Waziri Mh Lukuvi, Kamata kamata ya Wakulima ktk Shamba namba 7 ktk kijiji cha Mambegwa Kilosa inaumiza wakulima

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Ndugu wana bodi
Kumekuwa na kamata kamata ya wakulima wanao lima shamba namba 7 ambalo lipo ktk kijiji cha Mambegwa wilaya y Kilosa.
Inasemekana kuwa shamba namba saba amepewa muwekezaji mwaka 2015,na amepewa karibia ekari 1300.
Cha kushangaza ni kuwa, wakulima wao wanasema waligawiwa mashamba hayo yakiwa ni mapori mwaka 2009, na kila mkulima alipewa ekari tano na serikali ya kijiji Mambegwa.
Wakulima waligawiwa mshamba hayo baada ya mwekezaji wa zamani aliyekuwa akitengeneza pombe aina ya Kibuku kuyatelekeza mashamba hayo.
Baada ya wakulima kufyeka mapori na kuanza kulima mpunga takribani miaka 20 sasa, ameibuka mwekezaji mwingine na kuanza kutumia mgambo kuwa kamata wakulima na kuweka mawe ya mipaka kwa kizingizio kuwa ni WAVAMIZI.Na hii imetokea baada ya kiwanda cha uzalishaji sukari kuanza kazi.Lengo kuu la mwekezaji wa sasa ni kutaka kulima miwa.
Sasa wakulima wanajiuliza maswali haya
1.Je uongozi wa wilaya ya kilosa wakati inamgawia shamba muwekezaji hawakuwa na mawasiliano na serikali ya kijiji cha mambegwa?
2. Ni kwanini mwekezaji anakimbilia kuwakamata wakulima ambao walifyeka pori na huu ni mwaka wa ishirini sasa wakiwa ni wamiliki halali wa ekari tano kwa kila mkulima walizopewa na kijiji?
Wakulima kwa ujumla wao,wanaomba Waziri wa Ardhi kulitizama swala hili kwa jicho la tatu na haki iende kutendeka juu yao.
 
Back
Top Bottom