Waziri Mhagama, Mgawanyo wa watumishi Uzingatie uwiano

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,122
7,705
Waziri wa Umishi wa umma Jenista Mhagama amesama kuwa wameweka utaratibu utakao wezesha mgawanyo wa rasilimali watu ktk maeneo yote ya nchi hii na sio kama ilivyo hivi sasa, mfano shule ya Wilaya ya Muleba vijijini ina mwalimu mmoja anaye fundisha zaidi ya masomo 11 lkn wakati huo huo kuna shule nyingine ina walimu 10 wote wanafindisha somo moja ktk shule moja.

Naunga mkono hoja kama kweli hatua zitachikuliwa, lkn lazima ifahamike kuwa tatizo hili halijatokea kwa bahati mbaya la hasha! bali ni baadhi ya wakubwa/viongozi kwa kujuana wanataka watu wao wakae mijini. ukifanya utafiti asilimia kuwa ya watumishi walio pembezoni ni wale wasio julikana au hawana mtu wa kuwasemea. Na ukichunguza watumishi wote ktk idara mbalimbali ambao wapo mijini asilimia kubwa wamebenwa, wana watu wao juu, huwezi kukuta mtoto wa mlala hoi anakaa mjini. kuna tatizo kubwa kwenye eneo hili, kuna rushwa ya fedha na ngono na kujuana.

Kila idara ya Serikali inapaswa ifanye reshafle ya watumishi wa umma, kuna baadhi ya watumishi wa umma ni unttachable, yaani huwezi kuwahamisha na ujiharibu tu utakoma na wapo ambao wamepigwa pini hawawezi kuwapata uhamisho hata kama wanasababu za msingi, mifano ya uonevu huo ipo tele. no hatari kubwa kwa ustawi wa Taifa letu.

Kwa hili hongera Waziri Mhagama kamwe usimwangalie mtu machoni, Taifa hili ni la watanzania wote, wanyonge n.k, Futa hiyo kasumba eti bila kujuana jambo lako haliwezi kwenda.
 
Back
Top Bottom