Waziri Mkuu aagiza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kutopewa mradi huku akimtaka Mtendaji Mkuu kujitathmini

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro ajitathmini kuhusu utendaji kazi wake huku akiwasimamisha kazi wakurugenzi watatu wa wakala huo.

“TBA tunaihitaji lakini watu wake wana shida. Hatuwezi kuwaacha, TBA wasipewe miradi kwa sababu hawawajibiki na wanadhani kwa kuwa ni taasisi ya Serikali ndio wataachwa wafanye mambo ya hovyo.”

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi wakurugenzi hao leo (Jumatatu, Novemba 18, 2019) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi, Arch.Humphrey Killo, Kaimu Meneja wa Miradi, Abdallah Awadh na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushauri Arch. Hamis Kileo.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika miradi mbalimbali waliyopewa na Serikali ukiwemo ujenzi wa jengo la NEC ambalo ujenzi wake ulianza Julai, 2017 na ulitakiwa ukamilike Juni 2018 kwa gharama ya sh. bilioni 13. Hata hivyo mradi huo bado haujakamilika na ujenzi wake umesimama.

Akiwa katika eneo la mradi wa ujenzi wa ofisi ya NEC Waziri Mkuu alihoji sababu za mradi huo kutokamilika kwa wakati ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi alisema jengo hilo limeshindwa kukamilika kwa sababu wakati walipokuwa wanaanza kazi walibaini kuwa kuna vitu vilisahaulika wakati wa uandaaji wa Bill of Quantities(BOQ). TBA ndio waandaaji wa ramani ya jengo hilo na ndio wajenzi.

“Bajeti ya awali ilikuwa sh. bilioni 10 wakati wa uandaaji wa michoro ya ujenzi gharama ziliongezeka na kufikia sh. bilioni 13 ambazo ndizo tulikubaliana katika mkataba. Wakati tunaendelea na kazi tuligundua kuna vitu vimesahaulika kwenye BOQ jambo lililoongeza bajeti ya ujenzi na kufikia sh. bilioni 32.” Amesema Arch. Killo.

Waziri Mkuu akahoji tena “kutoka sh. bilioni 13 hadi kufikia sh. bilioni 32 je unaona inakuja vizuri hiyo” sh. bilioni 10 hadi sh. bilioni 13 tena hadi sh. bilioni 32 inazungumzikaje hii na je mwenye jengo mlikubaliana naye? Awali mwenye mahitaji alisema ana sh. bilioni 10 sasa imefikaje 32 je mlimshauri muhusika kuhusu ongezeko hili?

Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi Arch. Killo alipotakiwa kueleza sababu za kuongezeka kwa gharama za ujenzi huo amesema waligundua tofauti wakati wakiwa kwenye eneo la ujenzi kwamba kuna kazi zilitakiwa zifanyike lakini katika mkataba hazipo na hawakuwasiliana na muhusika.

Miongoni mwa vitu vilivyosahaulika katika BOQ ya mradi huo ni pamoja na kutokuwepo kwa ghorofa ya nne katika jengo moja wanalolijenga katika mradi huo ambalo ni la ghorofa nane, pia hapakuwa na paa la jengo la kuhifadhia vifaa mbalimbali vya NEC.

Waziri Mkuu amesema miradi mingi inayojengwa na TBA katika maeneo mbalimbali imeshindwa kukamilika kwa wakati, hivyo amemwagiza Waziri wa NchiOfisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama asitishe mkataba huo wa ujenzi na atafutwe mkandarasi mwingine aje amalizie.

“Jengo la TAMISEMI lililopo katika mji wa Serikali limejengwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.7, nyie wataalamu gani na kwa nini tuendelee kuwaacha ndani ya taasisi? TBA hamfanyi kazi vizuri wakuu wa mikoa na wilaya wanalalamika majengo hayakamiliki ni Serikali gani itakayowavumilia, mmeshindwa kutambua majukumu yenu.”

Waziri Mkuu ameagiza mkandarasi atakayepatikana ahakikishe mradi wa ujenzi huo unakamilika katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa na lijengwe kwa kutumia mfumo wa force account.
 
Hebu twende taratibu kidogo...yaani jengo la ghorofa nane limekosa ghorofa ya nne?????
kwa hiyo kwenye kuhesabu wakaona la kwanza hadi la tatu yapo ila la nne halipo halafu yakendelea la tano hadi nane
Duh!!!!! Something wrong and weird is heading toward our country.
 
Kwa TBA hili si la kushangaza...

Kuna sehemu nondo za ghorofa moja za beam & 1st floor yoote zilisahaulika kwenye BOQ...

Mjengo ulikuwa wa Serikali...

Lilichua muda sana kukalimika na gharama zaidi...

Hi FALSE AKAUNTI ingeanza kipindi hicho tungejenga miundu mbinu mingi sana kwa gharama nafuu...
 
Mkuu sio FALSE ACCOUNT.. nimecheka sana.. 😂😂😂😂 or you interpreted on your own way.
 
TBA wanaonewa bure, walipewa kazi nje ya uwezo wao, serikali ilipoingia ilidhani tba inaweza kufa ya kila kitu hivyo ikapewa tenda zote nje ya uwezo wao kifedha, rasilimali watu na vifaa unategemea wangefanyaje?

TBA ni Class I contractor, meaning wana uwezo wa kila kitu ktk ujenzi wa majengo yote, yaani manpower, technology + financial capabilities. Sasa sijui kwanini TBA ni wazembe sanaaa sanaa, miradi kibao inashindwa kumalizika na gharama zao ziko juu sana sana, Mh. Rais pia alihoji pale Vingunguki ktk ujenzi wa machinjio ya kisasa yaani ghorofa 2 na basement 1 eti gharama ni Bil 14. Na wajenzi ni hao hao TBA, kuna uwizi pale sana inaonekana.. TBA gharama zao sijui wanatoa wapi, hatari sana, i wish i could be PM, hiiii hiiii TBA ningepitisha uchunguzi mkaliiii sana sbb hizi gharama na uzembe ningefukuza woteee alafu naajiri wapya haraka sana.. Hiii hiiii😲😲
 
Hapo ndio utajua kuwa Siasa na Fact havishikamani... Toeni Pesa.. kwani huyo Mkandarasi Mwingine atajenga kwa free? Waziri Mkuu anachotakiwa ni Kuanzisha upya Mchakato aweke viongozi wengine au hao hao halisi ni halisi hayao mambo ya TBA kuweka quotation ndogo ipo kisiasa zaidi ili kuwanyima watu kazi za ujenzi so TBA waache Siasa wapewe upya kazi na waweke gharama halisi mezani kazi ianze.. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni... TBA kawabeba kwa Wananchi kwa kuweka Quotation ndogo na nyie Msiwafukuze kazi kisiasa na hadharani kumbukeni fadhira...
 
TBA wana lack compitent Engineers,QS na Architects,kuna wakati tuliwashauri watumie Consultant Firms na wao wabaki kama Coordinators wakakataa.
Na tuliwashauri wapewe ruhusa ya kuajili Professionals au kuunda vikosi kazi kutoka kwenye Consulting firms na labour force kutoka JKT au kutumia contractor labour based contract wakakataa.
Ni ngumu sana mtu mmoja kufanya kila kitu (design,quantities,construction na supervision).
Nashauri kabla ya kuwatowatumia katika ujenzi wa miradi yote waendelee na miradi michache kama pilot ya kuwapima.
Lakini pia Serikali itazame upya ushiriki wa sekta binafsi katika majenzi hasa washauri kwani ndio walimu/mentors wa wanafunzi/graduates,hivyo ushiriki wao ni muhimu kuandaa wataalamu wa kesho.
Thamani ya pesa katika miradi husika itaonekana kwa kuzingatia kuwa quality control & assurance ya kazi itakuwa valid w.r.t gharama za ujenzi,muda na scope ya kazi kwa kuzingatia kuwa teamworks ni kutoka entity tofauti na hivyo kusaidia kwa karibu check & balance na kujisahihisha mapema kama kuna kosa.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro ajitathmini kuhusu utendaji kazi wake huku akiwasimamisha kazi wakurugenzi watatu wa wakala huo.

“TBA tunaihitaji lakini watu wake wana shida. Hatuwezi kuwaacha, TBA wasipewe miradi kwa sababu hawawajibiki na wanadhani kwa kuwa ni taasisi ya Serikali ndio wataachwa wafanye mambo ya hovyo.”

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi wakurugenzi hao leo (Jumatatu, Novemba 18, 2019) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi, Arch.Humphrey Killo, Kaimu Meneja wa Miradi, Abdallah Awadh na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushauri Arch. Hamis Kileo.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika miradi mbalimbali waliyopewa na Serikali ukiwemo ujenzi wa jengo la NEC ambalo ujenzi wake ulianza Julai, 2017 na ulitakiwa ukamilike Juni 2018 kwa gharama ya sh. bilioni 13. Hata hivyo mradi huo bado haujakamilika na ujenzi wake umesimama.

Akiwa katika eneo la mradi wa ujenzi wa ofisi ya NEC Waziri Mkuu alihoji sababu za mradi huo kutokamilika kwa wakati ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi alisema jengo hilo limeshindwa kukamilika kwa sababu wakati walipokuwa wanaanza kazi walibaini kuwa kuna vitu vilisahaulika wakati wa uandaaji wa Bill of Quantities(BOQ). TBA ndio waandaaji wa ramani ya jengo hilo na ndio wajenzi.

“Bajeti ya awali ilikuwa sh. bilioni 10 wakati wa uandaaji wa michoro ya ujenzi gharama ziliongezeka na kufikia sh. bilioni 13 ambazo ndizo tulikubaliana katika mkataba. Wakati tunaendelea na kazi tuligundua kuna vitu vimesahaulika kwenye BOQ jambo lililoongeza bajeti ya ujenzi na kufikia sh. bilioni 32.” Amesema Arch. Killo.

Waziri Mkuu akahoji tena “kutoka sh. bilioni 13 hadi kufikia sh. bilioni 32 je unaona inakuja vizuri hiyo” sh. bilioni 10 hadi sh. bilioni 13 tena hadi sh. bilioni 32 inazungumzikaje hii na je mwenye jengo mlikubaliana naye? Awali mwenye mahitaji alisema ana sh. bilioni 10 sasa imefikaje 32 je mlimshauri muhusika kuhusu ongezeko hili?

Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi Arch. Killo alipotakiwa kueleza sababu za kuongezeka kwa gharama za ujenzi huo amesema waligundua tofauti wakati wakiwa kwenye eneo la ujenzi kwamba kuna kazi zilitakiwa zifanyike lakini katika mkataba hazipo na hawakuwasiliana na muhusika.

Miongoni mwa vitu vilivyosahaulika katika BOQ ya mradi huo ni pamoja na kutokuwepo kwa ghorofa ya nne katika jengo moja wanalolijenga katika mradi huo ambalo ni la ghorofa nane, pia hapakuwa na paa la jengo la kuhifadhia vifaa mbalimbali vya NEC.

Waziri Mkuu amesema miradi mingi inayojengwa na TBA katika maeneo mbalimbali imeshindwa kukamilika kwa wakati, hivyo amemwagiza Waziri wa NchiOfisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama asitishe mkataba huo wa ujenzi na atafutwe mkandarasi mwingine aje amalizie.

“Jengo la TAMISEMI lililopo katika mji wa Serikali limejengwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.7, nyie wataalamu gani na kwa nini tuendelee kuwaacha ndani ya taasisi? TBA hamfanyi kazi vizuri wakuu wa mikoa na wilaya wanalalamika majengo hayakamiliki ni Serikali gani itakayowavumilia, mmeshindwa kutambua majukumu yenu.”

Waziri Mkuu ameagiza mkandarasi atakayepatikana ahakikishe mradi wa ujenzi huo unakamilika katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa na lijengwe kwa kutumia mfumo wa force account.
Salam zimefika kwa mamlaka ya uteuzi. Jamaa anapotoka ofisini abebage kila kitu.
Majaliwa akikuongelea hivi ujue mkulu anakutumbua.
 
Katika miradi ya ujenzi Kuna kitu wataalam wanaita variation. Lakini sijawahi ona variation ambayo inashusha BoQ kuwa ndogo. Siku zote huwa naona variation ambayo inafanya BoQ kuwa kubwa.
 
Variations kwenye contract nyingi haitakiwi kuzidi 15% ya gharama ya mradi.
Inaweza kuzidi 15% iwapo contract husika ni design & build.
 
TBA ni Class A contractor, meaning wana uwezo wa kila kitu ktk ujenzi wa majengo yote, yaani manpower, technology + financial capabilities. Sasa sijui kwanini TBA ni wazembe sanaaa sanaa, miradi kibao inashindwa kumalizika na gharama zao ziko juu sana sana, Mh. Rais pia alihoji pale Vingunguki ktk ujenzi wa machinjio ya kisasa yaani ghorofa 2 na basement 1 eti gharama ni Bil 14. Na wajenzi ni hao hao TBA, kuna uwizi pale sana inaonekana.. TBA gharama zao sijui wanatoa wapi, hatari sana, i wish i could be PM, hiiii hiiii TBA ningepitisha uchunguzi mkaliiii sana sbb hizi gharama na uzembe ningefukuza woteee alafu naajiri wapya haraka sana.. Hiii hiiii😲😲
Machinjio ya vingunguti wajenzi ni NHC, acha kudanganya.
 
Salam zimefika kwa mamlaka ya uteuzi. Jamaa anapotoka ofisini abebage kila kitu.
Majaliwa akikuongelea hivi ujue mkulu anakutumbua.
Mh.Majaliwa anaweza akawafukuza ma-boss wa Tanroads kama alivyofanya kwa hawa wa TBA?
 
TBA ni Class A contractor, meaning wana uwezo wa kila kitu ktk ujenzi wa majengo yote, yaani manpower, technology + financial capabilities. Sasa sijui kwanini TBA ni wazembe sanaaa sanaa, miradi kibao inashindwa kumalizika na gharama zao ziko juu sana sana, Mh. Rais pia alihoji pale Vingunguki ktk ujenzi wa machinjio ya kisasa yaani ghorofa 2 na basement 1 eti gharama ni Bil 14. Na wajenzi ni hao hao TBA, kuna uwizi pale sana inaonekana.. TBA gharama zao sijui wanatoa wapi, hatari sana, i wish i could be PM, hiiii hiiii TBA ningepitisha uchunguzi mkaliiii sana sbb hizi gharama na uzembe ningefukuza woteee alafu naajiri wapya haraka sana.. Hiii hiiii
Mkuu Class A contractor ikoje hii kwenye mfumo wa CRB? Maana wao wana Class I, II, III -VII.

Hiyo Class A vipi wameanzisha utaratibu mpya wa kusajiri kampuni?
 
Wanatoa gharama ndogo kumfurahisha fulani kama kawaida halafu wanadai wamesahau kuorodhesha baadhi? Hapo hakuna kutumbua kwani wahusika ni wapendwa.
 
Salam zimefika kwa mamlaka ya uteuzi. Jamaa anapotoka ofisini abebage kila kitu.
Majaliwa akikuongelea hivi ujue mkulu anakutumbua.
Si mpaka, hao ni kama tanroads, wapendwa. Mambo ya expansion joints hayakutimuwa mtu kwenye hostel, ndio kwanza wakatangazwa hadharani kila tenda wapewe wao
 
Back
Top Bottom