Waziri Mhagama kutengua kitendawili cha Bodi kwa wataalam wa Rasilimali watu na watawala Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wataalamu wa Rasilimali watu na maafisa utawala hapa nchini wameiomba serikali kuangania namna ya kuruhusu vyama vyao kuunda bodi yao itakayokuwa na uwezo wa kusimamia utendaji kazi na kuleta ufanisi katika utawala bora.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano mkuu wa kimataifa ulioandaliwa na Taasisi ya wataalamu wa utawala Tanzania APAT na kuwakutanisha wataalamu wa rasilimali watu na watawala ,unaofanyika kwa siku tatu jijini Arusha.

Katibu mkuu wa APAT ,Christopher Kabalika alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili namna ya kuunganisha vyama vya wataalamu wa Rasilimali watu na watawala ili kupata chombo kimoja chenye nguvu kitakachowasimamia na kutetea maslahi yao.

Alisema kuwa mkutano huo ambao utafungwa ijumaa Mei 2O mwaka huu na waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora,Jenista Mhagama ,pia utajadili kuundwa kwa bodi itakayoshughulikia masuala ya maafisa tawala na rasilimali watu ili kushirikiana na serikali katika kulinda maslahi yao na kuajiri watumishi wanaostahili.

"Tukipata bodi tutakuwa na chombo imara chenye mamlaka ya kusimamia, kutetea, kushauri na kushirikiana na serikali katika kupata watumishi waliothibitishwa na bodi tofauti na ilivyo kwa sasa"alisema

Naye afisa utumishi manispaa ya Temeke ,Bihaga Yogwa alisema mkutano huo utasaidia sana katika mustakabali wa kuanzisha bodi itakayokuwa ikisimamia utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza tija katika utendaji kazi Kwa taasisi za serikali na zisizo za serikali.

"Changamoto tunazokumbana nazo kwa sasa ni kutokuwa na chombo imara kinachosimamia mambo yetu ,hivyo ujio wa waziri naimani maombi yetu ya kutaka kuunganisha vyama vyetu nankuwa na chombo kimoja yatafanyiwa kazi "alisema

Kwa upande wake mhadhili wa chuo kikuu cha Nzumbe,Venance Shilingi alisema manufaa ya kuwa na bodi kutasaidia kusimamia maafisa utumishi na wataalamu wa rasilimali wenye maadili na uwezo .

"Kazi ya uafisa utumishi na rasilimali watu kwa sasa imekuwa kama dampo kila mtu anaambiwa akafanye kazi ya kuajiri na kufukuza, tunataka bodi ili ituletee watu wanaostahili wenye sifa stahiki"alisema.

Alisema vyama hivyo vikiungana na kuwa kitu kimoja kutajenga heshima na misingi ya utumishi bora katika sekta hiyo tofauti na hali ilivyo kwa sasa ambapo afisa utumishi anakazi moja ya kuajiri na kufukuza bila kuzingatia misingi ya utumishi bora.

20220518_122809.jpg
 
Back
Top Bottom