Waziri Mkuu aitaka Wizara kutoa taarifa haraka kuhusu Mechi ya Simba na Yanga pamoja na Viingilio vya Mashabiki

Tff wanasikitika, Bodi ya Ligue inasikitika, Serikali nayo iliyosingiziwa kuamrisha mchezo kusogezwa mbele mtendaji mkuu wake naye anasema anataka taatifa toka kwa walioahirisha......yaani ni upuuzi mtu
 
Wasitufanye kuwa Watanzania wote ni mambumbumbu.Tatizo hapa siyo ratiba ya mechi kurudiwa wala siyo mambo ya viingilio vilivyokwisha kuchukuliwa.

Tatizo hapa ni serikali kukiuka kanuni za FIFA kwa kuingilia mambo ya michezo kitu ambacho kitatugharimu kama Taifa.Hivi kama Taifa tumetenda dambi gani hadi tunakuwa tunapata viongozi wapumbavu mfulilizo namna hii?!This is annoying!
Naiona FIFA ikikaribia.
 
Kichekesho. Wapangaji wa ratiba ni TFF kupitia bodi ya ligi na si wizara.
sawa TFF wapange ratiba kisha watutangazie tukaangalie mechi, tena ikiwezekana mwishoni mwa mwezi huu trh 28/5/2021 au trh 29/5/2021, lengo tunataka tuwatie adabu Yanga

yanga waache kudemka.
 
TANZANIA RAHA SANA.....kuna siku mtasikia mtu KABAKWA kwa maelezo (AMRI) kutoka juu, hatari sana hii.....patamu ni hapo kwenye kuwafidia viingilio......
 
Simba ndio waliosababisha.Wachezaji wao wengi wamefunga Ramadhani wakawaambia TFF kuwa watakuwa hawana nguvu sababu ya swaaumu hhivyo wakaomba mchezo uchezwe saa moja usiku baada ya wao kufuturu saa 12 jioni.

Ndipo sisi yanga tukagoma sababu kanuni ya kubadilishwa imekiukwa.
Wanaofunga Simba katika kikosi cha kwanza ni Aishi Manila, Mohamed Hussein na Shomari Kapombe tu. Wanaofunga Yanga Katika kikosi cha kwanza ni Farouk Shikalo, Kibwana Shomari,Adeyun, Mwamnyeto, Lamine Moro, Ninja, Feisal na Saido. Hapo utapata picha na hoja yako.
 
Wapenzi wa mpira kama kweli wako serious lazima kampeni ifanywe hakuna mtu kwenda mpirani mechi hiyo na pesa zao wadai warudishiwe.
Yanga wanakomaa wapewe pointi zao 3. Ishatoka, hakuna mechi iliyoahirishwa hapo.
 
Mimi natarajia wafafanue sababu za kuahirisha kutoka saa 11 kwenda saa 1 na baadae tena kuahirisha kutoka hiyo saa 1 mpaka itakapotangazwa tena. Nini kilisababisha ahirisho la kwanza? Nini kilisababisha ahirisho la pili?

Hayo mengine ya viingilio yapo wazi sana. Vipi kuhusu hasara nyingine za muda na mali? Wanafidiaje? Hakuna wa kufutwa kazi/kujiuzuru?
 
Back
Top Bottom