Elections 2010 Waziri mkuu akiilalamikia Serikali anayoiongoza hadharani maana yake nini?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Katika taarifa ya habari ya jana usiku, Redio One walikuwa na habari kuwa waziri mkuu Mizengo Pinda aliungana na wananchi wa mkoa wa Rukwa kulalamika kwa Rais Kikwete juu ya ukosefu wa soko la nafaka na kuomba serikali iiongezee CGR uwezo ili iweze kununua mahindi mengi zaidi kuliko ilivyo sasa.
Nilishindwa kuelewa kwa sababu nijuavyo Waziri Mkuu ndiye mtendaji mkuu wa Serikali na nilishikwa na butwaa kusikia hayo, mpaka sasa siamini kama kweli Pinda alifanya hivyo, lakini kama ni kweli basi hii ni sababu nyingine ya kutoichagua CCM kwa sababu imeshindwa kutekeleza wajibu wake. Imebaki kulalamika bila kutupatia ufumbuzi wa matatizo yetu. Na hii haikuwa mara ya kwanza kusikia watendaji wa serikali wakilalamikia juu ya mambo ambayo yako chini yao. Waziri Mkulo naye alishawahi kulalamika hadharani kuwa makampuni ya madini yanaidanganya serikali juu ya mahesabu yao na kwamba wanatoa takwimu za aina mbili, moja kwa ajiri ya serikali na nyingine kwa ajiri ya wanahisa wao. Je hapa kweli tutafika??
 
Hivi unadhani Pinda ana mamlaka yoyote serikalini zaidi ya kupasha joto kiti cha WM? Serikali imeshikwa na mafisadi, na Pinda kuna habari hazijui kabisa.
 
Hivi unadhani Pinda ana mamlaka yoyote serikalini zaidi ya kupasha joto kiti cha WM? Serikali imeshikwa na mafisadi, na Pinda kuna habari hazijui kabisa.

Hapa umenena kweli! Vinginevyo asingejidhalilisha vile mbele ya ulimwengu
 
Ni yale yaleeeeeeee, "Kikwete kadanganywa na wasaidizi wake.....hao ndo wa kulaumiwa"
 
Back
Top Bottom