Waziri Mkuu afurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma, ikiwa kati ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi nchini.

Akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali jana jioni (Jumapili, Januari 3, 2016) katika ukumbi uliopo Ikulu ndogo Songea, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa kuhakikisha kuna upatikanaji wa masoko kwa mazao mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa msukumo kwa wananchi.

Pia, ameupongeza uongozi wa mkoa huo kwa kutoa msukumo kwa wananchi na kufanyakazi, na kusema ni jambo linalosaidia kupanda kwa pato la mtu mmoja mmoja, hata hivyo hakusita kuwashukuru kwa mapokezi makubwa aliyopata.

“Nawapongeza sana wana Ruvuma kwa kuongeza pato la ndani kutoka kutoka shilingi 654,227, hadi kufikia shilingi 1,800,000 kwa kipindi cha mika 4 tuendelee kujiweka vizuri kwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa pia amesisitiza kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yote yenye mabonde ili wakulima waweze kuvuna bila kutegemea sana kipindi cha masika. Amesema ni lazima kuimarisha huduma muhimu na kusisitiza matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika mazao hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Ruvuma hutegemea kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara yakiwemo mahindi, mpunga ambao unalimwa sehemu za Tunduru na Songea vijijini, korosho ambazo zinalimwa sehemu za Tunduru, Namtumbo, Nyasa, Mbinga na Songea vijijinina tumbaku maeneo ya Namtumbo,Mbinga na Songea vijijini.

Alisema, Ruvuma imekua ikizalisha chakula kwa kiwango cha utoshelezi na ziada kwa kipindi cha mwaka 2012 – 2013, 2013 – 2014 hali hiyo imeendelea kuwa nzuri hadi kipindi cha mwaka 2015 – 2016. Mahitaji yakiwa ni tani 469,172 na ziada ikiwa tani 1,950,111, ametaja baadhi ya sababu za ongezeko hilo la tani ni pamoja na matumizi ya dhana bora za kilimo, matumizi ya pembejeo za kisasa na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo, aliongeza Mkuu wa Mkoa.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye jana (Jumapili, Januari 3, 2016) ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, kesho siku ya jumatatu atakuwa na shughuli za kufungua tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songea na kukagua Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Kupitia ziara hii Serikali ina lengo la kuona hali halisi ya utendaji wa shughuli za maendeleo kutoka kwa watendaji mbalimbali, kuwatia moyo na kuweka msisitizo katika maeneo yaliyopewa kipaumbele hasa katika sekta ya Afya.
 
Last edited by a moderator:
Kama mazao ni mengi hivyo tujiandae kwa el nino kama inavyoelezwa kila kukicha kuwa madhara yake yatakuwa makubwa sana.
Tujihadhari tu na Mungu yupo
 
Uwepo wa chakula cha kutosha songea sio habari mpya kwa songea/ruvuma.
Waziri mkuu alitakiwa sio tu kuona mambo mazurimazuri na kufichwa yale mabaya bali aelezwe na kuona hali halisi ya huduma za jamii hasa afya, maji na umeme. Tatizo viongoz wetu wanaogopa kuonesha matatizo ya wananchi kwa kuwazungusha viongoz wakubwa sehem nzurinzuri tu wkt inatakiwa kiongoz mkubw km huyo aone halisi ilivyo ili nae akawaungurumie wanaohusika huko mbeleni.
 
Nimeipenda hii ya kua na ziada ya chakula ya tani 1.9milioni. Hiv ndo tz inatakiwa kua.
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma, ikiwa kati ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi nchini.

Akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali jana jioni (Jumapili, Januari 3, 2016) katika ukumbi uliopo Ikulu ndogo Songea, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa kuhakikisha kuna upatikanaji wa masoko kwa mazao mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa msukumo kwa wananchi.

Pia, ameupongeza uongozi wa mkoa huo kwa kutoa msukumo kwa wananchi na kufanyakazi, na kusema ni jambo linalosaidia kupanda kwa pato la mtu mmoja mmoja, hata hivyo hakusita kuwashukuru kwa mapokezi makubwa aliyopata.

“Nawapongeza sana wana Ruvuma kwa kuongeza pato la ndani kutoka kutoka shilingi 654,227, hadi kufikia shilingi 1,800,000 kwa kipindi cha mika 4 tuendelee kujiweka vizuri kwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa pia amesisitiza kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yote yenye mabonde ili wakulima waweze kuvuna bila kutegemea sana kipindi cha masika. Amesema ni lazima kuimarisha huduma muhimu na kusisitiza matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika mazao hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Ruvuma hutegemea kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara yakiwemo mahindi, mpunga ambao unalimwa sehemu za Tunduru na Songea vijijini, korosho ambazo zinalimwa sehemu za Tunduru, Namtumbo, Nyasa, Mbinga na Songea vijijinina tumbaku maeneo ya Namtumbo,Mbinga na Songea vijijini.

Alisema, Ruvuma imekua ikizalisha chakula kwa kiwango cha utoshelezi na ziada kwa kipindi cha mwaka 2012 – 2013, 2013 – 2014 hali hiyo imeendelea kuwa nzuri hadi kipindi cha mwaka 2015 – 2016. Mahitaji yakiwa ni tani 469,172 na ziada ikiwa tani 1,950,111, ametaja baadhi ya sababu za ongezeko hilo la tani ni pamoja na matumizi ya dhana bora za kilimo, matumizi ya pembejeo za kisasa na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo, aliongeza Mkuu wa Mkoa.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye jana (Jumapili, Januari 3, 2016) ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, kesho siku ya jumatatu atakuwa na shughuli za kufungua tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songea na kukagua Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Kupitia ziara hii Serikali ina lengo la kuona hali halisi ya utendaji wa shughuli za maendeleo kutoka kwa watendaji mbalimbali, kuwatia moyo na kuweka msisitizo katika maeneo yaliyopewa kipaumbele hasa katika sekta ya Afya.
Hadithi kama za serikali iliyopita zimeanza,badala ya kutatua kero yeye anaanza kusifia na kutupia wengine watafute soko
 
Back
Top Bottom