Waziri Mhagama pambana na malimbikizo na haki za wastaafu usije kosa baraka hapo Utumishi

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,260
7,391
Katika vitu vinaumiza ni mtu kudai malimbikizo yake ya kazi aliyoitolea jasho halafu Fomu zinajazwa hapo wizarani unazikuta zinazagaa mpaka zinapigwa mateke kwa kukosa utaratibu mzuri

Ukiingia chumba cha Approvers ni aibu mafomu yametupwa kila mahali na kupelekea kupoteza haki za watu

Kuna watu walistaafu wakiwa hawajapata malimbikizo yao ikiwa ni kupanda cheo kwa walio wengi! mtu anapewa barua wiki za kustaafu anaondoka hajapanda cheo

Anajazishwa fomu zinatupwa tu hapo utumishi hii ni laana kwa waliowalea mpaka mmefikia kupata na ajira hizo

Waziri Mhagama watu wana imani na wewe hasa wakichukulia ni mwanamke unaweza kuwa na roho ya huruma na kujali

Dr Ndumbaro anafanya kazi vizuri ila awe mkali sana.

Kuna mdada mmoja hapo anaitwa ADERA ana roho mbaya sijawah ona anajibu mbovu wafanyakazi wakija kudai haki zao.
 
wanaokaimu nafasi mbalimbali mmejitahid mmeanza mfumo mpya mtu analipwa ila kuna inventive zingine mfano kwa nini mumnyime hela ya nyumba kwa anayekaimu nafas ambayo aliyekuwepo hatarudi tena?
 
Back
Top Bottom