Waziri Membe aitabiria ushindi CHADEMA uchaguzi mkuu ujao

siamini hili
yaani watu waliokuja kukunyanganya tonge mdomoni uwakirimu pasipo shuruba?
labda kama atakuwa mzalendo aliepitiliza ungwana
 
hata ccm wapo wanaipenda CDM, wengine wako huko kwa sababu ya vyeo walivyonavyo, mtu kama Membe angelikuwa hana cheo/uwaziri angekuwa amevua gamba na kuvaa gwanda, huyu ni baadhi wa wachache ndani ya CCM angalau hawanuki ufisadi wa kutisha, kama kuna mtu ana ushahidi wa ufasadi wa waziri huyu aweke hadharani.

Well said mkuu
 
Mnafiki, mzabizabina, nyoka wa mdimu......!


Umekosea sana Headteacher. Membe ni Afisa wa Serikali. Katika nchi yenye demokrasia makini afisa wa serikali anao wajibu wa kuweka pembeni ushabiki wake wa ki-itikadi, kichama, na kuiangalia nchi katika bigger picture ya vyama vyote na kuwa objective katika mitizamo. so Membe ametaka umma wa watanzania kujua kuwa anao uwezo wa kutazama outside the box. He is a good boy kwa maana hiyo. Nchi itajengwa na Wanachadema, WanaCCM, WanaCUF na wengine wenye mitizamo ya kuiangalia nchi kwa namna hiyo. objectively. Nikuambie sasa: ni objectivity ya watu katika serikali iliyomuondoa Nixon kule Marekani kipindi fulani na kuondoa aibu katika nchi. Nchi inajengwa kwa ukweli na haki miongoni mwa watendaji wa weserikali, siyo kwa uongo na ushabiki. Way to go Membe! We are moving in the right direction.
 
Mungu wa mbingu na nchi yaweke muhuri wa moto maneno ya mtu huyu na yawe kama alivyotamka, amen.
 
Membe ameongea ukweli na siasi si uadui yeye tunamkaribisha maana upepo wa wananchi kwa ccm ni mbaya sana kwa sasa. si ndani hata nje ya nchi ccm inachukiwa sana
 
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe amekitabiria ushindi chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu unaokuja.Waziri Membe amesema chama cha CDM kimetokea kupendwa na wananchi katika kila kona ya nchi na hata operesheni yao ya kusini imekitikisa chama tawala.
Waziri Membe aliyasema hayo katika chakula cha mchana alichowaandalia viongozi wa CDM nyumbani kwake waliokuwa katika jimbo lake la Mtama.Viongozi hao ni mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema,kamanda James Millya na viongozi wakuu waandamizi.
Waziri Membe aliwaambia viongozi hao ameishi nchi mbalimbali duniani zenye demokrasia ya hali ya juu hivyo hatashangazwa hata kidogo CDM kuingia Ikulu.
Kuhusu kesi iliyotengua ubunge Lema waziri Membe amedai kushtushwa na kusema kwa vile amekata rufaa anaamini mahakama ya rufaa itamrejeshea ubunge wake.

Source:Mtanzania Jumapili.

siamini kama maneno haya ni ya membe.
 
Membe ameongea yaliyo moyoni kwake. Pia, ameonyesha busara. Hata Maige ameshatoa kauli kama hii zaidi ya mara 1. Mwendawazimu Nepi ndio amebaki kichwa ngumu.
sidhani kama ni busara kwa kiongozi mwenye nafasi ya nape akiri kuwa ccm itashindwa..........ni kama mkuu wa kikosi cha kijeshi awambie wapiganaji wake kuwa watashindwa vita..........Hivyo msitegemee hata siku moja aseme kuwa ccm imechoka au itaanguka badala yake ataendelea kupambana mpaka mwisho akisubiri uchaguzi ili wananchi waamue wenyewe.
 
Hakuna cha unafiki hapo ndugu. Siasa si uadui, Chama kimoja kinatawala leo kesho kinatawala kingine.

Ila kwa ccm wakishatoka madarakani kamwe hawatorudi tena madarakani zaidi zaidi kitakufa na kikifa chonde chonde cdm msiwapokee ktk chama chenu hao mliowaweka ktk list ya mafisadi tofauti na hapo mkiwapokea tutajua mlikuwa mkiwania madaraka tu!
 
Membe ameongea yaliyo moyoni kwake. Pia, ameonyesha busara. Hata Maige ameshatoa kauli kama hii zaidi ya mara 1. Mwendawazimu Nepi ndio amebaki kichwa ngumu.

Anashindwa kuamini kwavile alikuwa na matarajio makubwa ya kufanyiwa na ccm apo baadae badala yake imekuwa isivyotegemewa
 
:A S 100::glasses-nerdy:ametishwa na kasi ya CDM huyo,alikuwa kma anawapliz CDM wamuoneee huruma:mwaaah::coffee::angry:
 
Hii habari itafanya nape apanic na kuandaa mkutano lindi na mtwara.
 
:A S 100::glasses-nerdy:ametishwa na kasi ya CDM huyo,alikuwa kma anawapliz CDM wamuoneee huruma:mwaaah::coffee::angry:
 
Back
Top Bottom