Waziri Mkenda: Hii sio Wizara ya Elimu tu, bali Elimu Sayansi na Teknolojia kwa mapana yake

Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amewataka Wafanyakazi wote kufanya kazi kwa ujasiri bila Uoga, Kwa utii Uaminifu na Uadilifu, Wasifanye kazi kwa nidhamu ya Uoga. Ameyasema hayo leo 10 Jan 2022 Jijini dodoma alipofika Ofisini kwake baada ya kuapishwa ma Rais Samia.

"Sisi ni Viongozi, tunawajibu na tunawajibika Wizara ikiyumba anayelaumiwa ni mmoja. Lakini nataka tusaidiane tusiyumbe. Tunahitaji sana kujibu Kiu ya Watanzania.

Hii sio wizara ya Elimu tuu bali ni Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. Sio Teknolojia ya habari tu bali kwa mapana yake. Hivyo tuna kazi kubwa." amesema Waziri Prof. Adolf Mkenda.

Prof. Adolf Mkenda ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo, amechukua nafasi ya Waziri Ndalichako aliyehamishwa Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Naye Katibu Mkuu Profesa Sedoyeka amesema kipaumbele chake ni matumizi ya teknolojia katika Elimu ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na kuwataka watumishi hao kushirikiana nae katika kuhakikisha sekta ya elimu, sayansi na teknolojia inaleta matokeo chanya katika uchumi wa nchi.
View attachment 2076107
View attachment 2076129
We need more of these kind of people we are lacking in a minute.

Umepewa nafasi sasa piga kazi boresha elimu ya vijana imeyumba sana.
 
Back
Top Bottom