Waziri Mkuu afanya mkutano na watumishi wa ofisi yake kuwafariji kuhusu safari ya kuhamia Dodoma

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961


Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekutana na watumishi wa ofisi yake na kuongea nao kuhusu safari ya kuhamia Dodoma.

Amesema wamezoea kuishi Dar lakini sasa hivi wanaondoka na ni kweli wanaondoka, amesema kuhamia Dodoma ni moja ya ahadi zilizopo kwenye ilani ya CCM lakini ilianza mwaka 1973 na Dar itabaki kuwa mji wa biashara.

Ofisi ya waziri mkuu ndio inatakiwa ianze na wengine wafuate ambapo inatakiwa ihamie tarehe moja Septemba.

Amesema wengi wana maswali na wasiwasi kuhusu sehemu ya kwenda kukaa lakini amewatoa wasiwasi na kuwaambia kuwa Dodoma ina majengo mengi sana
 
naogopa kuicheza video nahofia bundle,yote kasababisha magufuli

Kivipi wakati umeshaambiwa ni Ilani ya chama? Yeye ni mtekelezaji tu! Ndio hapo mjifunze kuzisoma na kuzielewa ilani za vyama; au huwa mnaziona kama makaratasi yasiyo na impact?
 
Maskini ila nawahurumia. wanapiga makofi kinafki. lkn ndio hivyo tena hawana namna nyingine zaidi ya kukubaliana
 
Kivipi wakati umeshaambiwa ni Ilani ya chama? Yeye ni mtekelezaji tu! Ndio hapo mjifunze kuzisoma na kuzielewa ilani za vyama; au huwa mnaziona kama makaratasi yasiyo na impact?
Mengi sana yanaizingizia ilani....ni kama vile wakati wanatoa ilani yao sisi hatukuwepo!
 
Watumishi wa Umma ambao wao watakwenda Dodoma wajiandae tu kisaikolojia maana zoezi hili halikwepeki kwa Magufuli na hali hiyo imeongezwa spidi na Jiji la Dar kuwa chini ya Ukawa! Magufuli hawezi kuwa chini ya Ukawa na huu ndio ukweli! Mbona suala hili halikusisitizwa namna hii wakati wa kampeni?
 
"Serikali ina majengo mengi sana Dodoma". Sasa hayo majengo hayakuwa yakitumiwa na taasisi za serikali? Yalikuwa yako wazi tu yanasubiri siku serikali ikiamua kuhamia ndo yatumike? Wanasiasa ni noma.
Ndugu kwa taharifa yako, makampuni ya ujenzi karibu yote ya nchi nzima yapo dodoma. Ihumwa sasa wizara zinajegwa kama uyoga, kuamia hamna litakalo shindikana.
 
Back
Top Bottom