofanywa na serikali kwenye kushusha bei ya sukari na kuthibiti uagizaji holela wa sukari sio sahihi?
 
Haya majamaa hayajui nchi inahitaji uongozi na sio umeneja. Hayatupeleki popote nimegundua
Hata hapa walipotufikisha ni mbele sana! Tulikuwa nyuma sana kimaadili, viongozi hawakuwa wanawajibika, ufisadi ulitawala, na watu tulikuwa tumekata tamaa!
Acheni kujaribu kuwavunja moyo viongozi wetu, ni mafisadi tu wanaoweza kukebehi utawala wa sasa!
 
Ila mi bado naona afadhali ya huyu mwenye uwezo wa kutoa kauli kwa wafanyabiashara wakubwa kuliko wale waliopita
 
Nani hataki mafanikio ya serikali? we huoni hoja kwenye hii hoja kweli? Au kila kinachofanywa na serikali kwako ni sahihi?

looser
Kwa hiyo hutaki bei ya sukari kuwa Tsh 1800?

Mchakato wa kupunguza kodi sio suala jipya na halihitaji muda mrefu wa majadiliano.

Hiku hizi mnaishi kwa kusubiri kauli tata za viongozi wa serikali ya Rais Magufuli ili mpate sehemu ya kusimama kisiasa!

Kauli tata ikitokea mnakimbia Jamiiforums kuja kusema, MNAONA NILIWAMBIA.

Mmekuwa kama wachawi ambao wako tayari kuhakikisha wengine hawapigi hatua za kimaendeleo!

Kuna baadhi ya watu hawapendi mafanikio ya serikali ya Magufuli!

Kuna wengine bado mko kwenye kampeni za Uchaguzi!

watu wa nongwa hao, wana wa wakosoaji; kila kitu kosa
 
Tunaposema serikali hii wanafanya mambo bila utafiti na kwa style ya zima moto watu hawatuelewi. Kuthibitisha hili jana akiwa Kihanga, Karagwe alisema kwa mbwembwe "niliagiza hivi karibuni kuja kufika saa nne siku hiyo bei ya sukari ishushwe hadi Tsh 1800". Wananchi wakapiga kelele " haijashuka, haijashuka"...

Waziri mkuu akashuka na kusema " Unajua leo asubuhi nimetembelea kiwanda cha Kagera Sugar na kukuta sukari ya kutosha kwenye maghala, shida kubwa nimeambiwa sukari ina kodi nyingi. Sasa tumeamua kuanza mchakato wa kuondoa kodi hizo".

My take: Kama alijua anaanza ziara ya Mkoa wa Kagera na atatembelea kiwanda cha sukari, kwa nini asingesubiri kutoa amri ya kushusha bei ya sukari ili ajionee hayo anayotwambia leo?

Nieleze kitu chochote nchi hii, ukianzia na chadema ambacho unashawishika walikifanya au kuamua baada ya tafiti

It takes strong leader to admit where they made mistake

unafikiri ile gia ya angani mbowe alikurupuka au alifanya utafiti? au kuwa Lowassa alifanya utafiti wa kuhamia chadema??

acha siasa

hata kama una lengo zuri kinachokuponza ni hiyo lugha mficho.......''MMEONAAA.....si nilisemaaaa' 'ona sasa'

kwa mfano ukiwa kama mtanzania, uliposikia sukari imeshushwa bei, wewe BINAFSI ulishauri wapi na mahali gani kuwa KODI haijawa considered? HAKUNA!

Kwa hiyo kuanzia kuwaziwa, unawaziwa kwa niaba, unashindwa kukosoa kabla, WALIOAMUA HAYO NDIO WANAOSEMA WAMEKOSEA WATAANGALIA ISSUES ZA KODI ( kitu ambacho haukuwahi hata kuwaz, ...ILA TAFITI UNAZIJUA VIZURI TU)

Looser!
 
Back
Top Bottom