Waziri Mkuu aagiza Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga achunguzwe

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bibi Judica Omari achunguze utendaji kazi wa Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga, Bibi Juan Mening.

Amesema hajaridhishwa na utendaji wake kwa kuwa ameshindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na hata hicho kidogo kinachokusanywa hakifikishwi Serikali.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Machi 2, 2020) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga pamoja na wananchi baada ya kufungua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.

Amesema Serikali inataka kila mtumishi wa umma nchini awajibike kwa kufanya kazi kwa bidii na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitowavumilia watumishi ambao ni wezi, wabadhilifu, wavivu na haitosita kuwachukulia hatua.

“Watumishi fanyeni kazi kwa bidii na msitarajie kuundiwa tume pale mnapofanya vibaya, ukiharibu kazi tunakushughulikia hapo hapo na huu ndio msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.”

Waziri Mkuu aliwaeleza watumishi hao kuwa wanatakiwa wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma na pia watambue dhamana kubwa waliyonayo, ambayo ni kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Pia, Waziri Mkuu amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuhakikisha wanakuwa wakali katika usimamizi wa makusanyo ya mapato pamoja na matumizi yake.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa siku 18 kuaznia leo Jumatatu, Machi 2, 2020 kwa watumishi wa halmashauri hiyo wanaoishi jijini Tanga wawe wamehamia katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa wabaki huko huko waliko.

Amesema Serikali inataka watumishi wa umma wawajibike na waishi katika vituo vyao vya kazi. “Nawataka watumishi wote wa wilaya hii wanaoishi jijini Tanga wawe wamehamia hapa ifikapo Machi 20 mwaka huu na wasiohamia waendelee kubaki huko huko.”
 
Ahaa kumbe bado kuna mapato ya serikali hayakusanywi kwa mfumo wa GePG?

Sent using Jamii Forums mobile app
GePG gani kama kule Kahama sijui wapi mgambo eti "alitokomea" na mapato ya mil17

Watu wanakusanya mapato wanatoa na risit ya efd ila anakabidhi muhasibu kienyeji muhasibu anazitafuna

Ubadhirifu ni janga la taifa na wala GePG haiwezi kulifuta
 
Back
Top Bottom