Waziri Mkenda: Tunaendelea na zoezi la kumwaga sumu kuua nzige ambao sasa wameelekea Monduli pia Simanjiro!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,830
141,748
Waziri wa Kilimo Prof Mkenda amesema kesho zoezi la kumwaga sumu ya kuua nzige litaendelea baada ya rubani aliyetelekeza ndege pale Kilimanjaro kurejea.

Mkenda amesema kuna kundi la nzige wadogo wameelekea Monduli hivyo wanawafuatilia ili wawatekeze.

Pia Simanjiro zoezi halikukamilika kutokana na mazingira ya huko ambayo yana vichaka na miiba hivyo kuna nzige ambao hawakufikiwa na timu ya wataalamu imetumwa kuwateketeza kwa kutumia ndege ya fao.

Katika hatua nyingine waziri Mkenda amemlaumu CEO wa oganaizesheni ya kupambana na nzige Afrika mashariki kwa kutotoa ushirikiano na hata kutopokea simu zake huku akijua wazi sehemu ya mshahara wake inatokana na kodi za watanzania.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Duuuu nimeshituka eti yule rubani aliyetelekeza ndege pale Kilimanjaro kurejea,, kama aliweza kutelekeza ndege atashindwaje kuzidisha maji kwenye dawa au kuweka asali ili kwenye maji yawe matamu kwa Nzige
 
nimemkuta kwenye maua yangu
20210228_093400.jpg
 
..walitakiwa watafute ndege mahali pengine.

..ni aibu nchi ina ma-dreamliner kibao halafu ndege za kuzuia maafa ya wadudu waharibifu hatuna.
Ndege zilikuwepo ila ziliuzwa hapo Kilimanjaro kwa wanaojiita ' mabilionea" kwa sh 500,000/= kila ndege!
 
Back
Top Bottom