Waziri Mkullo akataa kuipa tena fedha TANESCO kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya IPTL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkullo akataa kuipa tena fedha TANESCO kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya IPTL

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Oct 30, 2011.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Waziri Mkulo amethibitisha kwamba wizara yake haitoi tena fedha kwa ajili ya mafuta ya IPTL, akisisitiza: “Sema kabisa kwamba Waziri wa Fedha kasema wizara yake haihusiki na malipo hayo, hatuwezi kutumia fedha za walipakodi kununua mafuta huku watu wengine wakitumia umeme holela tu, fedha hizo zinatoka wapi!” “Tulitoa fedha kununua mafuta ya IPTL kwa miezi miwili tu, kazi ya hao watu wa umeme ni kuzalisha umeme na kuuza umeme wapate fedha nyingine wanunue mafuta, Serikali haina bajeti hiyo ya kununua mafuta kila mwezi,” alisisitiza Mkulo.

  Ni watu gani hao wanaotumia umeme kiholela??ana maana gani anaposema wanatumia umeme kiholela???Kwani huo umeme wanaoutumia kiholela haulipiwi???Je ni sahihi kwa Waziri kuumiza Wananchi walio wengi au kudeal na hao watumiaji holela ambao inaonesha hawalipii gharama za umeme????Kama wanalipia kwanini Waziri awalaumu wakati ni wateja wa Tanesco?? Hakika kuna maswali mengi kuliko majibu. Inaonesha nyuma ya pazia kuna zaidi ya aliyotamka Waziri. Naomba kutoa hoja.

  Mwananchi: Friday, 28 October 2011 20:01
   
 2. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  IPTL waondoke hatuwataki tena!!.. TOKA HAPA!!
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Akili za watanzania ni kunusu Dowans tu ,inashangaza pale ambapo wanaharakiti wanalilia Dowans wanasahau Iptl ambayo kiualisia ni mbaya kuliko Dowans,nyie wanaharakati acheni siasa za makundi kwa kupitia hoja nyepesi ya Dowans
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Mimi naona katika hili mh mkulo anayo hoja. Kwa nini tanesco inashindwa kununua mafuta yenyewe hata baada ya kuwa subsdized kwa miezi miwili? Ni lazima tanesco wajibu swali hili.
   
 5. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Kwa maana hiyo mgao utazidi makali....

  white house ndio wanatumia umeme ovyo?
   
 6. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  IPTL wanacholipwa ni almost 10 times ya anachotozwa mtumiaji wa mwisho wa umeme. Hii ni matokeo mabaya ya kusaidi mikataba ya kifisadi, hivyo Tanesco hata wakusanye mpaka tone la damu hawawezi kumudu kulipia mafuta ya IPTL. Ukisema wamtoze end users basi sote umeme utakuwa historia bali kwao wao tu
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Iptl ni matokeo ya kazi ya mikono ya boss wake, ironically. Naona kasi ya kukata umeme imekuwa kubwa sku hizi mbili tatu. Sijui ndio effect ya iptl?
   
 8. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  MKULLO kasema kweli si wanafanya biashara sasa kwa nini waendelee kuitegemea serikali ilihali biashara inalipa
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wameshaanza kuchukiana wewnyewe kwa wenyewe kwenye serikali!

  Hii inamaanisha kuwa Mkulo anamwambia Ngeleja ajitafuitie fedha za mafuta mwenyewe, wakati kwenye mipango ya dharula waliyoiwasilisha Bungeni walikubaliana kama serikali.

  Kama wao wanagombana hivyo, mwananchi wa kawaida atahudumiwa na nani? Hivi tukiwakataa 2015 watatuona wabaya?
   
 10. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkulo anayo point, inashangaza sana Tanesco kuendelea kutegemea serikali kujiendesha wakati wanauza umeme!! Kama hawawezi kuwaserious na biashara yao, si waifunge tujue moja? Hata hivyo, matatizo yote ya Tanesco kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na viongozi wenyewe wa serikali, hivyo Tanesco kama shirika linapaswa lielekeze lawama zote kwao.

  Kama saizi wamefikia hatua ya kukataa, basi waiache Tanesco ijiendeshe yenyewe kama yenyewe bila kuingiliwa na wanasiasa tuone kama kweli Engineers ni vilaza kiasi cha kushindwa kuiendesha Tanesco kitu ambacho ni ndoto. Politics ndo zinaiuwa Tanesco siku zote.
   
 11. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu suala la Tanesco, IPTL na Serikali(Mkullo) ni suala Mtambuka. Msisahau kuwa Serikali ndiyo iliyoyaingiza mashirika yetu kwenye mikataba yote feki/kandamizi/yakinyonyaji na ya yakifisadi kama wa IPTL, Richmond,ATCL,KIA, RITES-TRL n.k. Ni kweli, Tanesco ni shirika linalohitaji kujiendesha kwa faida na hata Tanesco yenyewe inajua hivyo. Kinachowafanya Tanesco waende kwa Mkullo ni kwamba Tanesco wanajua kilicholifikisha shirika lao hapo lilipo ni mikataba feki iliyoingiwa kwa Shinikizo la Serikali, kwa manufaa ya wezi wachache/mafisadi.

  Kama unafwatilia kwa makini, Sehemu ambayo serikali ilishiriki katika kuyaingiza mashirika yetu ktk mikataba feki, Serikali haina hiyana kuingia gharama za kuyaendesha mashirika hayo. Tumeshuhudia mara kadhaa Serikali ikilipa Billions of money kama Mishahara kwa wafanyakazi wa Shirika la Reli TRL na ATCL, tunaona Serikali inanunua mafuta IPTL, n.k. Serikali haifanyi haya kwa bahati mbaya, inajua mikataba waliyoingia na wawekezaji katika mashirika hayo isingepelekea mashirika hayo kupata faida, ila walifanya hivyo kwa manufaa ya wachache/mafisadi tu kwa expenses za walipa kodi.

  Binafsi simuelewi Mkullo, kwani wakati anaipa fedha tanesco miezi miwili ya kwanza hakujua kuwa Tanesco ni shirika linalijitegemea??Hajui nini kama Serikali ndiyo inayoingia mikataba na wawekezaji kwa niaba ya Tanesco???Hajui nini kama mkataba wa IPTL ni wakinyonyaji???au hajui maana ya mkataba wakinyonyaji???Kama serikali inatoaga shinikizo katika kuiingia mikataba hiyo, isione ajabu/haya kuingia gharama ya mikataba hiyo feki pale inapoleta hasara kwenye mashirika yetu.

  Serikali ndiyo inayo iua Tanesco, Ndiyo iliyoiua TRL na Ndiyo iliyoiua ATCL chanzo kikuu cha mauaji hayo ni UFISADI kupitia Mikataba ya kibabaishaji. So Mkullo usitafute sifa kwa wananchi kwa kujifanya una uchungu sana na fedha za walipa kodi sasa hivi. Uchungu huo ungeuonyesha enzi hizo za kuingia hiyo Mikataba ya Kifisadi. Mbona huonyeshi uchungu wa kufwatilia fedha zetu za Kagoda, Meremeta, Deep Green, Tangold n.k zilipo????Au hizi sio fedha za walipa kodi???Au wewe sio Waziri mwenye dhamana ya hizi fedha???Au hazikutoka Wizarani kwako???Acha kutafuta cheap popularity, wapeni Tanesco fedha maana hayo ndo mliyoyataka. After all mnafurahia hali hiyo mana na nyie mnatokea hapohapo, unadhani nani hajui hilo?????
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hawa Tanesco na wenzao wa wizara ya Nishati ni watu waliodekezwa na ndiyo maana sasa wanadiriki kutegemea ruzuki kila siku na huku wakijua kwamba wanakusanya fedha za umeme kutoka kwa wateja halafu wanarudi huku kudai fedha za walipa kodi ambao wana vipaumbele vingine vya msingi. Nashauri shirika hili litazamwe upya na ikiwezekana wapigwe chini.
   
 13. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu umesahau kuwa IPTL ndo inayoua band. Kile kiasi unacholipia umeme bado IPTL wanakomba kwenye mkataba na hawana mafuta. Tanesco kuweza kujiendesha ni lazima tukubali kukaa gizani kwa kuvunja mikataba yote ya Umeme wa dharura. Tukifanya hivyo TANESCO WATAWEZA KUANZA UPYA WAKIWA NA MZIGO MDOGO.
  Mkuu hawa akina mkullo wasikudanganye Tanesco ndo chuma ulete ya wakubwa serikalini. Mikataba yote hii ya umeme wa dharura wanamapato yao. Kwani huoni leo hii hamna anayeongelea Zile project kubwa za kumaliza titizo la umeme watu wako bize na majenereta ya dharura tu kila mwaka.

  Nchi ya kitu kidogo bwana!
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Hamna mbaya kukumbuka shuka wakati tayari kumekucha
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Heri mafuta yanunuliwe kwa vyovyote vile maana kuenda kulipa service charges bila kuzalisha umeme ni hasara maradufu.
   
 16. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  tumesahau alieinjinia kuwepo kwa kampuni ya IPTL ni KJ na sakata zima analijua yeye na mwandosya
  wkt huo akiwa waziri wa nishati, mengi yapo wazi wajuzi wa duru za kisiasa na matukio waweke hiyo taarifa hapa
  mnajua kwann KJ mwandosya na Luhanjo hawaachani?????
  nadhani maandamano yanatakiwa kwa ajili ya kushinikiza huu mkataba feki unaonufaisha wachache ufutwe
  na wawajibike waliosababisha ukawepo to mean KJ na wengineo ndio wametufikisha tulipo.
   
Loading...