Waziri Mkulo asema HANA UHAKIKA na wala HAJUI kama ufisadi na rushwa vitaisha tz! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkulo asema HANA UHAKIKA na wala HAJUI kama ufisadi na rushwa vitaisha tz!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Nov 20, 2009.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amesema hajui kama Tanzania itaweza kuondokana na tatizo la rushwa na ufisadi, licha ya juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na tatizo hilo.
  Mkulo alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka unaoikutanisha serikali na wahisani, kutathimini mafanikio, na maeneo ambayo hakukuwa na mafanikio katika bajeti iliyopita.

  “Sijui kama Tanzania itaweza kuondokana na suala la rushwa na ufisadi,” alisema Waziri Mkulo.

  Kauli hiyo ya Mkulo ilitokana na swali la mwandishi wa habari aliyetaka kiongozi huyo afafanue zaidi kuhusu suala la rushwa alilolizungumza wakati wa hotuba yake ya ufunguzi, ambapo aliwahakikishia wahisani kuwa serikali inachukulia suala la rushwa kwa umakini sana.

  Akifafanua suala hilo, Mkulo alisema kuna hisia kwamba serikali haijalivalia njuga suala la rushwa jambo ambalo si kweli.
  Aliongeza kusema kuwa suala la rushwa ni gumu kukabiliana nalo kutokana na kuhusisha watu wawili, yaani mtoaji na mpokeaji.

  “Kupambana na rushwa ni jambo ambalo halichukui mwaka mmoja ukasema umepambana na rushwa, linachukua miaka. Kwa mfano mwaka 2004 tulikuwa na kesi 58 mahakamani na mwaka huu wa 2009 tuna kesi 1,578 za rushwa.
  “Hapo huwezi kusema hatujafanya juhudi… suala la rushwa ni suala gumu na Sijui kama tutaweza kuondoka katika rushwa, lakini tunajitahidi,” alisema Mkulo.

  Mbali na hilo, akijibu swali kama pesa za safari na makongamano zinazotumiwa na viongozi ni za wafadhili, Mkulo alisema fedha hizo si za wafadhili, licha ya kwamba mikutano na makongamano yamekuwa mengi.

  “Kama alivyosema Waziri Mkuu, mikutano na makongamano hayo ni suala la kufikiria na kujaribu kutazama kama kweli yote yana maana, kwa hiyo ni suala la kufikiria,” alisema.

  Akizungumzia mkutano huo wa wiki nzima uliofunguliwa jana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mkulo alisema ni muhimu kwa kuwa serikali na wahisani walikubaliana kusaini misaada ya bajeti.
  Alisema kila mwaka serikali na wahisani wanakutana na kukubaliana vigezo na nchi wahisani wanaahidi kiasi cha pesa kwa ajili ya kuchangia kwenye bajeti.
  Mkulo alisema mkutano huo unatathimini yote yaliyofanikiwa katika kipindi cha mwaka uliopita na kwamba pale ambako serikali imeshindwa kufanikisha, inajieleza kwanini imeshindwa.
  Waziri huyo wa fedha alisema kuwa wamekuwa na mazungumzo katika maeneo mengi na wahisani na wamekubaliana katika maeneo machache, ikiwamo katika eneo la uchumi.
  Akielezea eneo ambalo kwa mwaka huu serikali imekwama katika kutekeleza maendeleo yake kama walivyokubaliana, Mkulo alilitaja eneo la kupunguza umaskini kupitia mkakati wa MKUKUTA.

  Alisema kwenye kupunguza umaskini, kasi haikuwa kubwa kama ambavyo walitarajia hadi kufikia mwaka 2015 kwamba umaskini uwe umepungua kwa asilimia 50 ????????????.

  Alizitaja sababu za kushindwa kupunguza umaskini kuwa ni pamoja na kilimo kuwa cha kusuasua, ubovu wa miundombinu, hususani barabara na mvua ambazo walitegemea zingenyesha, lakini hazikunyesha ???????.

  Aidha, akizungumzia suala zima la bajeti, Mkulo alikiri kulikuwa na upungufu katika miezi ya Julai na Agosti, lakini ilipofika Septemba hali iliweza kurejea vizuri.

  Alisema pia kulikuwa na pengo la sh bilioni 500 katika bajeti na walikubalina na Shirika la Fedha Duniani (IMF) waweze kukopa asilimia 1.5 katika pato la ndani.
  Mkutano huo wa wiki moja, unawakutanisha wahisani, wadau mbalimbali katika masuala ya bajeti pamoja na serikali.
   
 2. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Tunategemea nini? Uwezo mdogo wa Rais unaitwa ni uungwana! Kujisalimisha kwa Rais mikononi mwa Mafisadi kunaitwa ni uvumilivu! Kushindwa kufanya maamuzi kwa rais kunaitwa "mapenzi kwa nchi" na "uchungu kwa watu maskini".

  Kwa mtaji huu, Rushwa haitakwisha Tanzania.
   
 3. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kwa nini hawa watu wanashika nafasi za Uongozi?

  Mtu kama huyu huwezi kumuita kiongozi kwa sababu yupo pale kushibisha tumbo lake.

  Yeye binafsi amefanya nini kuondoa ufisadi katika wizara yake na idara zilizopo chini ya wizara ya fedha?

  From the get go watu kama hawa wana mentality ya kushindwa. It's just pathetic!!

  Inabidi awaachie watu wenye uwezo na kazi na sio kuwa msindikizaji.
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Heri MKULO umenena kweli. Kwani rushwa na ufisadi ni Fupa lilomshinda Fisi.

  Rushwa imeanza toka wakati wa JKN.
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Katika kauli nyingi zinazotolewa na Mawaziri wa awamu hii ina ukweli mwingi tu. Walarushwa ni wao wenyewe; itaishaje? Tofauti na ngonjera za watu kama Makamba.
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  MKULO EDUCATION :

  School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
  Almeda University - USA MBA 2004 2005 MASTERS DEGREE
  National Board of Accountants & Auditors CPA 1982 1982
  S'West London College - London ACCA 1975 1977
  Strathmore College - Nairobi ACCA 1971 1973
  Private Studies A-Level Education 1969 1970 HIGH SCHOOL
  Pugu Secondary School O-Level Education 1965 1968 SECONDARY
  Zombo Middle School Primary Education 1961 1964 PRIMARY
  Rudewa Primary School Primary Education 1956 1960 PRIMARY  Almeda University
  From Wikipedia, the free encyclopedia

  [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Almeda_University[/ame]

  Almeda University is an unaccredited American institution that offers various academic degrees through distance education, including a "Life Experience Degree". Almeda was founded in 1997.[1]

  Legally, Almeda University is a corporation registered on the Caribbean island of Nevis. [3] Almeda claims accreditation by the Council for Distance Education Accreditation, Interfaith Education Ministries (IEM) and the Association for Online Academic Excellence (AOAEX); [4] none of these is recognized by the United States Department of Education or the Council for Higher Education Accreditation.[5] On its website, Almeda states that its claimed sources of accreditation are not recognized by the U.S. Department of Education, with the results that students cannot receive U.S. federal loans or assistance under the GI Bill and Almeda degrees may not be recognized by academia or employers.[4]

  Connecticut:
  According to the Connecticut Department of Higher Education, Almeda was ordered to cease operating in Connecticut in October, 2001. After an investigation in 2002 indicated that Almeda was continuing to advertise its programs in Connecticut, the Department of Higher Education sent Almeda a second cease and desist letter and referred the issue to the Connecticut Attorney General for possible legal action.[6]
  Florida: In 2003 the Florida Department of Education made an agreement with Almeda to cease operating in the state. Although Floridians can still get a degree from the online university, Almeda warns Floridians that its degrees may not be valid for public employment in Florida.[7]


  Texas: Almeda is also on the Texas list of "Fraudulent or Substandard Institutions", making it illegal to use an Almeda degree in Texas in an advertisement; to get a job, promotion, raise, license, or to get admitted to an educational program or to gain many positions in government.[8]
  Other states: Almeda's website also warns Almeda degrees may not be valid for public employment in Illinois, Oregon, New Jersey, North Dakota, Washington and Idaho.[3]

  Commentaries
  Almeda's academic standards have been criticized by a variety of education organizations. According to Bear's Guide to Earning Degrees by Distance Learning, Almeda College and University is a "nonwonderful" [9] web-only university that offers degrees based on an assessment of a candidate's "life experience". Bear notes that Almeda states that it is accredited by the Association for Online Academic Excellence, but that that association is itself unrecognized.[10][11]

  In 2004 the CBS affiliate in Albany, New York, ran a report on Almeda that featured Peter Brancato, who had filled out an application for an associate degree on behalf of his dog, Wally. Part of the "life experience" listed on the application was "Plays with the kids every day ... teaches them to interact better with each other ... Teaches them responsibilities like feeding the dog." Almeda granted Wally an associate's degree in childhood development with a course list including European culture, college algebra, American history, and public speaking.[12] In reply, Almeda claims Brancato perjured himself by creating a false identity using a fabricated name and date of birth. They write, "He completed an application that included a background of the following: Eight-years tutoring pre-K children, curriculum design and development, teaching coping skills, and volunteer coaching."[13]

  In 2005 Wired News included Almeda University in an article about educational accreditation and diploma mills.[14]

  In 2006 a Naples, Florida, police officer was required to pay back a salary increase based on a degree from Almeda.[7] Two Naples police officers were also fired after investigation showed that they bought diplomas from Almeda University.
  [15] On October 28, 2006, both officers were given their jobs back with back pay but received 10-day suspensions and were required to take an ethics course before the end of the year.[16]

  According to Better Business Bureau (BBB) records, the Boise, Idaho address listed for Almeda University is a UPS Store (private mail box). Almeda University offered to provide their physical location to the BBB provided the BBB would not make it public. While the Better Business Bureau provides reports on Almeda University, Almeda is not a paid member of the BBB, however, Almeda does have a satisfactory record of complaint resolution.[17]

  According to the online shopping reliability tracking service, ePublicEye.com, since 2001 customers of Almeda have reported high levels of satisfaction in such categories as "Management Accessibility", "Customer Support", "On-time Delivery" and "Privacy Experience".[18]
   
 7. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
   
 8. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2009
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Tanzania, Tanzania,........nakupenda kwa moyo wote.....

  Ndio maana Lipumba ni muhimu kuwa Rais kwani hatachagua waziri wa fedha mjinga kama huyu ,sasa huyu ndio tutegemee kuwa uchumi wa nchi utakuwa?
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkullo Mkullo Mkullo!

  Nani alikudanganya uwaziri wa fedha, hata wa nchi sukuma liende kama Tanzania, ni sawa na kufukuzia visichana vya form two Jitegemee Secondary?

  Unaona matokeo yake hayo? Unafikiri kazi hii ni rahisi kama kupata degree ya Almeida?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu Radical, gap kubwa miongoni mwa watanzania ni ile ya wanaijali nchi yao na walio bora liende... hiyo ni gap kubwa kuliko ya kipato!!!

  think about it.
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa kama kazi haiwezi si awaachie wanaoweza kumake a difference, kwa nini hajiuzulu kama hawezi?
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kalcha ya kujiuzulu bongo hatuna... hata jitu likifumaniwa ofisini linaona sawa tu!!!

  Thats how difficult dhana ya uwajibikaji ilivyo tanzania
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,801
  Likes Received: 5,090
  Trophy Points: 280
  ..Mkullo ana degree toka chuo feki.

  ..huyu hafai kuongoza wizara nyeti ya Fedha,Uchumi,na Mipango.
   
 14. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Haswaa !! Waziri wa fedha, anayetakiwa kusimamia fedha, anasema hajui kama inawezekana kusimamia fedha...excuse me, but WTF are you still here ???
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkullo is another failure...hivi anaongea nini huyu..if you can't then quit..
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkullo has "foot and mouth disease", the minute he opens his mouth, he puts his foot in it.
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Sasa ukisikia mazingaombwe na Tanzania ndio haya, yaani Waziri mzima wa Jamhuri anatamka maneno kama haya mbele ya public, lakini hakuna demand ya uwajibikaji,

  - Nchi zinazojali sheria, hapo hapo anagetakiwa ku-elaborate with facts and evidence nani ni fisadi na nani ni mla rushwa, na kama anawajua kama kiongozi wa jamhuri amewafanya nini kuhusu kutabngulia kwenye sheria, lakini bongo waandishi wamekenua meno tu huku wamepewa soda za dezo na kuandika nonsense kila siku, sijui lini tutajifunza uwajibikaji hili taifa!

  - Jana Obama amesema kwenye public kwamba wale watu watano wa Guantanamo wanaokwenda kushitakiwa New York, watapata Death Penalty tu, leo magazeti yanadai a-recant maneno yake maana yata-influence mahakama zitakazo amua hiyo kesi, leo ameomba msamaha kwa kuropoka bila facts, tizama huu ndio uwajibikaji.

  - Yaaani bongo liwaziri lizima linaamka na kujiropokea tu hakuna facts wala evidence na waandishi wanafurahi maana eti habari kama hii huuza magazeti mengi kwa sababu na sisi wananchi tunapenda sana this kind of don't care journalism, inasikitisha sana! Ingekuwa nchi yenye kujali sheria leo Mkullo politically angekua kwenye hot water lakini kwa vile no bongo huyu ni hero amesema ukweli huyu, amewapa vidonge vyao. Nonsense!

  Respect.


  FMEs!
   
Loading...