Waziri Membe abanwa Atishia kujiuzulu, serikali yafunga mjadala, Chenge safi

yawezekana labda mtuhumiwa mmojawapo ni JK mwenyewe! mbona anakazania sana kuitetea....
 
Mi nadhani muda wa kuijadili hii serikali umekwisha.Sasa ni muda wa vitendo.Nimejikuta nikijihisi kama sina akili kuendelea kujadili haya mambo.Kumbe ndo maana watu wamekuwa wakilimwa ban kwa kasi siku za karibuni.Sasa ebu naombeni ushauri,hapa nini cha kujadili?
 
Yaani wanatufanya sisi mapuruzai kweli hawa.. Wale investigators walikuwa wanafuatilia trail ya zile hela za rada baada ya kulipwa.. Wakafuatilia na kuzikuta kwenye a/c ambayo baada ya kuangalia jina wakakuta ni Bw. Chenge.. na wakaona hapo kuna nyingine zimetoka na walipozifuatilia wakazikuta kwenye a/c ambayo baada ya kuangalia jina wakakuta ni la Bw./Dr Idrissa..! Hivi hawana hata aibu wanakanusha hawajapokea rushwa kweli..? Mungu awalaani wote nyie mliochukuwa rushwa na mnaotetea.. Haya mnayotutendea watanzania wenzenu hakika mtajalipa ciku moja.. Kama sio nyie wenyewe baci ni watoto wenu.. na kama ci watoto wenu baci hata wajukuu lazima walipe kwa dhambi zenu...
Ndo maana huwa napata shida kujadili hizi,unaweza patwa na jazba mbaya sana..
 
Kama hakuna ufisadi katika hili suala la rada kwa nini Uingereza walirudisha hiyo change ya radar? Ukweli CCM na viongozi wake wanatuchezea watanzania kwa sababu ya upole na roho ya subira ili kupata maelewano. Hakika iko siku itafika (na si mbali) watanzania tutakasirika ndipo watakaposhangaa. Wenye haki wana ujasiri wa ajabu na wadhalimu wana woga wa ajabu tutaona dawa yao iko jikoni
 
Waziri Membe pole mafisadi wanataka kukuangamiza. Usife moyo simamia haki Mungu atakupigania. Kumbuka Daudi alimua goliat kwa kombeo. Wewe ni Daudi katika ufisadi huu CCM ni goliati wataanguka tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
A

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe

na Tamali Vullu, Dodoma

Waziri Membe atishia kujiuzulu

Katika hatua nyingine, Membe ametishia kujiuzulu iwapo atajitokeza mtu atakayeweza kuendesha wizara hiyo kwa bajeti ya asilimia 42. Akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hoja yake, Waziri Membe alisema wizara hiyo inapata mgao kidogo wa bajeti isiyokidhi mahitaji na katika mwaka wa fedha ulioisha wizara hiyo ilipata asilimia 44 ya bajeti iliyoombwa.

"Kama atajitokeza mtu anayeweza kuendesha wizara hii kwa bajeti ya asilimia 42 nitakuwa tayari kujiuzulu, kwani wizara hii imekuwa ikipata mgao kidogo wa bajeti, hivyo tuna changamoto nyingi," alisema.

Mheshimiwa mleta mada,

Huyo mwandishi ana lengo la kutaka kupotosha jamii kwa kuleta hiki kichwa cha habari nafikiri kwa kutaka watu wengi wakimbilie kufungua.

Anchokiema waziri Membe ni kwamba yeye ameweza kudhibiti matumizi ya wizara hiyo kwa kiasi cha asilimia 44 kwa mwaka uliopita na hata mwaka huu bajeti imepungua kufikia asilimia 42.

Sasa anasema kama kuna mtu atakuwa tayari kujikimu kwa asilimia 42 kwa matumizi ya wizara (yaani yeye tu ndio anaweza) ambapo kiasi hicho ni kidogo basi atajiuzulu.

Yaani anajiamini kwamba ni yeye tu mwenye uwezo huo wa kutumia hicho kiasi.

Huo ndio mtazamo wangu.
 
Membe bana ana hadithi za ABUNUWASI eti akipatikana mtu anayeweza kuongoza kwa asilimia 42 ya bajeti ahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa, hoja za kitoto. Bajeti inaandaliwa na kupitishwa na baraza la mawaziri kabla ya kuletwa bungeni, na mgao wote, makusanyo yote lazima baraza linapata updates kupitia waziri wa fedha na uchumi. Je, anapopewa kiasi cha 44% out of 100% kwa mwaka jana na kukubali kutumia kwa mwaka uliopita, then mwaka huu apewe tena na atumie si ni kuwa kazoea na hapa anaendeleza zile stori zake feki za nikioteshwa (akipatikana) alali yeye anatumia hicho hicho!!
Membe bana!!!!! Kwa tathmini hafai kuwa kiongozi maana ana stori za mdako, katarina njoo mvua usije.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom