Waziri Mkuu aitaka halmashauri ya wilaya ya Itigi kurejesha sh. milioni 100

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1570195389040.png

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kurejesha sh.100.9 milioni zilizotengwa na Serikali kwa shughuli maalumu ambazo halmashauri hiyo ilibadilisha matumizi yake.

Katika hatua nyingine amemtaka Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Likilimke Otto kureshesha sh.milioni 1.6 alizolipwa kama posho za kwenda Dodoma kikazi ambapo pia amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Charles Fussi kupeleka sh.100 milioni Benki ya CRDB wilayani humo zilirejeshwa na madiwani baada ya kupewa mkopo na benki hiyo lakini hajazipeleka na riba yake kuwa kubwa.

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo wilayani Manyoni katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Singida wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo leo."Kuna fedha tulizileta katika Halmashauri yenu ya Itigi sh.100.9 lakini mmezibadilisha matumizi nataka mzirejeshe na wewe mweka hazina nataka mpaka siku yangu ya mwisho ya

ziara uniletee stakabadhi za malipo ya kurejesha fedha hizo" alisema Majaliwa.Majaliwa aliwata watumishi wa umma kuacha kukaa ofisini badala yake watumie siku tatu za wiki kwenda kuzungumza na wananchi ili kujua kero zao na kutafutiwa ufumbuzi.Alizitaka halmashauri zote nchini kutafuta vyanzo vya mapato na kutumia fedha hizo kwa miradi mikubwa badala ya kusubiri fedha kutoka serikali kuu.

Majaliwa alitumia nafasi hiyo kwa kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kusimamia vizuri fedha za miradi zinazotolewa na serikali. Katika ziara hiyo wilayani Manyoni aliweza kukagua ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Kintiku Lusilile, shamba la korosho la Misigati na Katika wilaya ya Itigi kuweka jiwe la msingi la jengo la ofisi ya halmashauri hiyo.
 
Huyu kila akifanya ziara ni lazima aibue madudu na hata kung'oa watendaji wa serikali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom