Waziri Mkuchika; Serikali imeishiwa fedha tangu mwaka jana, Halmashauri zote hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuchika; Serikali imeishiwa fedha tangu mwaka jana, Halmashauri zote hoi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Feb 3, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Ukurusa wa mbele wa gazeti la mwananchi la leo kuna habari hii ya kukatisha tamaa ya serikali kuishiwa na fedha. Gazeti limeandika, Akijiba swali la Mbunge wa Singida Magharibi, Mohamed Misanga, Waziri Mkuchika amekiri kuwa hali ya serikal kifedha ni mbaya ndiyo maana halmashauri zote nchini hazina fedha za kuendesha mambo mabali mbali ya kiutendaji. Waziri akinukuliwa gazetini alisema;
  Kiwango cha fedha ni kidogo na hili liko mikononi mwa waziri mkuu. Akaendelea.
  Tatizo hilo ni kubwa mpaka chama cha Serikali ya mitaa (ALAT) kimeomba kukutana na uongozi wa juu ili kuzungumzia tatizo hilo.
  Aliendelea
  Halmashauri zote nchini zina ukata wa fedha unaotokana na matatizo ya kifedha ambazo kwa muda mrefu hazijapelekwa huko, ………..hata fedha za mwaka jana hazijapatikana na kupelekwa kwenye Halmashauri. Mbaya zaidi, waziri huyo alishindwa kuwaeleza wabunge ni lini fedha hizo zitapelekwa huko.
  My question
  Hivi kama serikali inakiri kuwa haina fedha za maendeleo zaidi mishahara inayolipwa kwa Mbinde mwaka 2012 itawezaje kutufikisha 2015? Kukuru kakara za kuchakachua matokeo ya Urais kumbe hawajui suluhisho la matatizo yetu?
  Kwa kuwa Mwl Nyerere alisema kuwa Serikali inayokula rushwa haiwezi kukusanya kodi, - itaanguka, na
  kwa kuwa tayari hali hii imeshajitokeza tangu 2011, shughuli zote za maendeleo zimesimama na
  Kwa kuwa bado miaka 4 Serikali hii imalize muda wake
  Je, si kwamba kauli ya mwl Nyerere itatima kabla ya mwaka 2015?

  Nawasilisha.
   
 2. obm

  obm Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkulo aslimema wana hela liko wapi wajiuzulu mapema
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Jamani wacha halmashauri ziishiwe fedha ,kwa ufisadi uliotamalaki unaofanywa na maofisa wake,hebu tuambieni ukweli je ni halmashauri ya mji ipi hapa nchini ambyo mahesabu yake ni safi si tumeshuhudia ya Arusha na je si tumemuona waziri Mwanri alipotembelea Kagera na Makete?nchi hii kila sehemu imeoza
   
 4. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  wakati huo huo, Soma makala hii,
  JK AMEKAA NJE YA NCHI ZAIDI YA MIAKA 2, SIKU 966 NA TRIPU 322.

  Wakuu baada ya kufuatilia kwa karibu safari za Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi, nikatafakari kuhusu muda anaotumia kuitumikia nchi na gharama zake anazotumia ktk safari hizo. Muda

  Rais amesafiri nje ya nchi mara 322. Hilo halijadiliki – Liko wazi hapa JF na magazetini. Na halijawahi kukanushwa na mtu yeyote, ikiwepo ikulu yenyewe.
  Safaru nyingi za Rais anatumia kuanzia siku 4, 5 , 7 hadi siku 14 na kuendelea. Safari ya mwisho ya Davos – wiki iliyopita alitumia wiki moja.
  kwa kuwa safari zake nyingi ni nje ya Afrika Masharika – ambayo hutumia siku moja kwa kwenda na siku moja kurudi ni sawa na kusema anatumia Jumla ni siku 2 njiani kwa tripu mmoja tu.
  Kwa hiyo tukikadiria kuwa Rais ktk safari zake amefanya kazi kwa siku 2 tu. Ukijumlisha siku 2 ya kwenda na kurudi. Jumla ni siku 4 kwa wastani - kwa safari mmoja ya majuu.

  GHARAMA
  Kwakuwa sote tunakubaliana kuwa Rais amesafiri mara 322, tuzidishe hiyo idadi ya tripu/safari ( 322) kwa wastani wa hizo siku 4 kwa kila tripu/safari. Utapata jumla ya siku 1288. Hizi siku 1288 ukiZIgawa kwa siku 365/366 ( siku za mwaka mmoja) utapata miaka 3.5 (yaani mika 3 na miezi 6) Rais amekaa nje ya mipaka ya Tanzania.
  Kwa kuwa Rais Jk aliingia madarakani mwaka 2005 na hadi sasa 2012 amekaa madarakani kwa miaka 6. Kwa hiyo, Rais amekaa nje ya nchi nusu ya muda wake wote aliokaa ktk nafasi urais( 3.5 yrs out of 6 years)
  Je, Rais hajavunja rekodi ya kuingizwa ktk G. book of rekodi ya dunia? Yaani Rais aliyekaa nje ya nchi yake kwa muda mrefu kuliko marais wote wa dunia? Rais gani amemezidi Rais wetu?
  NB Rais wa Marekani ambao ni wafadhili wetu hata kwenye bajeti kuu aliyesafiri sana nje ya nchi zaidi tripu 70 (kama 74?) alipigiwa kelele. Wasaidiwa - TZ wanafanya tripu 322?
  Je, tumepata jibu la kwanini Rais mara nyingi husaini nyaraka feki kwa sababu ya ukosefu wa Muda wa kuzisoma?


  GHARAMA
  Safari ya mwisho ( safari ya 322) ya Davos iliigharimu Serikali Tsh mil 300. Nikiamu kuchukua theluthi mbili ya gharama hizo - yaani mil 200, kisha nikazidisha kwa idadi ya tripu 322. Jumla yake ni 64,400,000,000. Mabilioni haya ni mengi sana. Ukizigawa mil 50 ambazo ndio gharama ya kujenga zahanati mmoja kwa wastani, utapata jumla ya Zahanati 1288. Zahanati hizi ni sawa na idadi ya siku alizokaa nje ya nchi Rais wetu(refer red above).
  Pili,Kiasi hiki hizi zingetosha kuweka Zahanati kwenye zaidi ya 50% ya kila kata nchi nzima. Nchi yetu ina kata 2000 na kidogo. Ikumbukwe kuwa Tz wanawake wajawazito kati 24 hadi 36 kwa siku wanakufa kwa sababu kadhaa ikiwepo kutokuwepo kwa zahanati au ziko mbali.

  NB Hata ukisema Rais amefanya kazi nje ya nchi kwa siku moja tu( kitu ambacho binafsi siamini na inapingana na uzoefu halisi wa JK), jumlisha na siku 2 za kwenda na kurudi, unapata jumla ya siku 3 kwa tripu mmoja ya nje. Ukizidisha kwa tripu za nje 322 utapata siku 966 ambazo ukizigawa kwa siku 365/366 utapata 2. 5 (yaani miaka 2 na nusu.)

  Maswali ya ziada.

  Watetezi wa safari hizi za JK watueleze faida ya safari hizo ukilinganisha na gharama tulizoingia. Je, hizo neti za Gorge Bush zinaendana na Gharama tuliyoingia?
  Ikiwa Rais yuko nje ya nchi kwa safari mbali mbali kwa nusu ya muda wake wa kukaa ikulu, nani anakaa ikulu na kutafakari kuhusu utatuzi wa matatizo yetu?
  Je, Rais kwanini asiwatume watu wengine ( PM, Makamo, nk kufanya baadhi ya safari nje ya nchi kwa niaba yake?
  Je, Rais lazima aende na delegation kubwa ambayo inaongeza gharama za safari zake?
  Je, tutakwenda kwa mwendo huu mpaka 2015 kwa amani kweli?
  NB; Ikumbukwe safari hizi zinahusisha kwenda kutembelea wanamuziki maarufu wa USA - Boys 2 men na kubembea majuu.

  Your ideas please!
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Kwahyo wanakubaliana na hoja ya mh zitto aliyoitoa mwaka jana kwamba serikali imefilisika?
   
 6. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni kweli-serikali kwa sasa haina hela-hata kama baadhi ya viongozi wanakataa,ila walioserikalini wanaonaukata unavyoharibu utaratibu wa kazi
   
 7. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa ufupi ni kwamba wamekubaliana na hoja ya Zitto. Kwa upande mwingine Mkulo alikuwa anapiga propaganda. Waziri wa fedha anapodanganya ni hatari zaidi.
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Serikali Chali
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  unajua kwa sababu hii mijitu imeamua kukalia viti kwa lazima na sisi tumeshindwa kuitoa ni bora TUPOTEZEE TUUUU!
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  huku TRA wanatudanganya kwamba wanavuka malengo ya ukusanayaji kodi. unbelievable.
   
 11. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu watasema yote, kama mchawi aliyenyweshwa dawa ili atangaze siri zake zote.
   
 12. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,462
  Likes Received: 789
  Trophy Points: 280
  Hakuna la ajabu,kwanza serikali inategemea ruzuku katika bajeti yake kwa zaidi ya 60% kutoka kwa mataifa wahisani hao wahisani wana matatizo kwao,vile vile serikali imeshindwa kutekeleza masharti yao ili tupewe ruzuku/misaada na hata mikopo.Pili hiyo 40% yawezekana hakuna usimamizi mzuri na uwiano wa kulipa kodi.Tatu matumizi mabaya ya hiyo pesa kidogo iliopatikana.Nne inatakiwa wakati huo huo kulipa madeni ya kweli na yasioyakweli kwa pesa hiyo hiyo.La msingi yahitajika serikali kuongeza uwigo wa kutafuta mapato zaidi kutokana na raslimali tulizonazo.
   
Loading...