Waziri Mkenda: Hii sio Wizara ya Elimu tu, bali Elimu Sayansi na Teknolojia kwa mapana yake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amewataka Wafanyakazi wote kufanya kazi kwa ujasiri bila Uoga, Kwa utii Uaminifu na Uadilifu, Wasifanye kazi kwa nidhamu ya Uoga. Ameyasema hayo leo 10 Jan 2022 Jijini dodoma alipofika Ofisini kwake baada ya kuapishwa ma Rais Samia.

"Sisi ni Viongozi, tunawajibu na tunawajibika Wizara ikiyumba anayelaumiwa ni mmoja. Lakini nataka tusaidiane tusiyumbe. Tunahitaji sana kujibu Kiu ya Watanzania.

Hii sio wizara ya Elimu tuu bali ni Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. Sio Teknolojia ya habari tu bali kwa mapana yake. Hivyo tuna kazi kubwa." amesema Waziri Prof. Adolf Mkenda.

Prof. Adolf Mkenda ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo, amechukua nafasi ya Waziri Ndalichako aliyehamishwa Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Naye Katibu Mkuu Profesa Sedoyeka amesema kipaumbele chake ni matumizi ya teknolojia katika Elimu ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na kuwataka watumishi hao kushirikiana nae katika kuhakikisha sekta ya elimu, sayansi na teknolojia inaleta matokeo chanya katika uchumi wa nchi.

 
Naona elimu ikifa kwa speed ya ajabu. Hakuna hata mmoja kati yao anayefahamu matatizo ya elimu katika taifa hili.
 
Bora Da Joy kaenda kufuatilia mikataba ya vibarua huko kwenye viwanda vya wachina Buguruni
 
Asije tu Akawa kama Prof Maghembe Alivyotuvurugia Elimu.. Hawa maprofesa wetu siwaamini kabisa.
 
Hii wizara imepata watendaji wazuri sana. Mstituangushe na msimuangushe mheshimiwa Rais. Prof. Mkenda tunakujua na tuna imani na wewe. Ni miongoni mwa watu walinyooka wasiokuwa na chembe za kona kona. Pamoja na hayo yote, tunamshukuru sana Dr. Akwilapo hakika alikuwa mtendaji mzuri sana na bado utendaji wake huo unahitajika kwa Taifa hili hivyo mamlaka ya uteuzi tafadhali huyu mtu bado ni hazina kubwa kwa Taifa, tusimuache. Aidha Mheshimiwa Ndalichako nikuombe tu jitahidi sana hiyo wizara uliyopewa ukawe msikivu wa kupokea mawazo ya wataalamu na siyo kupiga rungu na kutumia ubabe. Sina ugomvi na wewe mama yangu lakini ni vizuri nikasema haya kwa maslahi mapama ya Taifa. Asanteni nawasilisha wana JF.
 
Binafsi namkubali Proff Mkenda kwani hutenda kile anacho amini ni sahihi kwa taaluma yake kitu ambacho ni muhimu sana kwa wizara nyeti ambazo hazihitaji blaa blaa
 
Story nyingi zinapoteza Njia, Tamtam ilimponza akamzuia Kaguta M7
mwambieni apige kazi majisifu kwa mangi sio jadi watamtafsiri vingine
mm naona kaponea tundu la sindano kwa Mama maamuzi ya kiProff .......
 
Hawezi kusema Sayansi na Teknolojia nchi ambayo Mwl wa chuo kikuu hawezi kutumia Computer!

Elimu yetu inahitaji bajeti kubwa kuifumua, waingie watu walio recent! Hawa ma Prof wa miaka ya 90 wanatakiwa wawape vijana nguvu ya kutoa mawazo yaliyo recent.

Inasikitisha sana graduate kuomba kutumiwa CV kwa email! Iko wazi, hata tu smartphones vijana wanaanza kutumia chuo kikuu.

Elimu yetu ni mbovu, graduates wanamaliza na GPA kubwa ila hawako competent, hata kuandika tu ni tatizo.

Inasikitisha.
 
Back
Top Bottom