Waziri Mkuu aagiza kaburi la Faru John lifukuliwe

Nilishangaa kuona wale jamaa wakipeleka zile pembe. Hata nilijiuliza hivi wanadhani kelele zingeishia kwenye pembe? Na kama walijua kuna hatua baada ya hapo walijipanga namna gani. Hapo nikajiuliza tena na nikajiaminisha faru john amekufa na kuzikwa ila nikajiuliza tena kama walipiga "dili" huyo waliemzika hapo walimtoa wapi? na ndo mwenye hizo pembe zilizopelekwa. Acha tusubiri
 
Swali nje ya Mada; hivi hamna faru wa dhehebu lingine mfano Juma au Hussein au faru jinsia nyingine kama Anna au Zakia? Maana yule wa mwanzo alieuwawa alikuwa anaitwa GEORGE huyu ni JOHN.
Akiitwa Hussein kuna faida gani na alipoitwa John kumetokea hasara ipi?
kuna mambo muhimu ya kudemand zaidi ya kutaka Mnyama aitwe Juma.
 
Hongera sana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hatua nzuri kufahamu ukweli. Wale waliozikwa kule Ruvu nao wataenda kufukuliwa lini kwa ajili kufanyiwa uchunguzi?wamekufa kwa mazingira tatanishi na kuzikwa katika mazingira tatanishi pia.
[HASHTAG]#Justice[/HASHTAG] For Lema
[HASHTAG]#Justice[/HASHTAG] For Maxence Melo
[HASHTAG]#Bring[/HASHTAG] Back Ben Saanane
 
Zile maiti zilizozikwa kando ya mtu ruvu hazina maana kwao.
Hazihitaji DNA kwani ni za wakimbizi! But for faru aagh! mbona watalimia meno!I. Ni Kama mbuga yote itavurugwa kuyatafuta masalia ya john. Haya nayo no maajabu japo hayawekewi kumbukumbu.
 
Binafsi nampongeza waziri mkuu kwa kuamua kulichunguza kwa makini suala hili kabla ya kuchukua hatua zaid
 
Faru John aliondoka ktk mazingira tatanishi sana toka Crater kwenda Sasakwa(Grumeti Game Reserve)
Kuna habari kuwa wale wawekezaji wa Sasakwa walihitaji Faru katika eneo la Lodge yao;kule Sasakwa kuna Logde inaitwa "FARU FARU LOGDE"(unaweza ku-google)

Hii lodge ni moja kati ya lodge zenye ghalama sana na hufikiwa na wageni mashuhuri na Celebrities toka sehemu mbalimbali za dunia.Usiku mmoja kulala ni $7,600,hapa ndipo Justin Timberlake na mkewe walifanyia fungate,Oprah Winfrey(!?) alikuja na kukaaa siku kadhaa.Celebrities wengi huja kificho na kukaa hapa.

Ili kuendena na jina la "Faru Faru Logde" ilibidi Faru John achukuliwe crater kwa ghalama kubwa na kwenda kuongeza uzao katka eneo hilo,ambalo ni eneo la muwekezaji;kwa hiyo JOHN alitolewa eneo la Crater la Serikali akapelekwa Sasakwa kwa mtu binafsi ili avutie utalii.

Kwanza,aliletwa ktk amzingira mapya,toka kwenye National Park mpaka kwenye Game Reserve.Wale askari wa Grumeti walikuwa na kazi ya kukimbizana na Faru asiende mazingira ya mbali na kuwapa watalii shida ya kumuona.Mazingira Mapya,purukushani na ugeni wa John ktk eneo asilolizoea,vilimletea matatizo na shida ya "home sickness"....Kwamba zile pembe ni zake?Na kwanni hasa alikufa?ngoja waje na majibu ili tuwe katika mazingira sahihi ya kubumbulua "deal" lote la Faru Dume.
 
Maiti ya Faru John imeshaoza Mh. Waziri Mkuu tutapata wapi sample ya kupima DNA?
 
Kwani ile miili kule bagamoyo ilifukuliwa?
Wazir husika nakuomba na ile miili 6 iliyozikwa na wavuv nayo ifukiliwe kama bado.
Mana hatuna aman inawezekana labda kuna ugaid umeingia
Tusiishie tu kwenye kulinda wanyama.
 
Back
Top Bottom