Waziri Membe abanwa Atishia kujiuzulu, serikali yafunga mjadala, Chenge safi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Membe abanwa Atishia kujiuzulu, serikali yafunga mjadala, Chenge safi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Aug 7, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe

  na Tamali Vullu, Dodoma

  WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisema hakuna rushwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada kutoka nchini Uingereza, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamemkalia kooni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakimtaka awataje watuhumiwa na kashfa hiyo.

  Wabunge hao walitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa wakichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa na kwamba mbali na kutajwa kwa watuhumiwa hao pia serikali iwachukulie hatua na si kufurahia tu chenji yake ambayo imerejeshwa nchini hivi karibuni.

  Mbunge wa Viti Maalum, Rachel Mashishanga (Chadema), alisema kuwa Waziri Membe alipata kueleza anawafahamu watuhumiwa na kashfa hiyo ni vema akawataja, ili jamii iwatambue. Naye mbunge wa Gando, Khalifa Khalifa (CUF), mbali ya kumtaka Waziri Membe kuyataja majina ya watu waliohusika katika kashfa hiyo, kwani kitendo cha kutoyataja kinaashiria kuwa naye anahusika.

  “Mheshimiwa Waziri utakapokuwa unahitimisha hoja yako wataje hao waliohusika katika kashfa ya rada…usifurahie chenji ya rada, kwani huo ni udhalilishaji mkubwa kwa serikali yetu.”

  Awali, msemaji wa kambi ya upinzani wa wizara hiyo, Ezekia Wenje, alisema kambi hiyo inaendelea kuhoji ni kwa nini mpaka sasa watuhumiwa wa kashfa hiyo wanaendelea kutembea vifua mbele bila kuchukuliwa hatua zozote.

  “Mpaka sasa haieleweki ni kwa sababu gani nchi hii pamoja na kudai kuwa ina uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe iliamua kuliachia suala hili kufanyiwa kazi na serikali ya Uingereza, kuanzia uchunguzi hadi mashtaka ya kurudishwa fedha zilizotokana na rushwa ya rada ambayo sasa imebatizwa jina tamu ya chenji ya rada,” alisema.

  Wenje ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara hiyo, alisema pamoja na serikali kushindwa kufanya uchunguzi na hatimaye kuwashtaki watuhumiwa wa rada, ilipobainika kuwa inatakiwa kurudishwa chenji ya rada serikali ilikuwa mstari wa mbele kufuatilia chenji hiyo na kuipangia matumizi.

  “Tunashindwa kuelewa umakini wa serikali uko wapi, kwamba inaweza kuweka msisitizo katika kuhakikisha fedha za rushwa ya rada zinarudishwa nchini, lakini haiwezi kuthubutu kushughulikia wale waliosababisha upotevu wa fedha hizo kwa njia ya mkataba,” alisema.

  Alibainisha kuwa taarifa mbalimbali zinazotokana na utafiti wa suala hilo, zinaeleza namna wizi huo ulivyofanyika ukiwahusisha Watanzania wengine wakiwa ni viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali ya CCM na kwamba Watanzania wanashangaa watuhumiwa hao sasa wanachaguliwa kuongoza mhimili muhimu wa Bunge.

  Serikali yalazimisha kufunga mjadala

  Akijibu hoja za wabunge kuhusu kashfa hiyo ya rada, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, alisema serikali imefunga mjadala kwani hakuna rushwa katika suala hilo. Alisema, hata Uingereza iliyochunguza suala hilo imeeleza bayana kwamba hakuna rushwa na katika hatua hiyo serikali haiwezi kumfikisha mahakamani mtu yeyote.

  “Katika hali kama hii tukimpeleka mtu mahakamani na ushahidi tunaoutegemea, ni upande ule wa BAE na SFO maana huku hakuna mashahidi… sasa kule hata kumtaja mtu hauruhusuwi na serikali hii iliingia mkataba na hawa, tukisema tunataka kumwita mtu aje kutoa ushahidi huku hawatakubali,” alisema.

  “Kwa hiyo naomba jambo hili lifike mwisho hakuna rushwa katika rada ambayo inawahusu Watanzania tunaowajua,” alisema. Alieleza kuwa kabla ya kuzungumza hayo aliwasiliana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kumuuliza kama kuna kitu kipya na alimwambia hakuna anayehusika.

  Alisema kuwa alilieleza suala hilo Julai 5 mwaka jana na kudhani kuwa limekwisha, lakini anaona bado linajirudia na kusema inaonekana jambo hilo halijaeleweka kwa wananachi. “…Jamani hakuna kesi ya rada dhidi ya mtu yeyote hapa Tanzania kuhusu sakata la rada…Niliomba kama kuna mtu ndani au nje mwenye ushaidi aulete, maneno maneno mahakamani hakuna unatakiwa ushahidi unaojitegemea.

  “Sasa nikaambiwa kuna kitabu kimeandikwa na mimi nimekisoma na wale waliotajwa kama ningekuwa mshauri wao ningewashauri wamfungulie mashtaka mwandishi wa kitabu hicho maana msingi wa kitabu chake ni magazeti. Anasema fulani mwizi ananukuu This Day, fulani mwizi ananukuu The Guardian.”

  Wiki iliyopita Rais Kikwete wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema hakuna rushwa kwenye ununuzi wa rada na badala yake kulikuwa na makosa ya uchapaji. Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina, lakini kwa kauli hiyo ni dhahiri kwamba alimsafisha Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa ndani na nje ya chama chake kuhusika na kashfa hiyo kutoka Kampuni ya BAE- System ya nchini Uingereza.

  Chenge, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, anatajwa kuhusika kutoa ushauri wa kisheria wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ushauri ambao unatajwa kuzingatiwa katika hatua za uamuzi. Mwingine anayehusishwa na kashfa hiyo, ni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Idriss Rashid.

  Pamoja na hao, wanatajwa wafanyabiashara wenye asili ya India, lakini ambao wanaishi/walipata kuishi Tanzania, Tanil Somaiya, ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya uwakala wa simu ya Shivacom na Sailesh (Shailesh) Vithlani kuwa watu wa kati wa biashara hiyo. Mchakato wa ununuzi wa rada, uliwahusisha watu wa madaraka na kada mbalimbali ambao ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair.

  Blair anatajwa kuwa ndiye aliyemshawishi aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin Mkapa, kununua rada hiyo kutoka kampuni ya kutengeneza silaha ya Uingereza BAE-Systems. Wakati huo aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa, Clare Short, alikataa katakata Tanzania, moja kati ya nchi maskini kabisa duniani, kutumia sh bilioni 40 kununua rada katikati ya umaskini unaonuka.

  Waziri Membe atishia kujiuzulu

  Katika hatua nyingine, Membe ametishia kujiuzulu iwapo atajitokeza mtu atakayeweza kuendesha wizara hiyo kwa bajeti ya asilimia 42. Akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hoja yake, Waziri Membe alisema wizara hiyo inapata mgao kidogo wa bajeti isiyokidhi mahitaji na katika mwaka wa fedha ulioisha wizara hiyo ilipata asilimia 44 ya bajeti iliyoombwa.

  “Kama atajitokeza mtu anayeweza kuendesha wizara hii kwa bajeti ya asilimia 42 nitakuwa tayari kujiuzulu, kwani wizara hii imekuwa ikipata mgao kidogo wa bajeti, hivyo tuna changamoto nyingi,” alisema.

  Alisema pamoja na mapungufu hayo, wizara hiyo ambayo ni kiungo muhimu cha nchi yetu na nchi za nje imeendelea kushirikiana kwa karibu na wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi kuhakikisha nchi inafaidika kwa kadri iwezekanavyo na fursa mbalimbali zenye manufaa kwa nchi.

  Alitoa mfano kuwa wizara hiyo imeshirikiana na ubalozi wa China na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Fedha kuhakikisha nchi inapata dola bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tanzania inanuka kwa umaskini huko vijijini ndio uoza, Hivi kweli viongozi wa Tanzania ni maskini ? Inasemekana michahara ya Viongozi na mawziri wa Tanzania basi waziri wa Europe hapati good time, tuje kwa walala hoi kitumu chama cha ccm?.

  Niaibu kubwa Jinchi kama Tanzania lenye Rasilimali nyingi na ardhi yakutocha na haliyahewa mzuri kuambiwa ni nchi yenye umaskini wakuticha na katika nchi maskini Tanzania imechika Bendera Africa, yani ziko nchi nyingi tu za africa utachangaa uchumi wao lakini haziombi ombi kama aibu ya Tanzania.

  It is Shame & Sad tatizo la Tanzania ni watanzania wenyewe kuwalea viongozi mafisadi wa mamilionea na wenye utajiri wa kujilimbikizia mamali yakuticha, bado watanzania vichwa usaha tunaleana kwa mabaya na kuwadekeza wala ruswa wakubwa wa mamilionea.
   
 3. o

  oche Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  fungua attachnment cheki nani mkweli, kikwete au SFO
   

  Attached Files:

 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ushahidi ni pesa iliyorudishwa na BAE Systems baada ya kukili ku inflate price ya Rada ili kuwalainisha Chenge na Dr. Idrissa Rashid. Je, wanataka ushahidi gani zaidi ya huo? Au DPP/serikali nayo siku hizi ni mahakama inasubiri kuletewa ushahidi mezani, badala ya kuutafuta?!.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sasa kabanwa vipi? Issue hapa ilikuwa ni kutaja majina na kwa sasa majina ya watuhumiwa hao ni public knowledge hata kama kuna inadequacy katika ukusanyaji wa ushahidi. Chikawe hakuja na kitu kipya. Amekuwa na msimamo wa kutotaka kuchukua hatua hata kama kungekuwa na ushahidi. The truth will remain that kuna usanii ulifanyika na so far Chenge ameshindwa kueleza alivyopata fedha zilizokutwa kwenye akaunti yake.
   
 6. HASSAN SHEN

  HASSAN SHEN JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chenge hasafishiki
   
 7. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Simple logic, they are guilt but we cannot convict them (particularly, in the court system).
  People's power can put them into justice.
   
 8. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Sarakasi za nchi hii ni kiboko,nadhani hata shetani anashangaa ujuzi walionao viongozi wetu kwa kupindisha mambo
   
 9. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wajinga ndio waliwao. Kimsingi BAe walikuabali kuhonga ila kwa makubaliano na mahakama walikiri kosa la "kutoweka mahesabu vizuri" na kupigwa faini ikiwa ni pamoja na kurudisha "change" ya rada na mambo yaisjie hapo. Rais na Chikawe wake wanachopaswa kusema ni kwamba ni kweli rushwa ilitolewa ila kwa vile BAe amabaye angekwa shaidi number moja hatakubali kutoa ushaidi (maana kesi yao imefungwa) hivyo itakuwa vigumu Tanzania kupeleka mahakamani wala rushwa wa rada. Je kwa maana hiyo ya Chikawe Saileth Vithlani anaweza kurudi nchini kama mtu huru?
   
 10. o

  oche Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  na PCCB wlikiri kuwa chenge akutaja mali zake kama SFO walivyosema
   
 11. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hana ubavu wa kujiuzulu,anatikisa kibiriti. Mbona mwaka jana ameendesha wizara kwa fungu hilola asilimia 44 (44%)?nina uhakika hata akipata asilimia 20% ataendesha wizara hivyo hivyo.
   
 12. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  hawa viongozi wa serikali ya ccm siwatofautishi sana na genge la wezi. mwizi siku zote husema hajaiba. tangu lini mwizi akakili kirahisirahisi tu kuwa kweli kaiba? cha msingi hapa watanzania wapenda haki tujipangeni tuliondoe hili genge la wezi madarakani halafu tuwafungulie mashitaka.
   
 13. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Pum..vu anatishia kujamba akati ana tumbo la kuhara? Kutokana na kutokua na vyanzo au ukusanyaji mbovu wa pato la taifa basi serikali ya Tanzania imekua ikijiendesha kwa Deficit Budget so what anataka kujiuzuru? Afanye bila kujiuliza wala kutu-ALERT. We have a lot to take care of, haya ndio matatizo ya copy & paste image ya mtu alietangulia katika wizara hiyo.

  What the Hell ar u by the way????.... Expectations he had are fedding & he is afraid of the UNKNOWN!
   
 14. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,736
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  That called tanzania is about to vanish on earth. No mercy the foul you played is enough to burry you. This country itagawanwa vipande vipande cause onlu sukuma land existed before coloni. Mazee twafwaa yaani is a big curse. If tanzania is blessed country for that reason we have betrayed our lord the giver we have to be punished severely. Let us change unless our offspring will just pay for our bad did.
   
 15. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Yaani wanatufanya sisi mapuruzai kweli hawa.. Wale investigators walikuwa wanafuatilia trail ya zile hela za rada baada ya kulipwa.. Wakafuatilia na kuzikuta kwenye a/c ambayo baada ya kuangalia jina wakakuta ni Bw. Chenge.. na wakaona hapo kuna nyingine zimetoka na walipozifuatilia wakazikuta kwenye a/c ambayo baada ya kuangalia jina wakakuta ni la Bw./Dr Idrissa..! Hivi hawana hata aibu wanakanusha hawajapokea rushwa kweli..? Mungu awalaani wote nyie mliochukuwa rushwa na mnaotetea.. Haya mnayotutendea watanzania wenzenu hakika mtajalipa ciku moja.. Kama sio nyie wenyewe baci ni watoto wenu.. na kama ci watoto wenu baci hata wajukuu lazima walipe kwa dhambi zenu...
   
 16. B

  Bob G JF Bronze Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ushahidi huu utatumika vizuri kumtia jela Mzee wa Vijicent mara ccm itakapokuwa imeondolewa madarakani 2015, ccm wamedhamilia kuendelea kuchezea akili na mali zetu
   
 17. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Shame on you bunch of thieves ! !!!!!! protecting each other like hell ghosts.
   
 18. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Bado nitasema. Viongozi wa ccm wangekuwa wanajua mashine ya kuformat mbongo za watanzania ili ikifika 2015 tuwe tumesahau hizi sarakasi zao na kuwaona wao ni wasafi wangeitafuta kwa gharama yoyote hata kama niku tu -ULIMBOKA nusu ya population yote.

  Njia ya muongo wakati wa kukaribia ukombozi huwa ni fupi.
   
 19. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,108
  Likes Received: 7,364
  Trophy Points: 280
  Pia hakamitiki!!
   
 20. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo woteee...!
   
Loading...