Waziri Mkuu afuta posho kwa watumishi wa umma nchini

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276


Waziri Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya posho mbalimbali zisizokuwa za kisheria zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.

“Kuanzia sasa marufuku Wakurugenzi kutoa posho zisizotambulika kisheria zikiwemo za mazingira magumu, kujenga uwezo na vitafunwa katika halmashauri zenu na badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo,” amesema.

Agizo hilo litawezesha Jiji la Dar es Salaam kuokoa sh bilioni 130 zilizokuwa zitumike na Halmashauri na Manispaa za jiji hilo, ambazo kwa sasa zitaingizwa kwenye miradi na shughuli za maendeleo.

“Katika halmashauri zetu kila mtumishi anashiriki katika ukusanyaji wa mapato hadi walinzi, lakini mwisho wa siku vitafunwa huliwa na wachache wanaojiita wakubwa huku wengine wakisikilizia kwa nje. Jambo hili haliwezekani,” amesisitiza.
=====

JAMII LEO


Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Mkurugenzi yeyote atakayebainika kulipa posho hizo baada ya siku ya leo atakuwa amejifukuzisha kazi.

Aidha, ameagiza fedha zilizokuwa zikitolewa kwa madiwani kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo zisitolewe moja kwa moja kwa madiwani na badala yake zipelekwe kwenye kata husika na zifuatiliwe matumizi yake.
 
Posho gani zilizopigwa marufuku za serikali kuu na serikali za mitaa/halmashauri za wilaya/manispaa, overtime, posho ya wafanyakazi kuwa na makazi mawili rasmi Dodoma & Dsm, uhamisho, posho ya vikao ?

Manake matamko yasiyosema bila shaka yoyote baadaye tutasikia ''ufafanuzi'' ukipiga uzi/ nukuu ya taarifa hii nzuri ya Francis12
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom