Waziri Membe aitabiria ushindi CHADEMA uchaguzi mkuu ujao

Bora awe mpole maana asira zitamuangusha kabisa na ndoto zake za urais zitayeyuka
 
Kwanini asimwamshe aliyelala NAPE NNAUYE? aanze kufikiria angalau agombee Ubunge? sababu Ujumbe wa CC hata kuwa na Nguvu ya kuwakemea Chama cha Madereva wa Usafiri wa Mabasi au kukemea kiwanda cha Ngozi kuhamishwa toka Ruvuma kwenda Morogoro.
Ni kweli kamanda.....
 
Afadhali yeye amesoma alama za nyakati,hawa wanaonajisi demokrasia eg. wassira wajiandae kukumbwa na kimbunga cha mabadiliko na magamba mengine yote,hata huyu membe kama ameongea kinafik hatapona.
 
Mh Membe kafunguka kasoma alama za nyakati hata yeye kachoshwa na hali iliyopo wapo lkn hawajui litakalo tokea 2015 bora asiharibu upande wa pili wapate kwa kuendelea na siasa kamsaidia hata nape afunguke mtazamo tu.
 
Hata madiwani wengi tu wa ccm wanakiri wazi,CHADEMA ni chama makini,chenye watu wasiokuwa kwenye matabaka.Jambo la msingi ni kuendelea kujenga msingi wa namna ya kuendesha nchi.Wanaopinga mabadiliko,iko siku mabadiliko yatawabadisha wao.
 
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe amekitabiria ushindi chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu unaokuja.Waziri Membe amesema chama cha CDM kimetokea kupendwa na wananchi katika kila kona ya nchi na hata operesheni yao ya kusini imekitikisa chama tawala.
Mungu wa mbingu na nchi yaweke muhuri wa moto maneno ya mtu huyu na yawe kama alivyotamka, amen.
Na iwe hivyo Amen
 
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe amekitabiria ushindi chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu unaokuja.Waziri Membe amesema chama cha CDM kimetokea kupendwa na wananchi katika kila kona ya nchi na hata operesheni yao ya kusini imekitikisa chama tawala.
Waziri Membe aliyasema hayo katika chakula cha mchana alichowaandalia viongozi wa CDM nyumbani kwake waliokuwa katika jimbo lake la Mtama.Viongozi hao ni mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema,kamanda James Millya na viongozi wakuu waandamizi.
Waziri Membe aliwaambia viongozi hao ameishi nchi mbalimbali duniani zenye demokrasia ya hali ya juu hivyo hatashangazwa hata kidogo CDM kuingia Ikulu.
Kuhusu kesi iliyotengua ubunge Lema waziri Membe amedai kushtushwa na kusema kwa vile amekata rufaa anaamini mahakama ya rufaa itamrejeshea ubunge wake.

Source:Mtanzania Jumapili.

Updates......
Katika taarifa ya habari ITV saa mbili usiku waziri Membe ameonyeshwa akiwakaribisha viongozi wa CDM nyumbani kwake kijijini Jimboni Mtama na kukaririwa akiwashutumu wabunge wanaolalamika kuvamiwa na CDM majimboni mwao katika vuguvugu la M4C.Membe amesema wabunge hao hawajui ni nini maana ya siasa ya vyama vingi.

Kudos Membe.....Thats what we want to hear.Hawa ndio mawaziri wenye hekima na sio watu kama kina Wasira.
 
Kwani angefanyaje jamani? Kuzuia M4C ni sawa na kukinga maji ya mto Ruaha kwa kuweka udongo kwa kutumia jembe la mkono. Membe ameshaliona hilo na bora aiache tuu asije akajikuta anapunguza siku zake za kuishi kwa presha.
 
anakaribishwa kwa chama kubwa lakini lazima kwanza amwagiwe maji na kubatizwa kwa ubatizo wa moto ili gamba limtoke
 
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe amekitabiria ushindi chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu unaokuja.

Waziri Membe amesema chama cha CDM kimetokea kupendwa na wananchi katika kila kona ya nchi na hata operesheni yao ya kusini imekitikisa chama tawala.

Waziri Membe aliyasema hayo katika chakula cha mchana alichowaandalia viongozi wa CDM nyumbani kwake waliokuwa katika jimbo lake la Mtama.

Viongozi hao ni mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema,kamanda James Millya na viongozi wakuu waandamizi.


Waziri Membe aliwaambia viongozi hao ameishi nchi mbalimbali duniani zenye demokrasia ya hali ya juu hivyo hatashangazwa hata kidogo CDM kuingia Ikulu.

Kuhusu kesi iliyotengua ubunge Lema waziri Membe amedai kushtushwa na kusema kwa vile amekata rufaa anaamini mahakama ya rufaa itamrejeshea ubunge wake.


Source:
Mtanzania Jumapili.

Updates......
Katika taarifa ya habari ITV saa mbili usiku waziri Membe ameonyeshwa akiwakaribisha viongozi wa CDM nyumbani kwake kijijini Jimboni Mtama na kukaririwa akiwashutumu wabunge wanaolalamika kuvamiwa na CDM majimboni mwao katika vuguvugu la M4C.

Membe amesema wabunge hao hawajui ni nini maana ya siasa ya vyama vingi.

Membe haishi Kenya anaishi Tanzania na Dar zaidi.Membe ni mtu tena mwana usalama maarufu na yeye anajua namna ya kupata habari .Membe anaujua ukweli na ameamua kuwa katikati maana lolote linaweza kutokea so hawezi kuendeleza u wassiara wa kijinga .Membe kazinduka ndiyo ukweli huu .
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom