Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma: Lugha ya malkia Elizabeth, mhhhhh!

Jamani tusimsakame sana huyu Dada kuhusu lugha ya Kiingereza, ilo ni tatizo la Taifa, mfano kidogo tu hii thread tuigeuze kuwa ya Kingereza tuone kama kuna mtu atabakia humu, tutabaki wachache

Ndo maana tukaamua kuongea kwa kiswahili sababu tunajua hilo kwetu ni tatizo.
Yeye alijifanya mashauzi kutaka kusoma kwa kiingereza (sio kuongea), matokeo yake ndo yakatokea hayo yaliyotokea.
Kulikuwa na ulazima gani wa kutumia lugha ile. Si angewaambia tu waliomwandikia, wamwandikie kibongo?
 
Lugha ni tatizo la kitaifa huko Tanzania. Tuulize sisi waalimu tutakwambia.

Hata Viongozi wenu woooote hakuna hata mmoja anayeweza kutoa hotba kwa lugha ya kimombo bila kushika karatasi na kusoma kama risala..

Angalia hotba za JK Nyerere kama alikuwa anashika karatasi na kusoma.??

Wewe ndugu yangu umenena! achilia mbali hicho kidhungu si lugha yetu hata kiswahili sasa hivi viongozi wetu lazima wasome mwanzo mwisho! huwa siwaelewi wanapokomalia makaratasi kusoma hata paragraph 2-3 za shukrani kwa kiswahili eti lazima wasome! Mwl. Nyerere was exellent kwenye speech, iwe ya Kizanaki, Kiswahili, Kiingereza alipiga bila kusoma! Tatizo viongozi wengi wa sasa kwanza wanaandikiwa, halafu hawana muda wa kupitia na kusoma na pengine hata wanachokizungumzia hawakijuwi!
 
Acha umbea na majungu..onyesha au leta evidence wapi mama amekosea katika hotuba yake ikiwa wewe ni mkweli....

Unakuja na perception yako na mke wako ukiwa umejificha kwenye chuki zako ...leta evidence au audio sisi tutaamua ikiwa amekosea au la?

Kwa sasa unastahili kuwekwa kwenye kundi la wazushi, wongo, wenye chuki binafsi..

Nadhani ingekuwa busara kukaa kimya kuliko kuchangia usichokijua, eti uletewe evidence!? Kama hukumsikiliza tulia. Tuliomsikiliza ndio tunajua nini kilichotokea. Na hii si mara yake ya kwanza, siku moja nilimsikiliza kwenye TV nilisikitika sana. Ile halaiki ilikuwa ni ya Watz, maadhimisho ya Watumishi wa Serikali na si wa kutoka International organizations - kwanini kiswahili? Huko Bungeni wanatuambia Kiswahili ndio lugha ya taifa, anahutubia Watz wenzie kiingereza cha nini hata kama alikuwa anakijua kuliko malkia mwenyewe? Kama wageni ni wengi aongee Kiswahili na mkalimani awepo. Maana hotuba ikikosa mvuto hata ujumbe haufiki vizuri kwa walengwa. Usimtetee!
 
Wewe ndugu yangu umenena! achilia mbali hicho kidhungu si lugha yetu hata kiswahili sasa hivi viongozi wetu lazima wasome mwanzo mwisho! huwa siwaelewi wanapokomalia makaratasi kusoma hata paragraph 2-3 za shukrani kwa kiswahili eti lazima wasome! Mwl. Nyerere was exellent kwenye speech, iwe ya Kizanaki, Kiswahili, Kiingereza alipiga bila kusoma! Tatizo viongozi wengi wa sasa kwanza wanaandikiwa, halafu hawana muda wa kupitia na kusoma na pengine hata wanachokizungumzia hawakijuwi!

Hata jana wakati anatoa majumuisho ya wizara yake kule bungeni, alisoma mlolongo wa shukrani, spika akamwambia hiyo hawana shida nayo na haina umuhimu wowote.
 
Sielewi ni kigezo gani kilitumika kumpatia huyu bibie ulaji. Kwa wale waliomwona jana nadhani watakubaliana na mimi huyu mama suala zima la uwasilishaji taarifa ni sifuri.
Alijawa na jazba kubwa huku muda mwingi akidai wananchi wawapuuze wapinzani bila kutoa sababu za msingi. Pole sana bibie maushungi.
 
Back
Top Bottom