Waziri Mkuu: Ajira kwa wageni mgodi wa Taurtz, Igunga -Maalumu

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Huu ni mgodi wa dhahabu kwa jina la Taurtz medium scale cyanide leaching gold processing plant ulioko eneo la Nanga maeneo ya Igunga. Ni mradi ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka 5. Kuna raia toka Uganda, Kenya, India, Zimbabwe walioingia Tanzania kama washauri (consultants), lakini wakiwa nchini wanwekwa kwenye payroll kwa kazi zingine ndani ya mgodi na kuishi kwa miaka mingi.

Ili kuhalalisha kuwepo kwao kwa muda mrefu, wafanyakazi hawa kila wakati huondoka ili wapate border exit stamp kwa siku chache na baadaye hurudi na kuendelea na kazi. Kuna hisia ya mazingira ya rushwa kutumika hadi maafisa wahusika kutolifuatilia. Hisia yetu ni kwamba linafahamika kwa mbunge wa Igunga, Uhamiaji Tabora na hata Mkuu wa Wilaya.

Angalia ushahidi huu:
Sree Rama Murthy #2 kwenye payroll anatambulika kama Project Manager lakini mktaba wake unaonesha aliingia kama consultant mwezi January 2016 na alitakiwa kuondoka 30 April.

Tendai Mabwinye #3 kwenye payrol aliingia kama consultant February 2016 angeondoka by May 2016. Lakini payroll inaonyesha ni labour Manager.

Wote wenye tick kwenye Payroll wana mikataba ya aina hiyo, kazi ambazo wa-TZ wanazimudu kabisa! Hata security Manager anatoka Kenya. Angalia payroll #11
employees.JPG
Consult-2.Kota.jpg
Consult-3.Mabwinye.jpg
Consult-11.Njoki.jpg
 
Safi sana wakuu watalifanyia kazi,

Lakini niulize, hivi tatizo sisi watz ni nini?Uaminifu?
 
Hongera sana mleta uzi. Kazi zote ulizozionyesha hapo kuna Watanzania wengi tu wanaweza kuzifanya na wengine wengi wapo mtaani hawana ajira hasa waliokuwa waajiriwa wa Migodi ya ACACIA....Bulyanhulu na Buzwagi. Hivi kweli tunaleta Experts wa kuja kuwa Plant Operators wakati Operators tunao mtaani kibao, nani katuroga Watanzania? Hapo mtazamo wangu katika hizo nafasi labda huyo Managing Director kuwa Expert ni sawa lakini zilizobakia hakuna haja.
 
Japo umevunja sheria lakini una hoja.
Naamini wahusika watalifanyia kazi..

Hii ndio faida ya JF, nani angesubutu kuanika huu uozo kwa jina lake halisi?
Samaritan, HIYO KAMPUNI NI YA NANI NA WA WAPI?
 
Kama ni kweli, huu ni ushahidi tosha kwamba never listen to what politicians say. Wanasema matters of principles, lakini huku site mambo ni kinyume kabisa. Ndiyo maana tunaitwa wachochezi.
 
Safi sana wakuu watalifanyia kazi,

Lakini niulize, hivi tatizo sisi watz ni nini?Uaminifu?
Tatizo watanzania ni hatujitumi kila ukipewa Nazi unataka kusimamiwa - sasa inakuwa gharama kwa tajiri. Yaani akuajiri wewe (mTanzania) halafu aajiliwe nyampara wakukuangalia! Hii haipo kwa has a waZimbabwe, wao pia wanajiongeza - yaani ukimajiri kama boiler technician, anaweza akatengeneza choo kama imeziba bila kuambiwa na MTU. Lakini mTanzania atakataa nausema hiyo siyo kazi yake na ataendelea kutumia choo hiyo hiyo mbovu (huo ni mfano mdogo). Kubadirisha mind set ya mTanzania ni very costly. Ninayo yasema ndiyo yale Yale anayokumbana NAyO mheshimiwa raising kutoka kwa hats mawaziri. Wanasubiri awasimamie. Watu so far wanaojituma ni Makonda, Lukuvi .... Hivyo msilalamike sana huenda kizazi kijacho kitajifunza kutoka kwa has a wageni - wanatuzidi
 
Mkuu hongera kama hutojali sema nikupe namba ya paul makonda uwasiliane nae maana hao wakuu wa mikoa wengine hawana msaada wowote.

Hongera kw kazi nzuri
 
Tatizo watanzania ni hatujitumi kila ukipewa Nazi unataka kusimamiwa - sasa inakuwa gharama kwa tajiri. Yaani akuajiri wewe (mTanzania) halafu aajiliwe nyampara wakukuangalia! Hii haipo kwa has a waZimbabwe, wao pia wanajiongeza - yaani ukimajiri kama boiler technician, anaweza akatengeneza choo kama imeziba bila kuambiwa na MTU. Lakini mTanzania atakataa nausema hiyo siyo kazi yake na ataendelea kutumia choo hiyo hiyo mbovu (huo ni mfano mdogo). Kubadirisha mind set ya mTanzania ni very costly. Ninayo yasema ndiyo yale Yale anayokumbana NAyO mheshimiwa raising kutoka kwa hats mawaziri. Wanasubiri awasimamie. Watu so far wanaojituma ni Makonda, Lukuvi .... Hivyo msilalamike sana huenda kizazi kijacho kitajifunza kutoka kwa has a wageni - wanatuzidi
Acha ujinga wewe
 
Makonda kafanya nini. Barabara zote za Dar zimejaa mipasuko ama mashimo.
Anachoweza kufanya ni mambo madogo sana yanayoleta publicity tu na kwa harambe siyo kwa bajeti!
 
Back
Top Bottom