Waziri Mkuu a New Zealand ni Mjamzito

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
_99658100_a7af0efb-02c2-4c4c-908b-c194a95b16ac.jpg

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amefichua kwamba yeye ni mjamzito.

Bi Ardern alisema kwamba yeye na mpenzi wake Clarker Gayford walikuwa wakitarajia mwana wao mwezi Juni ambapo baadaye atachukua likizo ya wiki sita.

''Na tulidhani kwamba mwaka 2017 ni mwaka mkuu'', aliandika katika mtandao wake wa Instagram.

Bi Ardern mwenye umri wa miaka 37 alikuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo nchini New Zealand tangu 1856 akiungwa mkono wakati alipotangaza kuhusu hali yake mpya siku ya Ijumaa.
Waziri mkuu wa New Zealand asema ni mjamzito
 
Huu uzi umeandikwa kwa codes au?? Mbona nashindwa kuuelewa?? Mwanamke kuwa mjamzito ni big news?? Kuna stori gani imefichwa hapa siielewi labda.
 
Mama huyo ni mtata sana nipo huku mtaani kwake. Acheni kabisa .

Ila mambo hayo ni mtambuka hua hata Simba anajikuta tayari imo.

Japo, kwa mwanamke kuwa mjamzito ni kawaida, na ni furaha kwa wahusika wakati mwingine kwa jamii nzima.
 
Hata wanawake na watoto wetu wa kike wanaweza kuwa viongozi, nasi tumebarikiwa kwa kina Makinda, Mongella, Tibaijuka, Migiro, Mghwira, Malecela, Samia etc etc
Safi sana
 
Hakuna shida hapo ww... Kwan sini mwanamke? Tena aged 37!! Kuna shida gani hapo tena ameolewa..
Sioni tatizo hapo..
tizama hata chanzo cha habari ndio utanielewa ...........................ni mwanamke WAZIRI MKUU
 
Kwanza, hiyo ndiyo mimba yake ya kwanza.

Watu hasa Africa tunapaswa kujifunza kuwa mwanamke siyo miaka 12 ameisha pachikwa mimba.

Pili, wanawake na wanaume tusikimbilie kuwatukana wanawake kuwa wana miaka sijui 30 ila hawana mtoto au kuolewa.

Tatu, ni Waziri Mkuu,
Kumbuka hapa New Zealand siyo nchi ya kisportsport kwa hiyo ni hatua kubwa.

Nne, yeye kuwa mjamzito inatoa picha nyingi sana kwa nchi na wazungu hawazai hovyo ivyo kwa hiyo inakuwa ni story fulani yenye mambo mengi.

Reference: waziri wa madini hapo Tanzania, mbona naye kila siku anajadiliwa ni kwa nini kama ni kawaida mwanamke kuwa mjamzito!?

Nitarudi tena.
 
Back
Top Bottom