mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 802
- 725
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka mikoa ambayo bado haijatekeleza agizo lake la kuandaa makongamano ya uwekezaji ihakikishe inafanya hivyo mara moja.
Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Oktoba 19, 2019) wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji kwa mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
“Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi wa mkoa wa Pwani kwa kutekeleza agizo nililolitoa Juni 18, 2018 wakati wa kongamano la tatu la uwezeshaji wananchi kiuchumi la kuhakikisha mikoa yote inaandaa kongamano la uwekezaji na inakuwa na mwongozo wa uwekezaji wa mkoa. Mikoa ambayo haijatekeleza agizo hilo, ifanye hivyo mara moja,” amesema.
Waziri Mkuu amesema mkoa huo umeweza kubaini fursa zilizopo katika mkoa wa Pwani na kuzitangaza kupitia mwongozo wa uwekezaji ambao pia ameuzindua leo.
Amesema kaulimbiu ya kongamano hilo isemayo: ‘‘Ijenge Tanzania, wekeza Pwani mahali sahihi kwa uwekezaji (Build Tanzania, Invest in Pwani, the Best Place for Investment)” ina maana kuwa, licha ya mkoa wa Pwani kubainisha na kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo, unajipambanua vizuri na kuonyesha kuwa ni kwa namna gani umejiandaa na umetengeneza mazingira bora yanayovutia wawekezaji wa ndani na nje.
“Ili kudhihirisha dhamira ya dhati ya kukuza uchumi kupitia viwanda, nimeelezwa kuwa mkoa umetenga hekta 53,016 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambavyo vitatumia rasilmali zilizopo ndani ya mkoa na maeneo mengine ya nchi kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wanachi,” amesema.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe wanasimamia miundombinu inayoelekea kwenye viwanda vilivyopo kwenye maeneo yao.
"Kila mmoja ahakikishe maji, umeme na barabara vinafika kila eneo ambalo mwekezaji anataka kujenga kiwanda. Nitumie fursa hii kuwaomba mlete mabadiliko chanya yanayotokana na maboresho yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano."
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Bibi Angella Kairuki alisema kwamba Serikali imeanza kutekeleza mapendekezo ya mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (Blueprint for Improving Business Environment Regulatory Licensing in Tanzania) kwa kuondoa tozo 163 zilizokuwa zikilalamikiwa na wawekezaji.
“Pia tumetenganisha majukumu ya TBS ya TFDA ambayo sasa ni TMDA. TBS itashughulika na vyakula na TMDA itashughulika na dawa na vifaatiba. Vilevile, tumeondoa ada za usajili sehemu za kazi ambazo zamani ilikuwa ni sh. 28,000 na sasa hivi zinatolewa bure,” alisema.